Mamlaka iwaruhusu watu waende kwenye mashamba na vijiji vya karibu wakajitafutie chakula, hapa tulipo ni nyika tupu

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,885
Kutokana na ugumu wa ajira kwenye nchi hii naomba Mh Rais urahisishe mchakato wa watu kwenda nje ya nchi kutafuta ajira na kazi.

Kikwazo kikubwa cha watu kwenda nje ya nchi ni passport na masharti yake. Hili limepelekea watanzania walio nje ya nchi wawe wachache sana.

Nchi kama US kuna Watanzania kama 20,000 tu lakini Wakenya ni zaidi ya 100,000. Hapo Kenya wanajipatia fedha za kutosha kupitia Remittances.

US mbali, kuna nchi kama Congo DR nchi inayohitaji wataalamu wengi na sisi tuna hadi madaktari waliokosa kazi, ikirahisishwa namna ya kwenda nje ya nchi hawa wanaweza kwenda na nchi ikajipatia pesa. Bado manesi, mainjinia, waalimu na watu wengine kibao ambao nchi haiwezi kuwaajiri lakini wanaweza kupata kazi nje ya nchi.

Nashauri kigezo cha kupata passport iwe ni kuwa na namba/kitambulisho cha NIDA tu. Yasiwepo mambo mengine ya kikwamishaji na urasimu usio na maana. Na gharama ya passport ikiwezekana ipunguzwe. Waache watu watoke. Nchi kama Mexico inahimiza kichinichini watu wake wahamie Marekani. Wamexico wanatuma nyumbani karibu USD 36 billion kwa mwaka kutoka US. Hii ni zaidi hata ya bajeti yetu.

Wacuba wanatuma madaktari duniani kote, kuna madaktari wa Cuba Kenya, Angola na kote. Wana madaktari Venezuela na wao wakilipwa mafuta.

Waethiopia wamejaa duniani kote kusaka kazi na kutuma pesa nyumbani.

Turahisihe na kuhimiza watu kutoka nchini. Tutawanye watanzania huko Msumbiji, Malawi, Zambia, Congo, Angola na kote.

Kwanza kuweka vikwazo kwa watu kutoka nje ya nchi hakuna faida wakati huna uwezo wa kuwatumia, zaidi zaidi ni kuzidi kuchochea bomu la ajira lilipuke.

Nashauri nchi ifanye hivyo sababu sisi hatuna uwezo wa kulisha wanaume elfu tano kwa samaki wawili na mikate mitano.
 
Jamani kikwazo sio passport pekee,siku hizi tumewekwa Black/Red listed kwa maana ya kwamba ukiwa Mtanzania huruhusiwi kuingia takriban nchi nyingi duniani kwa sababu tumekataa kudeclare kwamba kuna Corona Na pia Tumekataa kuagiza Chanjo kupitia mpango wa WHO.Waislamu Watanzania Hawaruhusiwi kwenda Hijja,au Wakristo Huingii Vatican au Jerusalem.
 
Passport ni kikwazo namba moja, katika nchi hii taasisi nayoichukia kuliko zote ni uhamiaji. Jinsi nilivyopata passport inabaki siri yangu, nawajua wabongo wengi wanaamua kwenda nje hapa hapa africa bila ya passport matokeo yake hawaaminiki na wengi wao huuwawa ovyo. Passport pale uhamiaji imekua kama visa.

Wenye connection hii haiwahusu maana wao hupiga simu tu na huletewa passport hadi hwalipo. Kwa watanzania masikini watafutaji hii Migration tanzania si rafiki kwao. Mtoa mada yupo sahihi, mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa.

Ila with time i hope pale uhamiaji in 10 years hao maprimitive wakiondoka mambo yatakuja kukaa poa siku moja. Uhamiaji ni jipu kwa watu masikini.
 
Kutokana na ugumu wa ajira kwenye nchi hii naomba Mh Rais urahisishe mchakato wa watu kwenda nje ya nchi kutafuta ajira na kazi..
Passport ni kikwazo namba moja, katika nchi hii taasisi nayoichukia kuliko zote ni uhamiaji. Jinsi nilivyopata passport inabaki siri yangu, nawajua wabongo wengi wanaamua kwenda nje hapa hapa africa bila ya passport matokeo yake hawaaminiki na wengi wao huuwawa ovyo. Passport pale uhamiaji imekua kama visa.

Wenye connection hii haiwahusu maana wao hupiga simu tu na huletewa passport hadi hwalipo. Kwa watanzania masikini watafutaji hii Migration tanzania si rafiki kwao. Mtoa mada yupo sahihi, mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa.

Ila with time i hope pale uhamiaji in 10 years hao maprimitive wakiondoka mambo yatakuja kukaa poa siku moja. Uhamiaji ni jipu kwa watu masikini.
 
Upo sahihi kabisa...kingine mtu akiwa na ticket na viza asianze kukwamishwa pale airport,watu wa immigration haiwahusu kuhoji mtu eti unaenda kufanya nini huko nje.wao wagonge tu stamp yao ya exit basi.

Mataifa mengine mengi yametapakaa dunia nzima mfano Nigeria,south Africa,Us,Ethiopia,Sudan,Cameroon,China,Ghana,Egypt,Uganda nk..lakini watanzania tupo wachache sana nje yaani tunajirudisha nyuma na kufuga umasikini
 
Jamani kikwazo sio passport pekee,siku hizi tumewekwa Black/Red listed kwa maana ya kwamba ukiwa Mtanzania huruhusiwi kuingia takriban nchi nyingi duniani kwa sababu tumekataa kudeclare kwamba kuna Corona Na pia Tumekataa kuagiza Chanjo kupitia mpango wa WHO.Waislamu Watanzania Hawaruhusiwi kwenda Hijja,au Wakristo Huingii Vatican au Jerusalem.

Na jana Kigwangala kama sio juzi alitoa wazo kuwa serikali ikubali kupokea chanjo lengo nikujitoa kwenye red list ya Nchi za Magharibi ambazo kiuchumi zimekuwa na mchango katika ukuaji wa sekta ya Utalii.
 
Naunga mkono hoja.
Passport ni haki ya raia wa nchi, kwa Tz inaonekana kama dhambi kuiomba.. Na hapo tunalipia. Jamani ebu badilikeni wahausika
 
Kati ya vitu vya kijinga ni kuzuia pasiport kwa kigezo mtu awe na safari, nchi yetu imejaa wa kigeni kibao wasio nq sifa lakini sisi tunaweka masharti magumu kwa watanzania kutoka nje ya nchi matokeo yake tunakaa na rundo la watu wenye uwezo wa kufanya kazi bila kazi.
Taratibu za passport zilegezwe kwani kuwa mtanzania mwenye umri wa miaka 18 ndio kiwe.kigezo pekee
 
Na pasi ni haki ya kila raia,hili naona wengi hawalitakii
Mtu yeyote akiitaka ali mradi awe na uwezo wa kulipia na kitambulisho nida inapaswa kupewa
 
Bongo bado kuna mambo ya ajabu sana,kuweka vikwazo vingi katika kupata passport,hii ni haki ya mwananchi,kusema kwamba mpaka upate safari ndio upewe passport,ni akili za hovyo sana.Safari inaweza ikatokea wakati wowote,kwahiyo lazima mtu ajiandae
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom