Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Ndugu Zangu,

TAARIFA zimetufikia, kuwa Mwenyekitiki wa CCM, Jakaya Kikwete amevunja CC na Sekretariati nzima ya CCM.

Tafsiri yangu; haya ni mabadiliko makubwa ndani ya CCM tangu kuundwa kwake mwaka 1977. Mabadiliko makubwa ya kichama yalifanyika mwaka huo wa 1977, wiki mbili tu baada ya CCM kuundwa.

Kuvunjwa kwa CC na Sekretariati kuna tafsiri kadhaa za haraka. Angalia hapa, ina maana; CCM imeondokana na Rostam na Chenge kwenye CC. Wawili hao hawarudi tena kwenye CC mpya itakayoundwa. Ndio, CCM wana namna zao za ' kufukuzana' wanapoacha ' kulindana'.

Na hiki ndio kile tulichoambiwa; Chama Kujivua Gamba, au labda magamba. Na kuna changamoto kwa Mwenyekiti wa Chama hicho- Unafanyaje na magamba yaliyovuliwa? Unayafukia, au unayaacha yakitapakaa? Na Magamba mengine hayaozi!

Ndio, Uchaguzi uliopita ulikuwa na ujumbe mmoja mkubwa kwa CCM kutoka kwa wapiga kura. Ni huu; MABADILIKO. Ndio, Watanzania wanataka mabadiliko. Kilichotokea Dodoma jana usiku ni jaribio la CCM kujibu matakwa ya wananchi. Je, wamefaulu? Tuna sababu ya kusubiri huku tukipima upepo unavyovuma.

Kuna maswali pia ambayo hatujapata majibu yake. Moja ni hili; Je, Mabadiliko haya ndani ya CCM yana ukubwa na athari gani kwa wakati huu na ujao?

Yepi zaidi yanakuja?
Tegemea - Kuwa asubuhi hii JK atakuwa 'busy' akishauriana na ' wazee' akina Msekwa, Mwinyi, Malecela, Mkapa na hata Spika Makinda. Wamsaidie mawazo katika kupendekeza majina kama 26 hivi yatakayopelekwa kwenye NEC ili yapigiwe kura na kupatikana wajumbe 18 wa CC.

Tegemea- Kuwa mengi ya majina hayo yakayopendekezwa yatatokana na wajumbe vijana wa NEC.

Nani atakuwa Katibu Mkuu?
Tegemea - Kuwa Katibu Mkuu atakuwa ama kijana au ana sura ya kijana. Jina kama Emmanuel Nchimbi si la kulibeza, William Lukuvi si ana sura ya kijana?

Kwa yanayotokea Dodoma CCM itakuwa imemaliza kazi ya ' kujibua' au kujivua gamba?

HAPANA. Kazi hiyo lazima iendelee. Kwa vile Sekretariati itaundwa upya, basi, kutakuwa na sura nyingi mpya. Tegemea, kuona vijana wengi zaidi wakipewa nafasi kwenye Sekretariati. Makatibu Wakuu wengi wa Mikoa na Wilaya watapanguliwa. Na vijana wenye fikra za ' kizamani' nao watapotea, na hapa, Tambwe Hizza laweza kuwa ni jina la ' vijiweni' kule Temeke Mikoroshini. Na kuna wengi ndani ya CCM wanaofanana na Tambwe Hizza.

Na upi ni mtihani mgumu kwa JK kwa sasa?
KATIBA MPYA, KATIBA MPYA, KATIBA MPYA….. ! Ndio, Watanzania wengi wa sasa na hususan vijana wanataka MABADILIKO, na Katiba kwao ni sehemu muhimu ya mabadiliko hayo. Watanzania wameshaamka na kubaini, kuwa KATIBA yao ya sasa nayo ni ' Maghumashi'. Neno hilo la mitaani lina maana ya mambo ya kiini macho na ubabaishaji.

Kwa vile JK ameshawajengea matumani ya kuwasaidia kupata Katiba Mpya itakayokidhi matakwa ya wakati uliopo na ujao, basi, nao wanataka iwe hivyo. Na kama JK atataka abaki akikumbukwa hata na vizazi vijavyo, basi, awe na ujasiri wa kuwasaidia Watanzania kupata KATIBA MPYA itakayolifanya taifa hili liwe la kisasa na lifanye mambo yake ikiwamo chaguzi katika mazingira ya kistaraabu. JK ana lazima ya kuacha kuiangalia kwanza CCM na bendera yake, badala yake aingalie kwanza Tanzania na bendera yake. Maslahi ya Nchi Kwanza. Maana, tunakokwenda, hata ndugu wa JK wanaweza wasiipigie kura CCM.

Na walioandaa Muswaada wa Sheria ya Kuanzisha Mchakato wa Katiba kimsingi wamechangia kumpunguzia JK heshima yake. Muswaada ule ni wa kiwango cha chini sana. Na JK akikubali kuasisi mchakato wa Katiba kwa kufuata ' ramani' ile tulioletewa juzi na kuambiwa tuitolee maoni, basi, nahofia, kuwa kuna watakaosema mitaani; " Na JK naye ni Maghumashi!"

Maggid
Iringa,
Jumapili, Aprili 10, 2011
0788 111 765
Mkuu, nayaheshimu mawazo yako hata kama sikubaliani nayo. Mswada wa sheria umeandaliwa kwa mapendekezo ya mkuu wa kaya na si viginevyo. Kwa msingi huo kinachofuati ni wabunge watukufu wa CCM kuupitisha kwa kishindo na kisha mkuu wa kaya kuharakisha kuuweka saini harakaharaka kuwa sheria. Si uliona viongozi wa CCM Dar walivyowakusanya watoto wa mitaani kwenda kufanya fujo kwenye kamati ya bunge wakaishia kusinzia kwa njaa huku polisi wakiwa hoi. Nani alikemea kitendo kile?
 
Mimi mbona bado siamini amini habari za kuvunjwa kwa CC. Kama itawezekana na kama kweli maamuzi hayo yamefanywa na wanaccm wenyewe (sio wale wanaotajwa kuwa mafisadi) basi ccm ime-rejuvinate.

Hofu yangu ni kwamba hawa mafisadi wanaweza kuamua kujitoa CC ili wananchi kurudisha tena imani kwa ccm ili hata utakapoanza mchakato wa kuteua mgombea wa urais imani itakuwa bado kubwa kwa ccm. Ila kama maamuzi yamefanywa kwa lengo la kuwaangusha mafisadi basi ccm inaelekea kuzimu maana vita ya wenyewe kwa wenyewe itakuwa dhahiri shahiri.

Tatizo lingine sina imani na JK kama kweli ana uwezo huo wa kimaamuzi.....ngoja tuone.
 
WAZO LA BURE KWA CCM.

Kwa vile wanamakatibu wa chama wa mikoa; na kwa vile makatibu wa chama wa kila mkoa wamekuwa ndiyo watendaji wakuu katika kutimiza malengo ya chama chao. JK hanabudi kumteua mmoja wapo kati ya hao ili awe katibu wa chama Taifa. Kulilko kuteua kati ya hao walikwisha tajwa na wanaJF.

Lakini yote kwa yote; sitaki kupoteza muda kuijadili sana CCM kwani ilipotufikisha watanzania hapafai.
 
Na walioandaa Muswaada wa Sheria ya Kuanzisha Mchakato wa Katiba kimsingi wamechangia kumpunguzia JK heshima yake. Muswaada ule ni wa kiwango cha chini sana. Na JK akikubali kuasisi mchakato wa Katiba kwa kufuata ’ ramani’ ile tulioletewa juzi na kuambiwa tuitolee maoni, basi, nahofia, kuwa kuna watakaosema mitaani; ” Na JK naye ni Maghumashi!”

hao hapo kwenye red ndio ninaowatamani sana yaani ni wehu, hivi walitaka kumu-impress nani, shame on them

hao mafisadi wachukuliwe hatua sio tu kujifanya wamewatema, tutajuaje kama watakuwa wanakula nao, kwani nani aliwaambia sisi tunawaonea wivu kuwa kwenye hiyo cc, kwa hiyo na sisi tushangilie sio, hicho chama ni chao hakituhusu hata wakitaka wasiwe na cc hilo ni shauri lao, tunachotaka sisi ni tanzania yenye haki, mazingaombwe tumechoka.

habari zao za magamba wakae nazo, tumeona magome itakuwa magamba!!!!
 
