Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

Nilikuwa na zamu ya kwenda madrasa na tuition ,ikifika zamu ya madrasa nasingizia naumwa kulikuwa na viboko balaa yule maalim anachapa kweli ,kuna rafiki zangu wakawa wananipitia twende nilikuwa sipendiii
 
mimi kulala mchana...nilikua sipendi na ilikua hamna kwenda kucheza hadi ulale mchana...basi nkifika room najilizaaaa hadi macho yawe mekundu af nachukua kitana nafunga kune paji la uso hadi alama itokee eti ndo mistari mistari ile ukitoka kuamka...af nakaa kidogo nasepa zangu kucheza...
Jamani kulala mchana hivii mi sijafurahia kabisa maisha ya utoto nafurahi hivi mkubwa najiamulia mwenyewee
 
Mdogo angu alkua anapenda sana wali sasa kila mtu na sahani yake, mama alkua akitujazia msahani mkubwa, mi nakula nabakisha cha kula na chai asubuh dogo akimaliza chake mama anachukua changu anampa, nilikua nakasirika balaa, siku moja ili kumkomoa nikamaliza chote nilivimbiwa usiku sikulala ni kugugumia tu
Hahaahahahah
 
Zamu za nyumbani, kufagia uwanja, kusafisha vioo, kumwagia maua na bustani ya mboga. Unaamshwa asubuhi subuhi unafanya kazi na shule uwahi, kijeshijeshi.
 
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:

1: Kurudi home mchana nakuta madha anachambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,

2: Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha, madha anaongea kwa sauti ya juu 'We hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo’

Duuuh, nilikuwa nakasirika vibaya! Wewe je?
 
mimi tulikuwa tunashindana kuwahi shule ya msingi na rafiki yangu siku moja nikawahi kulala saa moja nikashtuka baadae kidogo kwa kuwa nilikuwa nishavaa sale ya shule kabisa nikavaa viatu huyo nikawaacha hom wamelala mi nikasepa,
ashukuliwe yule mlevi aliyeniludisha mpaka nyumbani,ilikuwa saa tano usiku ye ndo katoka bar.
 
mimi kulala mchana...nilikua sipendi na ilikua hamna kwenda kucheza hadi ulale mchana...basi nkifika room najilizaaaa hadi macho yawe mekundu af nachukua kitana nafunga kune paji la uso hadi alama itokee eti ndo mistari mistari ile ukitoka kuamka...af nakaa kidogo nasepa zangu kucheza...
 
kuna siku niliona wanapika ugali na nyanya chungu nikasema nimeshiba ule mda wapo wanakula nikapita sebleni nikakuta tobaa!kumbe mzee aliludi na nyama choma,machozi yakaanza kutoka nikaulizwa nini nikasema kichwa kinauma nilipelekwa mpaka dispensar kuchomwa sindano za bure,nyama hajawai niacha salama
 

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom