Baba wa Kiroho

Baba wa Kiroho

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
7,654
Reaction score
19,654
1000008628.jpg


Moja ya maana ya Baba wa kiroho ni mtu ambaye Mungu amemweka katika maisha yako ili kukuongoza, kukufundisha, kukuombea, kukurekebisha na kukusaidia kukua kiroho.

Sio kila mtu mkubwa au mhubiri maarufu ni baba wa kiroho.

Baba wa kiroho huwa na uhusiano wa kweli katika malezi na uwekezaji wa kiroho katika maisha yako. Haishii kukuona kanisani tu, anakulea na anabeba mzigo wa maisha yako mbele za Mungu.

Kanuni za Baba wa Kiroho:
Anakuombea.
Anakulea.
Ni msiri.
Ni mnyenyekevu.


LAKINI UKWELI MCHUNGU NI WANAWAKE WENGI KUHARIBU NDOA KWA SABABU YA "BABA WA KIROHO"

Wanawake wengi leo wameharibu ndoa zao kwa sababu wamemweka baba wa kiroho mbele kuliko mume.

Mikesha kila siku na maombi ya mara Kwa mara huku nyumbani mume na watoto kusahaulika.

Mwisho wa siku, baba wa kiroho anachukua nafasi kubwa katika familia.

Hii husababisha Mume wa kweli kuchoka, na kuondoka kwa amani. Ndiyo maana wanaume wengi leo wanasema bora kubaki single.

Baba wa kiroho wa kweli anakujenga Kiroho na kuimarisha ndoa Yako. 😊

1000008629.jpg
 
😅😅😅😅Jamani.
Hajamwibia mtu kiukweli.
Hajalazimisha watu kumuamini.
Yani anawakusanya tu kama manyumbu na nyie mnakubali et anawafungulia milango ya ridhiki,anaondoa vvu,anaondoa mapepo,anarudisha nyota....nk

For real jamaa anajua dark psychology kwa kiwango cha juu sanA
 
Siku nikute kwenye simu ya mkewangu ana namba ya mtu kama IPM amem-save baba wa kiroho.
..
Kumama anaondoka siku hiyo hiyo kwao
 
Siku nikute kwenye simu ya mkewangu ana namba ya mtu kama IPM amem-save baba wa kiroho.
..
Kumama anaondoka siku hiyo hiyo kwao
Mbona mna hasira hivo na hao watu jamani 😅
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom