Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
Wengi wamesikia kuhusu kauli ya Nape akiwa Bungeni akilalamika na kufoka kuhusiana na kauli ya Tundu Lisu aliyoitoa, akimtaja Rais Samia ni Mzanzibari. Hoja aliyoisimamia Nape ni kule kumwita Rais Samia ni Mzanzibari. Kwa kauli ya Nape, inamaanisha kumwita mtu Mzanzibari ni tusi, ni ubaguzi na ni fedheha. Ni ajabu kubwa sana! Na huyi naye eti ni kiongozi!!
Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi, na wananchi wake wanaitwa Wazanzibari, na Wazanzibari wenyewe wanaonea fahari kujiita Wazanzibari, na wana vitambulisho vyao vya Mzanzibari. Leo Nape anaona mtu kuitwa Mzanzibari ni ubaguzi na ni tusi. Na huyu ni waziri!! Fikria tuna waziri wa kiwango cha namna hii.
Hakuna mtu mwenye akili timamu, hata Rais Samia mwenyewe, anayeweza kukana kuwa Rais Samia ni Mzanzibari. Na hata nafasi aliyo nayo aliipata kwa sababu ni Mzanzibari. Katiba ya JMT inatamka wazi kuwa kama Rais atatoka upande mmoja wa Mwungano, makamu wake atatoka upande wa pili. Maana yake ni kwamba kama Rais wa JMT atakuwa Mtanganyika, Makamu wake atakuwa Mzanzibari. Na ile katiba ya Zanzibar inatamka kuwa ili mtu kuwa na sifa ya kugombea urais wa Zanzibar, ni lazima mtu huyo awe Mzanzibari.
Ubovu wa katiba yetu, usiwafanye watu kukosa hata yale maarifa ya kawaida. Ni ukweli ambao Watanganyika na Wazanzibari, wote wamekuwa wakiusema na kuulalamikia. Watanganyika wamekuwa wakisema wazi kuwa muundo wa Muungano wetu ni mbaya kwa sababu baada ya Muungano, Zanzibar imeendelea kuwa nchi na Serikali yake, huku Tanganyika ikivipoteza vyote. Lakini upande wa Zanzibar, wamekuwa wakilalamika kuwa japo Tanganyika kinadharia imekufa ila bado ipo ikiwa imejivika koti la Muungano.
Hatuwezi kubakia tunawalalamikia Nyerere na Karume kuwa walitutengenezea Muungano wenye utata. Kufanya hivyo ni kuthibitisha kuwa sisi sote tunaoishi sasa hatuna akili wala maarifa ya kuweza kurekebisha au kuboresha chenye kasoro. Hiyo ni sawa na kusema kuwa Watanzania wote hawana akili, waliokuwa na akili ni Karume na Nyerere tu. Jambo ambalo ni uwongo, upuuzi na ujinga wa kiwango cha hali ya juu. Waasisi wa Muungano waliamini kuwa watakaofuatia watakuwa ni watu wenye maarifa ambao wanaweza kuboresha, kurekebisha na hata kuufuta Muungano, wakiona ni lazima:
Karume alisema kuwa Muungano ni kama koti, likikubana unalivua. Kulivua koti alikokumaanisha Karume, ni kujivua kwenye Muungano, yaani kuua Muungano.
Nyerere alisema kuwa amekuwepo madarakani kwa muda mrefu. Kuna mazuri alifanya lakini pia kuna makosa alifanya. Tena alihoji kuwa wao wasifanye makosa kwani ni malaika? Akasema kuwa kinachosikitisha ni kuona watu wanayaacha yaliyokuwa mazuri, wanayachukua mabaya.
Yawezekana waziri Nape anaishi kwa kukariri. Anapofanya hivyo atambue kuwa kuna binadamu wamezaliwa ni wakweli wa nafsi zao, kamwe hawawezi kukubali kuwa wanafiki au wakaiita spade ni kijiko kikubwa. Katika watu hao, kwa nchi yetu TUNDU LISU NI NAMBA 1. Na tuna haki ya kumshukuru Mungu kwa kutupatia watu wa namna hiyo japo ni wachache sana, tena wakiishi katikati ya kundi kubwa la watu waongo na wanafiki.
Ni ukweli usiopingika kuwa muundo mbaya wa Muungano wetu, na katiba mbaya, ndiyo vinawezesha Wazanzibari kuwa marais wa Tanganyika, wakati hakuna Mtanganyika anaweza kuwa Rais wa Zanzibar. Na hili haliwezi kuwa na faraja kwa upande wowote wa Muungano, na hakika mambo kama haya yatazidi kuudhoofisha Muungano siku baada ya siku badala ya kuuimarisha. Na wanaochangia sana kwenye hili ni hawa viongozi wanafiki na waliokosa maarifa.
Tumwombe Mungu azidi kuwabariki, kuwalinda na kuwapa ujasiri zaidi wale wenye uwezo wa kuunena ukweli bila ya kuupindisha.