Bora ingekuwa aibu hii ni fedhehaa, haja kubwa na ndogo huwa ni za siri na huwa mtu anapata kwa wakati wake, inapotokea hadharani huwa ni fedheha. Pata picha umebanwa na mkojo huna hata pa kujisetiri yaani hamna, bora wanaume wanapiga magoti hata hadharani anafungua zipu tuu aungo yake hayaonekani.
Sie akina dada ndo issue hasa ukutwe umevaa suruali au kimini kama hiko maungo yote wazi. Hii ni fedheha kwa kweli maana hata mwanaume inaweza kumtokea.
Huwa sipendi hali ambayo unakuta mtu kaenda chooni kujisaidia baada ya kujisafisha na maji anavaa nguo zake kisha anakaa kabla yale maji hayajakauka akiinuka unaona alama matakoni za maji yaani huwa sipendi kabisa.
Wakati nasoma A level shule moja ya serikali miaka hiyo ilikuwa matata sana kuna ticha mmoja aliingia darasani na mikogo kumbe katoka chooni na suruali yake matakoni imelowa maji yeye hakujua, ile amegeuka ubaoni tuu kuandika GEOGRAPHY, darasa zima tukacheka kwa nguvu akageuka kuuliza kwa kizungu, ''what is the problem''? Mvulana mmoja akamjibu Sir, ''your back is wet''. Darasa zima tulizidi kucheka kwa nguvu sasa ticha yule alikuwa anajipenda sana, sasa asitoke nje akajikague pembeni akageuka kujiangalia matakoni na kuvuta suruali kwa mbele akiwa mulemule darasani, huku wanafunzi tukazidi kucheka nakumbuka kuna mwanafunzi mmoja darasani hadi na yeye mkojo ukamtoka kwa kucheka. Nikikumbuka hili tukio huwa nacheka sana na siku hiyo hatukusoma tena Geography kipindi kiliishia hapo.
Back to the topic hiyo ni kama ajali na inawea kumpata yeyote popote alipo, kwa wanawake au wadada ni kosa kutembea bila khanga, je wanaume wakipatwa na shida kama hii wanfanyaje? wantakiwa kutembea na misuli? heheheheee just thinking aloud looh