Mambo yaliyokuwa yanakuudhi nyumbani ulipokuwa mdogo...

Mdogo angu alkua anapenda sana wali sasa kila mtu na sahani yake, mama alkua akitujazia msahani mkubwa, mi nakula nabakisha cha kula na chai asubuh dogo akimaliza chake mama anachukua changu anampa, nilikua nakasirika balaa, siku moja ili kumkomoa nikamaliza chote nilivimbiwa usiku sikulala ni kugugumia tu
uchoyo mbaya sana
 
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:
1:kurudi home mchana nakuta madha ana chambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,
2:Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha,madha anaonge kwa sauti ya juu'we hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo,duuu nilikuwa nakasirika vibaya, wewe je?

Hiyo ya kuosha vyombo kumbe umetukuta wengi aisee
 
Mimi nilikuwa nakereka kwa mambo haya:
1:kurudi home mchana nakuta madha ana chambua mboga halafua ananiambia nikawashe jiko na inabidi nirudie shule,
2:Anapita home msichana tunayesoma naye darasa moja hata sijamwongelesha,madha anaonge kwa sauti ya juu'we hivi leo si ndio zamu yako kuosha vyombo,duuu nilikuwa nakasirika vibaya, wewe je?
Kuwa mzoa ma.vi ya kuku arafu wageni wakija wanachinjiwa watoto tunapewa miguu na shingo.
 
Kaz za nyumbani zilinifanya nipende shule yan wek end nilikua naona kama mwez . Nilikua cpend tufunge shule kwa kweli mzee wetu alitufanya tusipende hom hata tukisafili tunaomba mungu tubak uko uko. Dah
 
Unapewa kipande kimoja cha nyama unakishikilia mkono wa kushoto huku wa kulia ukikata mitonge; hukitafuni hicho kipande hadi ushibe ugali.

Ukishashiba ugali unakaa pembeni unaanza kukusurubu kile kipande; ukimaliza kukila ukijicheki mkono huo uliokuwa umeshika hicho kipande cha meat unakuta kuna michirizi ya michuzi hadi kwenye kiwiko.
 
Wenzangu wamekuja kunipitia home nikacheze chandimu/sodo/sambisambi, Mzee ananituma niende mashine kukoboa na kusaga. Nilikuwa namuona Mzee ni katili sana..
 
Wenzangu wamekuja kunipitia home nikacheze chandimu/sodo/sambisambi, Mzee ananituma niende mashine kukoboa na kusaga. Nilikuwa namuona Mzee ni katili sana..
hakuna kipindi kinaudhi kama kiangazi cha kupiga mahindi hapo hata kama ulikuwa hupendi ile twisheni ya mathe ya jioni school utaipenda tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom