Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Kusema kuwa CCM imejitakasa sasa ni sawa na kukiri kuwa tatizo la CCM alikuwa Makamba, which is not. Makamba aliingia katika mtandao uliokuwepo kabla yake tena kama wapo walionufaika na huo mtandao makamba si mmoja wao. Kwa hiyo mabadiriko ya kweli bado hayajaonekana labda tusubiri halmashauri kuu ya taifa kama itacheua lolote, so far, gamba liko pale pale.

Kurekebisha muundo na kuifanya sekretarieti kuwa ya watu wasio na majukumu mengine, ni jambo zuri. Jambo baya ni kuwa sekretarieti hii haina meno ya kung'ata. Hii sekretarieti ilitakiwa iwe ndo miwani inayoangalia mambo yanavyoenda serikalini na kuwang'oa wale wote wanaokwenda kinyume na maadili ya chama. Sekretarieti ikiwa na meno hayo halafu ikawa nje ya serikali tunaweza kuamini kuwa itaisadia serikali kuona kile ambacho wananchi wanakiona ila serikali haikioni. Kwa majina yaliyokwisha tajwa kuwa ndo wahusika wa hiyo sekretarieti mpya, hatuioni sekretarieti ikimsaidia rais kuisafisha serikali kwa kuwaondoa wale ambao hawafai.

Kumbuka CCM ilipotea mwelekeo pale ilipoamua kuwa ndani ya serikali na serikali ndani yake. Mambo yalikuwa yakienda kutegemea usafi wa watu fulani tu lakini si kwa kufuata "principles". Sasa wale watu walipoondoka, matatizo ya kukosa principles yakaanza kuwa wazi kuwa sasa chama hakitafika mbali. Sasa hivi kiongozi haondoki madarakani kwa makosa ya kiutendaji au ukosefu wa maadili. Kiongozi anaondoka kwa kuwa walioingia si mtandao wake, hilo ndo tatizo. Ndo maana ufisadi umekuwa ndo "modus operandi" na chama kikishuhudia na kupata kigugumizi kifanye nini.

Sasa kazi kubwa iliyopo mbele ya CCM ni kuipora ajenda ya kupambana na ufisadi na kuifanya ya kwake. Mtanziko au dilemma iliyopo ni je CCM hii inaweza kuifanya kazi hiyo? Wananchi wanauona ufisadi serikalini, kila mahali. CCM iliamua kuwa kupambana na ufisadi ni ajenda ya wapinzani wao haiwahusu kwa sababu hawauoni ufisadi! Hapo ndo tunaposema CCM lazima ife. Kwa sababu haiwezi kupambana na ufisadi bila kuukata uti wa mgongo wa CCM yenyewe kwani iko compromised centre, left and right!!

Hatuna sababu yoyote ya kushangilia kufukuzwa kazi kwa Makamba tu. Mhimili wa maovu (axis of evil) ndani ya serikali bado unapeta na ufisadi utaendelea kuisumbua serikali hii nyuma na mbele! Tusubiri tuone.
 
Naomba kuwa mtu wa kwanza kumsihi mpiganaji aliyeko wrong ground bwana nape nnauye asije kulipiza kissasi kwa uvccm ambao wamekuwa wakimpinga na kutaka afukuzwe uanachama wa jumuiya na chama.

Namsihi kufuatia uteuzi wake wa kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama hivyo kupelekea kuwa bossi wa uvccm
 
Wanajf

Baada ya kufanya kazi kubwa ya kukisafisha Chama sasa hivi kinaanza kumeremeta

Nakumbushia mkoa wa DAR es salaam kuandaa maandamano makubwa ya kumpokea na kumpongeza

Hata wanaJF wenye mapenzi mema na JK na MUkama kuwapa nguvu maana TANzania inazaliwa upya

Tumpongeze kwa lipi kama mlikuwa mlitualaumu tuliposema kuwa anawakumbatia wanaokiharibu chama? mnataka msifiwe lakini kukosolewa hamtaki
 
Umbea wenu tu nani aliwaambia nyoka akivua gamba anakuwa njiwa?
Au mmejisahau.....nahisi bado mnausingizi, acha ni waamshe CCM, CCM! CCM Eeeh!. Ngozi mpya sumu ileile au mnasemaje WanaJF.
 
Ni Zakhia huyu huyu aliwapangia watoto wake na marafiki zake waarabu vitalu mpaka kwenye hifadhi za taifa zinazomilikwa na TANAPA aliuza mpaka eneo la asili la wahazadbe,yeye ndio aliruhusu fedha za EPA zikasaidie uchaguzi kwa wana CCM ukumbuke kwenye enzi zake walikubaliana kila mwanaCCM aliyetaka kugombea angepewa millioni 25 zikaisihia na zikaleta manuq'uniko mengi sana
 
kama mm ndo nape, kwanza naanza na hao uvccm nawafunga midomo af then naenda kwa mizee na yenyewe naipa onyo kali itulie tujenge chama 2015 turudishe ushindi wa elninyo
 
nami nitakuja kwenye hayo maandamano.. kibali kimepatikana polisi..?
 
Umbea wenu tu nani aliwaambia nyoka akivua gamba anakuwa njiwa?
Au mmejisahau.....nahisi bado mnausingizi, acha ni waamshe CCM, CCM! CCM Eeeh!. Ngozi mpya sumu ileile au mnasemaje WanaJF.

Heshima mbele Mkuu wangu: Biology ya nyoka kujivua magamba ni kuongeza uwezo wake wa sumu. vitu hivi vina negative relationship. Yaani uchanga wa ngozi ya nyoka hufanya sumu yake kuongezeka. Kwa hiyo basi Upya wa ngozi huleta SUMU ZAIDI.
 
Umbea wenu tu nani aliwaambia nyoka akivua gamba anakuwa njiwa?
Au mmejisahau.....nahisi bado mnausingizi, acha ni waamshe CCM, CCM! CCM Eeeh!. Ngozi mpya sumu ileile au mnasemaje WanaJF.

nimeipenda hii.

umejiunga leo, lakini waonekana uko na akili mingi sana!!

karibu JF.
 
Ni kweli JK ndiye gamba lakini wanaliogopa. Huyu jamaa amefaidika both direct and indirect na huo ufisadi ndani ya CCM na serikalini. Leo hii anakuja na single ya kuvua gamba chama.....crap. SISIEMU haiwezi kusafishika hadi JK na genge lake waondoke katika hicho chama, tofauti na hapo hakuna cha kuvua gamba. Hapo ni kukuna tu gamba, na wana-CCM wanaogopa hata kuzungumzia kumuondoa JK kwenye chama kwa sababu wanajua CCM as institute inafaidika na hilo gamba.
 
Uandamane na ummpongoe kwa lipi hasa? Kama angebadili serikalini hapo tungefikiria labda kukenua meno na sio kumpongeza! kubadli CCM na huku majizi kayashikilia na kuyahusudu huko serikalini wala hakuna maana yoyote kwa taifa labda kwenu nyie CCM kwa maana mnapanga njia za kuibia nchi kwa changa la macho eti kafanya maamuzi mazito. Kama ni maamuzi mazito yangekuwa kupunguza matumizi ya anasa ya fedha za wavuja jasho la nchi hii na kuelekeza hizo pesa kwenye maendeleo ya nchi. Akifanya hivyo pia bado sishawishiki kuundamana maana ni kazi yake kama mtawala. Nitaaandamana na kumpongeza pale akija na fikra binafsi za kutatua matatizo ya nchi hii na sio kuongeza umasikini nchi kwa kuwajaza majizi na wababe kama MUKAMA maana namjua natoka nae kijiji kimoja huko MUSOMA.
 
ndg yangu revenge in politics is worthless,kwani itendlea kuongeza mpasuko ndani ya ccm!yeye afanye kazi ya uenezi c ku-revenge !
 
Nape mshughulikie kwanza Riz1 maana ana influence UVCCM kuliko hata baba yake!
 
Umaneni tu na wa mwisho atakayebakia aje kulipoti kituoni.....nadhani hii kauli polisi wa kituo cha wazo hill inafaa kutumiwa hapa, na sio kama huyo askari aliyefungwa kwa minyororo ya mafisadi alivyowaambia wale ndugu zetu.
 
Kikubwa CCM wanatakiwa kukubali kwamba watanzania wamewachoka na kubadili mawazo ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili, siyo mabomu. Kwa hiyo gamba tunalotarajia siyo la uongozi (kumbadilisha Makamba na Mkama) ni utendaji kazi za chama. Hata hivyo Makamba amepromote kweli upinzani hasa alikopita kama kule Tarime. Big up Makamba.
 
Asilipize kisasi kwa faida ya nani?
Mimi naomba nape awe chachu ya kuangusha ccm,wali mdhililisha sana,walimtukana sana,....
Mda ndo huu,ameshika panga basi awamalize na aimalize ccm aje kwenye kundi la wapiganaji wa kweli
 
ni kweli jk ndio tatizo......ccm lazima wasema kwaheri jk na mob yake then chama kitakuwa safi
 
We muongo au unaongozwa na hisia zaidi kwa kuwa wote wanatoka arusha labda,lakini tunaomjua kinana yeye na Lowassa ni chui na paka hata Lowassa anajua kwamba Kinana hajawahi kumkubali na ni yeye Kinana Aliekuwa anamshauri JK (without success)Awatose kina EL na R.A.kwenye kampeni asiende majimboni mwao kuwainua mikono kwani watazidi kuiharibia ccm na kuwapa wakati mgumu kumnadi yeye Jk,pia amekuwa ni kinana ndani ya kamati kuu akiongoza upinzani dhini ya kampeni chafu za E.L. na genge lake dhidi ya SAM SITTA wakitaka kamati kuu imvue uanachama wa ccm mzee Six,na mara ya mwisho ni hivi majuzi kwenye uteuzi wa mgombea uspika atakaesimama kwa niaba ya ccm kila mtu aliona/kusoma jitihada za kinana,membe,chiligati kujaribu kumnusuru Sitta atetea kiti chake huku LOWASSA na genge lake wakimsimamia Spika wa sasa na kuhakikisha SITTA harudi tena,sasa KINANA anakuwaje mtu wa LOWASSA?
 
Iwe isiwe Nape lazima apitishe panga la ukweli kwa hao vilaza wa UVCCM ambalo kwa kuwa wanaupeo mdongo watakuwa wanakimbilia kufikiria kwamba analipiza kisasi lakini siyo. Hao ndo watu atakao wafanya nao kazi. Malalamiko yapo tu.
 
Naona walio kabidhiwa jembe la kuchimba kaburi la ccm wana iweza sana kazi yao
 
Back
Top Bottom