Mama Sabrina
JF-Expert Member
- Jul 30, 2016
- 16,621
- 27,567
Hahahaahhahaah"Kasage mahindi ndo ukacheze" ukirudi unatumwa kingine mpk giza linaingia
Hahahaahhahaah"Kasage mahindi ndo ukacheze" ukirudi unatumwa kingine mpk giza linaingia
Jamani kulala mchana hivii mi sijafurahia kabisa maisha ya utoto nafurahi hivi mkubwa najiamulia mwenyeweemimi kulala mchana...nilikua sipendi na ilikua hamna kwenda kucheza hadi ulale mchana...basi nkifika room najilizaaaa hadi macho yawe mekundu af nachukua kitana nafunga kune paji la uso hadi alama itokee eti ndo mistari mistari ile ukitoka kuamka...af nakaa kidogo nasepa zangu kucheza...
Unalala mpaka sasa hivi una magari mangapi?Mimi nilikuwa sipendi kuamshwa asubuhi..utamsikia mzee anasema"wengine washaamka na kulima eka moja wameshamaliza,nyie bado mmelala tu"
HahaahahahahMdogo angu alkua anapenda sana wali sasa kila mtu na sahani yake, mama alkua akitujazia msahani mkubwa, mi nakula nabakisha cha kula na chai asubuh dogo akimaliza chake mama anachukua changu anampa, nilikua nakasirika balaa, siku moja ili kumkomoa nikamaliza chote nilivimbiwa usiku sikulala ni kugugumia tu
Mama zetu wqna maneno jamaniMi nilikuwa sipendi kutumwa dukani usiku alafu duka lipo mbali kweli maza anasema nenda kama unaliwa uliwa uliwe nitazaa mwingine
Hahaaaahaaa!!kweli!!Dingi anapewa pande kubwa la samaki, madogo mnapewa tupande tudogo tudogo
Siupendi huo wimbo kabisaaa mpaka leo huwa unanikumbusha kuamkaKuoga maji baridi, pia kale kawimbo cha amka kumekucha, nilikuwa kuwa sikapendi radio free saa 11:30am.sijui kaimba msanii gani
mzima lakini?Mama zetu wqna maneno jamani
inawezeakana hujaelewa kweli maana avatar yako yenyewe ina balimi, pengine ushazitingaKumbe ulafi na tamaa haujaanza Leo?
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:
1: Kurudi home mchana nakuta madha anachambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,
2: Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha, madha anaongea kwa sauti ya juu 'We hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo’
Duuuh, nilikuwa nakasirika vibaya! Wewe je?
hahahaahah, wanaona fahari. hahahahahahahhaMi mama ana tabia hiyo mpaka sasa hivi anapenda kutambulisha jamanii sijui wanasikia rahaa
mimi tulikuwa tunashindana kuwahi shule ya msingi na rafiki yangu siku moja nikawahi kulala saa moja nikashtuka baadae kidogo kwa kuwa nilikuwa nishavaa sale ya shule kabisa nikavaa viatu huyo nikawaacha hom wamelala mi nikasepa,
ashukuliwe yule mlevi aliyeniludisha mpaka nyumbani,ilikuwa saa tano usiku ye ndo katoka bar.
Dada wa kazi alinitesa sana kuhusu kulala mchana natandka mito naenda kucheza anakuja kunifata mbinu zote alikuwa anazijua hahaha da Happy popote ulipo nakusalimia ulinitesa sana mshenz ww
mimi kulala mchana...nilikua sipendi na ilikua hamna kwenda kucheza hadi ulale mchana...basi nkifika room najilizaaaa hadi macho yawe mekundu af nachukua kitana nafunga kune paji la uso hadi alama itokee eti ndo mistari mistari ile ukitoka kuamka...af nakaa kidogo nasepa zangu kucheza...
kuna siku niliona wanapika ugali na nyanya chungu nikasema nimeshiba ule mda wapo wanakula nikapita sebleni nikakuta tobaa!kumbe mzee aliludi na nyama choma,machozi yakaanza kutoka nikaulizwa nini nikasema kichwa kinauma nilipelekwa mpaka dispensar kuchomwa sindano za bure,nyama hajawai niacha salama