Mambo ya kuzingatia katika Kudhibiti Mbu waenezao Malaria, Uchunguzi wa Ugonjwa na Tiba sahihi ya Malaria

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Mambo muhimu juu ya udhibiti wa Mbu waenezao Malaria kwa njia za Utangamano;​
  1. Matumizi sahihi ya Vyandarua vyenye dawa kwa kila mwanajamii kila siku​
  2. Upulizaji viuatilifu ukoko kwenye kuta ndani ya nyumba ni njia fanisi ya kuua mbu waenezao malaria na hivyo kupunguza maambukizi ya malaria​
  3. Upulizaji viuatilifu ukoko ndani ya nyumba hauleti wadudu wengine​
  4. Udhibiti wa mazalia ya mbu unahusisha kunyunyizia viuadudu vya kibailojia kwenye mazalia ili kuua viluwiluwi ambavyo baadaye vitakuwa mbu kamili wanaoeneza malaria​
  5. Uangamizaji wa viluwiluwi ni njia salama na fanisi ya kuzuia malaria. Husaidia kupungua kwa mbu waenezao malaria na hivyo kupunguza maambukizi ya malaria katika jamii​
  6. Udhibiti wa mbu waenezao malaria katika jamii ni jukumu la kila mtu​
  7. Wanajamii wanapaswa kuchukua hatua sahihi na rahisi ili kubadilisha na kutunza mazingira yanayozunguka nyumba zao na hivyo kuzuia na kuondoa mazalia ya mbu​
  8. Serikali za Mitaa zina wajibu mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa utunzaji wa mazingira katika kupanga, kuweka sheria na kuhusisha jamii na wadau wengine​
1702381948047.png

Mambo muhimu juu ya Uchunguzi wa Ugonjwa na Tiba Sahihi ya Malaria​
  1. Ni muhimu kutambua mapema dalili za malaria na kwenda kwenye kituo cha kutolea huduma za afya ili kupata matibabu ndani ya saa 24. Kuchelewa kutafuta tiba dhidi ya malaria kunaweza kusababisha kupata malaria kali ambayo inaweza kuwa ngumu kutibu na kupoteza maisha​
  2. Gharama za kutibu malaria sio kubwa ikilinganishwa na kumpoteza mtu kutokana na malaria​
  3. Vipimo vya malaria vinapatikana katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya​
  4. Sio kila homa ni malaria, nenda kapime kabla ya kutumia dawa, amini matokeo ya vipimo na usitumie dawa za malaria kama matokeo ya vipimo yanaonesha huna malaria​
  5. Kiwango cha maambukizi cha ugonjwa wa malaria kinapungua, hivyo si ajabu kuona watu wakipima na kupata matokeo yanayoonesha hawana ugonjwa wa malaria​
  6. Watoa huduma wahakikishe wagonjwa wenye dalili za malaria lazima wafanyiwe vipimo ili kupata uthibitisho wa uwepo wa vimelea vya malaria na wazingatie miongozo ya Wizara ambayo inaelekeza kutibu baada ya kupata uthibitisho wa vipimo​
  7. Watoa huduma watatafute chanzo kingine kinachosababisha homa pale ambapo kipimo cha malaria kimeonesha hakuna malaria na watoe matibabu inavyotakiwa​
  8. Wagonjwa wa malaria watumie dawa zilizoidhinishwa na wahakikishe wanakamilisha dozi ya dawa kulingana na maelekezo ya mtoa huduma ila wapone​
  9. Dawa zilizoidhinishwa kutibu malaria zina uwezo mzuri na zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani na Wizara ya Afya​
  10. Vifaa, vifaa tiba na dawa za malaria zinagizwe kwa wakati na kwa kiasi kinachotakiwa na upelekaji wake katika vituo vya kutolea huduma za afya ufanyike kwa wakati na kwa kuzingatia kiasi kilichoagizwa​
1702383995370.png

Pia soma:
- Fahamu Tiba Kinga ya Malaria kwa Wajawazito

- Ujue Ugonjwa wa Malaria: Dalili, Madhara, Kinga, Tiba, Malaria kwa Wajawazito na Mpango wa Serikali katika kuzuia Malaria
 
Maelezo ni mazuri ila hayanisaidii kupata ufumbuzi kwa hizo dawa za kunyunyuzia hazipo kwenye maduka ya pembejeo za kilimo, pia niliwahi kusikia kuna dawa inatengenezwa Kibaha nayo pia haipo madukani na sijui nitaipata wapi.
Upulizaji wa hiyo dawa ya ukoko ni deal kwa watu wa halmashauri hivyo usitegemee upatikanaji wake uwe rahis
 
Shuguhuli zote hizi za udhibiti wa mmbu wa malaria ni za maafisa afya mazingira,cha ajabu mnalazimiaha wasimamizi wa vitengo vya udhibiti mmbu wa malaria viwe chini ya daktari,hapo mtegemee kufeli kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.
 
Mashariti magumu sana hayo mzee, mimi huwa nachoma au kutumia ya spray nafunga madirisha na mlango baada ya muda naingia kulalaa
 
I don’t think chandarua ni solution Kuu la taifa only killing mazalia ya mbu ndio permanent sio biashara zenu za dawa ya mbu na vyandarua
 
Back
Top Bottom