Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

kuna siku niliona wanapika ugali na nyanya chungu nikasema nimeshiba ule mda wapo wanakula nikapita sebleni nikakuta tobaa!kumbe mzee aliludi na nyama choma,machozi yakaanza kutoka nikaulizwa nini nikasema kichwa kinauma nilipelekwa mpaka dispensar kuchomwa sindano za bure,nyama hajawai niacha salama
 
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:
1:kurudi home mchana nakuta madha ana chambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,
2:Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha,madha anaonge kwa sauti ya juu'we hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo,duuu nilikuwa nakasirika vibaya, wewe je?
 
mimi kulala mchana...nilikua sipendi na ilikua hamna kwenda kucheza hadi ulale mchana...basi nkifika room najilizaaaa hadi macho yawe mekundu af nachukua kitana nafunga kune paji la uso hadi alama itokee eti ndo mistari mistari ile ukitoka kuamka...af nakaa kidogo nasepa zangu kucheza...
Utakua mkorofi wewe, hahahhah
 
1-Mimi nilikuwa sipendi kumwagilia bustani maana bustaniyetu ilikuwa karibu na barabarani sasa wasichana niliokuwa nasoma nao wananiangalia wananichekaaaa

2-Kitu kingine mzee alikuwa hapendi uende kanisani bila kuchomekea,sasa kama unalazimishwa kufungwa mkanda.Nilikuwa kama mti vile kwa jinsi nilivyokakamaa

3-Kuna siku nikatoka shule sikumkuta mama home ila nikakuta chakula mezani mapaja 2 ya kuku na wali nikajua leo maza kanitunuku msosi mzuri nikapiga yale mapaja yote na wali nikabakiza kidogo,bwana eeeh hamadi nasikia sauti ya mama inasema karibu ingieni ndani,maza kaja na wageni nakile chakula kumbe ndio alikuwa amewaandaalia,nikajiongeza nikaenda kulala kwa shangazi yangu mtaa mwingine nilirudishwa baada ya siku moja maana nilijua kifuatacho ITV ni nini
 
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:

1: Kurudi home mchana nakuta madha anachambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,

2: Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha, madha anaongea kwa sauti ya juu 'We hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo’

Duuuh, nilikuwa nakasirika vibaya! Wewe je?
 
niletee kitunguuu-- unaleta
niletee nyanya-- unaleta
niletee kisu-- unaleta
niletee maji-- unaleta
hujakaa sawa
niletee mwiko-- unaleta
hujapumzika unasikia
hebu niletee chumvi
hadi hicho chakula kiive umeshatembea zaidi ya km 10 kufata vitu tu.
Eheeee yaan sipendii hiii kitu,mi utoto wangu jamani halaf nilikuwa naonaga sipo huru kabisa
 
Mie nilikuwa nachukia mama yangu alikuwa ana tabia kwa mfano kama tunatembea naye njiani, akikutana na mtu pale alipokuwa anaanza kunitambulisha "HUYU NI MWANANGU WA 3 KUMZAA ANAITWA...."
Kuna siku alikuwa ametupanga mimi na ndugu zangu baada ya kutoka church, siku alisalisha padre mgeni, basi akaanza zake "PADRE HAWA NI WANANGU, WA KWANZA NI HUYU, WA PILI NI HUYU WA TATU NI HUY...." mie hapo hapo nikatoka nduki kukimbia kuelekea home, wakati bado angali anatutambulisha kwa father mgeni, alivyorudi nyumbani akanikuta, kilichonipata....... ngoja kwanza nitamalizia kesho

Yote kwa yote R.I.P mama yangu kipenzi
Mi mama ana tabia hiyo mpaka sasa hivi anapenda kutambulisha jamanii sijui wanasikia rahaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom