Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Sasa Makamba is gone does that mean kwamba Tambwe Hizza ndiyo mwisho wake pia au inakuwaje ?
 
Mbona mafisadi papa, EL & RA, bado wanaendelea kupeta tu? Au kujivua gamba ilikuwa ni kujikoroga tu kwa kumbanjua bwana marope tu?
 
alifanya madudu pale wizara ya afya alipoondoka walifurahi waulizeni watu wa wizarani ikabidi aletwe mama Nyoni kuweka mambo sawa hadi sasa mama Nyoni anahangaika na madudu yake ,Je CCM ataiweza ? pia ni mshikaji sana wa JK kama kawaida yake ushikaji mbele

Niliwahi pata nyepesi kwamba wakati huyu bwana mukubwa akiwa katibu mkuu afya, aliwahi kwaruzana na 'nguli' moja pale wizarani ambaye aliaminika kuwa mtu wa system... kilichotokea ni kwamba mmoja alimwaga mboga na mwingine akamwaga ugali, wote wakang'oka; Mukama akapelekwa jiji mwingine sikumbuki alitupwa wapi...
 
Ni bora tuvute subira tuone jinsi atakavyoweza kuvivaa viatu vipya vya ukatibu mkuu ni mapema kumpa hukumu.
 
JF kuna mambo, ndio kusema nikiwa Rais mnaweka hapa hadi barua za mapenzi nikiwa secondary, mtataja ma ex boyfriends, ex husbands, ex girlfriends, memo zote nilizopigwa kazini, miradi yangu yote iliyofail, F zote zilizo kwenye transcript yangu nk.

Bora nijiweke pembeni mapema.
 
nakubaliana kiasi flani na ndugu fairplayer. Lowasa pamoja na ujambazi, unyang'au ni mtu anaediriki.ana uthubutu wa kimaamuzi,kama alikosea ktk mambo kadhaa ni ubinadamu tu. hakuna mtu aliekamili. jamaa mwizi lkn mtu wa kazi sana na anawezesha vtu kwenda. watumishi wengi tu wa serikali walikuwa wanamwogopa enzi zake sio leo wakati wa pinda ambae akikuta uozo anaanza kulia badala ya kuchukua hatua firm. to me lowasa hata akiwa presidaaa 2015 sawa tu!!
Huyu pinda aliokotwa wapi na ni zao la nani? kapewa rungu la kuulia kabla ya kuua analia kwanza asaidiwe kuua anajiliza kinafki.. pia mie simuamini tena kwani ni Muongo anadanganya hadi Bunge..
 
- Mukama a great man and good leader, one of CCM's long time behind the scene propangandists, loongtime Chuo cha Kivukoni, my very close loongtime friend, and with Kinana it means only one thing, the end of Mafisadi.

- Alikuwa ni Mukama, aliyegundua ubadhirifu wa ajabu sana uliofanywa Jiji na kumuarifu Rais no wonder aliyetoka huko mlo ukaisha! This is great change for CCM, isipokuwa ni mapema sana kutabiri what it means to Taifa, lakini with Kinana ninaamini this to be the end of Mafisadi.

FMeS!

kuna mtu anapingana na wewe, anasema Kinana ni mtu anayependa pesa sana, na hajali anatumia njia ipi kuipata!
 
Kama haya ni ya kweli, basi CCM haina shukrani. Makamba kawapigania siku zote! Alikubali kupakwa matope ya chama akabaki nayo ili chama kinusurike! Eti kaondoka kirahisi hivyo? Makamba usijali Mungu atakulipia!
CCM imepata a political technocrat.

Mtu anayeweza kuendesha chama kwa misingi ya kiitikadi na kukubalika kwa wananchi.Kwa kumteua Mukama CCM haijakosea, huyu ni mtu ambaye aana uzoefu wa kucheza chess ya kisiasa.
Niliwahi kusema huko nyuma kuwa masikini Makamba, he is neither a political analyst. nor a thinker or a strategist!!!

Na aliteua watu uozo kama Tambwe Hizza-Hadija Kopa wa kisiasa-watu wa mipasho badala kupata ya watu wenye uwezo wa kufikiri na kupanga.

Ukimlinganisha na aliyemuachia ofisi , Philip Mangula, ni wazi kuwa alikuwa akipwaya katika idara zote, funga kazi ni madudu ya uchaguzi wa 2010.

JK hajafanya kosa kumwomba Makamba akae pembeni kwani hata yeye(JK) nafasi yake ilianza kupwaya vibaya kutokana na madudu ya chama-yeye akiwa mweyekiti.

Wana CCM-maslahi wamemtumia vilivyo Mzee Makamba, hili liko wazi.

Kiitikadi kuondoka kwa Makamba ni upepo na harufu nzuri kwa uhai wa Chama.