JK, anapaswa kuachana na wazee wenye mawazo ya kikoministi. Inabidi safu hiyo aweke vijana wenye umri wa miaka 30-39.


MkamaP,

Tatizo si umri, kwani umesahau majuzi vijana wa UVCCM wa mkoa wa pwani walivyotoa tamko lenye kupenyeza chuki za ukanda kwa kushambulia watu wa Kaskazini na hao wote umri wao ni kati ya 30 -39. Hivi Mzee wetu wa africa Nelson Mandela alichukua madaraka ya chama na uongozi wa nchi yake akiwa na miaka mingapi? Kumbuka ili siku zote, Umri wa mtu na Mawazo anayoyatoa yanauhusiano sana na malezi aliyokulia.
 
MkamaP,

Tatizo si umri, kwani umesahau majuzi vijana wa UVCCM wa mkoa wa pwani walivyotoa tamko lenye kupenyeza chuki za ukanda kwa kushambulia watu wa Kaskazini na hao wote umri wao ni kati ya 30 -39. Hivi Mzee wetu wa africa Nelson Mandela alichukua madaraka ya chama na uongozi wa nchi yake akiwa na miaka mingapi? Kumbuka ili siku zote, Umri wa mtu na Mawazo anayoyatoa yanauhusiano sana na malezi aliyokulia.

Kuhusu hao vijana, ni matamko tu ya wazee waliowaelekeza nini wazungumze hao vijana. Ni kweli mkuu, malezi ya watanzania kuanzia miaka 50 nchini TZ ni malezi ya kikoministi. Kuhusu Mandela, mandela hakuwahi kuwa mkomnisti. Hawa wazee wa Tanzania ni tatizo sana ni kama akina Putin na Mevedved walivyo makoministi watu wachache matajiri harafu masikini wengiiiiiiii, ndio maana wana rotate tu, sahizi kipindi hiki putin anataka kuwania urais.

Tatizo la msingi la kwanza, Tz ni wazee, wanamawazo ya kikomnisti. Wewe nenda kiwandani na ka digrii kako ukakute kazee ka VETA uone katakovyokufanyia fitina.
 
JK, anapaswa kuachana na wazee wenye mawazo ya kikoministi. Inabidi safu hiyo aweke vijana wenye umri wa miaka 30-39.

Haaa Haaa... CCM ya Kikwete walah.... kwa usanii nimewavulia kofia. Ona huyu msanii mwingine anasema wawekwe vijana wa miaka 30-39. Vijana wale wale wanaosema wazee ondokeni kwani mmeshakula hadi mkavimbiwa... tuachini nasi tuvimbiwe..
Anyway hapa mtawapata wengi lakini si mimi, kwani mlikolala ndio nilikoamkia. Hii CC kujiuzulu sijui mdudu gani ni usanii wenu. Ndio maana wooooote mawakala wa mafisadi hapa JF leo mmeibuka mlikokuwa mmelala. Kuja kokoleza usanii wenu uwaingie Wadanganyika eti CCM imejisafisha....
USANII UKO HIVI....
1. Kabla ya kikao vumisha uvumi kwamba mafisadi wanataka kumwondoa Kikwete kwenye uenyekiti... tena kuweka mkazo sema wanataka kufanya kama walivyofanya kwa Mbeki
2. Wakati kikao kinaanza mjumbe mmoja ibuka na hoja ya kutenganisha kofia ya uenyekiti na urais.
3. Kikwete jifanye umeshtuka saaana na utoe shinikizo ili CC wajiuzulu. (Ni bora hawa marafiki zako waukose huu ujumbe lakini tunajua tunachokifanya)
4. Kwenye hatua hii waandishi walioko kwenye 'listi yetu' (wa magazeti tv na hata kwenye mablog...) changamkeni na mpige debe kwa sana kuwa hatimaye maamuzi magumu yamefanyika...
5.
6.
7.
 
