Fahamu Tiba Kinga ya Malaria kwa Wajawazito

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Wajawazito wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa wa Malaria katika Jamii. Dawa ya SP hutolewa kukinga madhara ya Malaria kwa kuua vimelea vinavyojificha kwenye kondo la nyuma.
TIBA KINGA YA MALARIA KWA WAJAWAZITO (SP)
Malaria wakati wa ujauzito ni hatari zaidi kwa mama na mtoto aliye tumboni mwake. Tiba kinga wakati wa ujauzito, matumizi ya vyandarua vyenye dawa pamoja na tiba sahihi pale mjamzito anapougua malaria ndizo mbinu zinazoainisha kuwa na ufanisi katika kujikinga dhidi ya malaria na madhara yake wakati wa ujauzito

Tiba Kinga kwa kutumia dawa ya SP hutolewa kwa vipindi wakati wa ujauzito. Mjamzito anatakiwa apate dozi 3 au zaidi katika kipindi chake chote cha ujauzito.

Tafiti zinazonesha kuwa idadi kubwa ya Wajawazito wanachelewa kuanza mahudhurio ya Kliniki na hivyo kusababisha kutomaliza dozi zote za tiba kinga zinazotakiwa kwa mjamzito.

Madhara ya Malaria kwa Mjamzito
Malaria wakati wa ujauzito huweza kusababisha madhara yafuatayo;​
  • Upungufu mkubwa wa damu mwilini​
  • Mimba kuharibika​
  • Kujifungua mtoto njiti au mtoto mwenye uzito pungufu (Chini ya kilo mbili na nusu)​
  • Kujifungua mtoto mfu​
  • Afya ya Mama kudhoofika​
  • Kifo huweza kutokea kwa mama na mtoto​
1702378572504.png

1702378636095.png


UJUMBE MUHIMU JUU YA TIBA KINGA YA MALARIA KWA WAJAWAZITO
  1. Wajawazito wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa malaria kuliko watu wengine kwa sababu mwili wa mjamzito unapungua nguvu ya kupambana na magonjwa​
  2. Vimelea vya malaria vinaweza kujificha kwenye kondo la nyuma la mama na hivyo kuathiri ukiaji wa mtoto ingawaje mama anaweza kuonekana mwenye afya​
  3. Kwa sasa inashauriwa kutumia dozi tatu au zaidi za SP wakati wa ujauzito ili kuzuia maambukizi ya malaria kwa mama na mtoto aliye tumboni​
  4. Ugonjwa wa malaria wakati wa ujazito unaweza kusababisha mtoto kuzaliwa na uzoto mdogo au mimba kuharibika​
  5. Weka wazi hali yako ya ujauzito na wahi Kliniki ili uweze kupata huduma stahiki za pamoja zinazotolewa​
  6. Wajawazito wafuate ushauri na maelekezo ya mtoa huduma za afya​
  7. Huduma ya Tiba Kinga dhidi ya Malaria kwa Wajawazito kwa kutumia SP hutolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya bila malipo​
1702379509341.png

Pia Soma:

 
Back
Top Bottom