Holly Crap.
Hakuna kujivua gamba bali hapo ni kupaka rangi gamba. Hao watu mnaosema kuwa mmewasafisha bado wako ndani ya chama. Walitakiwa kuvuliwa madaraka, uanachama na kufikishwa mahakamani kwa kusababishia Taifa hasara.
Hilo game CCM inalocheza linaitwa MDAKO 2.0, unaondoa vi-mawe kwenye kijishimo halafu unavirudisha tena kwenye kijishimo kwa staili tofauti ya vidole. Huwezi kutuambia kuwa umesafisha chama wakati unamrudisha Zakia Meghi (Mama Mkwe), Kinana ambaye naye ana gamba lake analotakiwa kulivua, Lowassa bado anashikilia Kamati nzito ya Bunge, fisadiz wengine bado ni wabunge na wanachama wa CCM. Na visadi mkuu bado anawatambia kuwa vita ndo imeanza. Kazi kwenu.
CCM wameshindwa kujitakasa, wasubiri Tsunami ya ndani kwa ndani.