Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

Wimbo wa Sabuni ya Mshindi halafu nasikia kawimbo ka Matukio Radio Free Africa, hapo najua muda wa shule. Bas Mama anaanza kutuamsha mimi na braza, asubuh baridiiii
 
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:

1: Kurudi home mchana nakuta madha anachambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,

2: Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha, madha anaongea kwa sauti ya juu 'We hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo’

Duuuh, nilikuwa nakasirika vibaya! Wewe je?
Hahahahaaaa.. Ukweli mtupu mzee baba
 
mimi kulala mchana...nilikua sipendi na ilikua hamna kwenda kucheza hadi ulale mchana...basi nkifika room najilizaaaa hadi macho yawe mekundu af nachukua kitana nafunga kune paji la uso hadi alama itokee eti ndo mistari mistari ile ukitoka kuamka...af nakaa kidogo nasepa zangu kucheza...
Nilikuwa naliaa sanaa,eti lala ukue halaf nue unasikia wenzio wanacheza

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom