Mambo ya watanganyika ndiyo ya watanzania? Ya wazanzibar yana msimamizi maalum. Kuna mtu anakula bila kunawa hapa

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
2,060
4,352
Sifahamu iwapo naeleweka vizuri. Kama nitakuwa nje saana mtaniwia radhi. Kuna mambo yananipa kuchanganyikiwa na nisijue lolote!

Mambo ya wazanzibari, yanasimamiwa na serikali ya Zanzibar na yanakuwa ya wazanzibar kwa sababu serikali yake ipo inayasimamia!

Mambo ya watanganyika hayana msimamizi wake maalumu yanasimamiwa na serikali ya Tanzania na yanakuwa ya watanzania kwa kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar kwa sababu Tanganyika inakuwa ni kama imefungiwa mahali.

Hapa kuna mmoja anakula bila kunawa aisee.
 
Ipo wazi hiyo mkuu, nchi yetu hii Tanganyika haina mwenyewe na hata akipatikana tunayeweza kusema huyu ndiye ni hatakiwi na wenyewe.
 
Ndiyo unamwona leo, halafu anawasimanga wanaompa chakula
 
Baba Tanganyika alifanya kosa kumuoa mwanake asiyempenda na kumthamini. Haya tunayoyashuhudia ni maafa na misiba kwa sababu ya kumng'ang'ania asiyempenda wala kumjali.

Watoto wanabaki kulia na kuchanganyikiwa wasijue la kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…