Si wengi watakao mlilia Makamba. ila wale waliofaidika kimaslahi kwa yeye kuwepo pale kama katibu mkuu.
 
Viongozi wasio kwenye makundi yeyote, wachapa kazi na wenye uchungu wa nchi ndio wanaweza kutufaa mwaka 2015 kutuongoza.
Kiongozi kama Lazaro Nyalandu- naibu waziri wa viwanda na biashara anasifa na anafaa kuongoza nchi akigombea kwa chama chochote atapeta na hana mpizani...!
 
niliwahi pata nyepesi kwamba wakati huyu bwana mukubwa akiwa katibu mkuu afya, aliwahi kwaruzana na 'nguli' moja pale wizarani ambaye aliaminika kuwa mtu wa system... Kilichotokea ni kwamba mmoja alimwaga mboga na mwingine akamwaga ugali, wote wakang'oka; mukama akapelekwa jiji mwingine sikumbuki alitupwa wapi...

wewe hukumbuki kitu/vyote...mukama katoka ukatibu mkuu afya kaenda maji..huwezi kukumbuka kurudi jiji haikutokea KINYUME..INAWEZEKANA HABARI YOTE UMETUNGA TU
 
Viongozi wasio kwenye makundi yeyote, wachapa kazi na wenye uchungu wa nchi ndio wanaweza kutufaa mwaka 2015 kutuongoza.
Kiongozi kama Lazaro Nyalandu- naibu waziri wa viwanda na biashara anasifa na anafaa kuongoza nchi akigombea kwa chama chochote atapeta na hana mpizani...!

yani post yako ya kwanza unatumia kumnadi mtu kwa urais!
 
huyu mkama anatoka jimbo la mwibara wilayani bunda mkoani mara. ni msomi mzuri maana namfahamu personally. anaweza kuisaidia ccm kuendeshwa kisayansi kwasababu ni mtu aliyekomaa kisiasa na kiitikadi. huyu bwana amewahi kufundisha chuo cha ccm wakati ule kikiitwa chuo cha chama kivukoni. amewahi pia kuwa mkuu wa wilaya,nakumbuka ilikuwa ni wilaya ya dodoma vijijini kwa muda mfupi. baadaye akawa mkurugenzi wa jiji la dar, baadae naibu katibu mkuu tamisemi, na alistaafu utumishi serikalini almost miaka miwili iliyopita akiwa katibu mkuu wizara ya afya. ni mwelewa na he is politically and ideologically mature. Mashaka yangu ni kama anaweza kwenda na kasi ya mabadiliko ambayo inabidi ccm iadopt.he looks a bit conservative, probably due to his age. Remember he is in sixties. Apunguze pia jazba maana kuna wakati zinaiba logic yake hasa anapokuwa katika mijadala moto. otherwise tumpe muda, time will tell.
 
Mukama wa Musoma ni mjita na hana tofauti na Wassira kwa tabia yake yake ya ubabe....
 
CCM imepata a political technocrat.

Mtu anayeweza kuendesha chama kwa misingi ya kiitikadi na kukubalika kwa wananchi.Kwa kumteua Mukama CCM haijakosea, huyu ni mtu ambaye aana uzoefu wa kucheza chess ya kisiasa.
Niliwahi kusema huko nyuma kuwa masikini Makamba, he is neither a political analyst. nor a thinker or a strategist!!!

Na aliteua watu uozo kama Tambwe Hizza-Hadija Kopa wa kisiasa-watu wa mipasho badala kupata ya watu wenye uwezo wa kufikiri na kupanga.

Ukimlinganisha na aliyemuachia ofisi , Philip Mangula, ni wazi kuwa alikuwa akipwaya katika idara zote, funga kazi ni madudu ya uchaguzi wa 2010.

JK hajafanya kosa kumwomba Makamba akae pembeni kwani hata yeye(JK) nafasi yake ilianza kupwaya vibaya kutokana na madudu ya chama-yeye akiwa mweyekiti.

Wana CCM-maslahi wamemtumia vilivyo Mzee Makamba, hili liko wazi.

Kiitikadi kuondoka kwa Makamba ni upepo na harufu nzuri kwa uhai wa Chama.

Si wengi watakao mlilia Makamba. ila wale waliofaidika kimaslahi kwa yeye kuwepo pale kama katibu mkuu.

Are you serious? Kuna wanaojali watanzania ndani ya hili shirika la majasusi? Pole kwa kuwa na hope ya ccm na ufisadi wao. Jitihada zako elekeza mahali unapojua kuna hope sio ulioyaona. Hujui historia ya ccm na unamategemea itatoka shimoni ili wakutawale tena. Please man.
 
Huyu alishawahi kuwa katibu mkuu wa wizara ya maji na afya katika vipindi tofauti vya serikali ya awamu ya nne
 
Back
Top Bottom