Siasa za fitina na majungu, ubaguzi na visasi ndo ulikuwa mwanzo wa kusambaratika ccm. Wataendelea hivyo mpaka watapotezana wote. Yangu macho.
 
Nadhani ni moja ya mabadiliko makubwa CCM watajivunia na labda badiliko hilo linaweza leta sura mpya ktk uongozi wa cc na NEC kwa ujumla,tuendelee kuwa na imani kwamba kila jambo huwa lina mwanzo na mwisho wake,hivyo basi watu kama kina Tambwe hiza,makamba na RA nadhani mwisho wao ndio umefika sasa
 
Mkuu wa ughaibuni,

Kuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama siyo kila kitu,kumbuka kamati ina wajumbe wengi ambao wanweza wakawa na mawaoz tofauti.

Pili ,Rais ndiye Amri Jsshi mkuu hivyo usidhani kuwa EL ana nguvu kiasi hicho.,kamati ipo kwa directive za serikali.Hell No...there is somehing you doesn;t know coz hii move ya CC haijaanza leo iliaznia pia kwenye idara huko mwezi machi..

Tatu,Kwa kuwa wametoka kwenye CC nasi jua hata nguvu yao kwenye chama inazidi kupungua na i see this good move ya Jk kuweka mambo sawa.

Majjid,I agree with you points..tutegemee wale watiifu wa Jk kuwemo kwenye NEC na wanajulikana wazi..
 
Haaa Haaa... CCM ya Kikwete walah.... kwa usanii nimewavulia kofia. Ona huyu msanii mwingine anasema wawekwe vijana wa miaka 30-39. Vijana wale wale wanaosema wazee ondokeni kwani mmeshakula hadi mkavimbiwa... tuachini nasi tuvimbiwe..
Anyway hapa mtawapata wengi lakini si mimi, kwani mlikolala ndio nilikoamkia. Hii CC kujiuzulu sijui mdudu gani ni usanii wenu. Ndio maana wooooote mawakala wa mafisadi hapa JF leo mmeibuka mlikokuwa mmelala. Kuja kokoleza usanii wenu uwaingie Wadanganyika eti CCM imejisafisha....
USANII UKO HIVI....
1. Kabla ya kikao vumisha uvumi kwamba mafisadi wanataka kumwondoa Kikwete kwenye uenyekiti... tena kuweka mkazo sema wanataka kufanya kama walivyofanya kwa Mbeki
2. Wakati kikao kinaanza mjumbe mmoja ibuka na hoja ya kutenganisha kofia ya uenyekiti na urais.
3. Kikwete jifanye umeshtuka saaana na utoe shinikizo ili CC wajiuzulu. (Ni bora hawa marafiki zako waukose huu ujumbe lakini tunajua tunachokifanya)
4. Kwenye hatua hii waandishi walioko kwenye 'listi yetu' (wa magazeti tv na hata kwenye mablog...) changamkeni na mpige debe kwa sana kuwa hatimaye maamuzi magumu yamefanyika...
5.
6.
7.

Pole sana.
 
Kuvunjwa sekretariate na CC ya CCM ni kwa manufaa ya Taifa au JK binafsi?

Katika mtiririko wa habari zilizokua zinaingia jana kutoka Dodoma, ilielezwa kwamba JK alicharuka baada ya kusikia mapendekezo kutoka upande wa "mafisadi" kwamba kukinusuru chama ni bora Rais atolewe cheo cha uenyekiti wa Chama Taifa ili aendelee kutumia muda wake mwengine kwenye mambo ya serikali na aachie mambo ya chama mtu mwengine (Lowassa). Hii inamaanisha kama hilipendekezo laku mnyang'anya JK uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi lisingepelekwa mbele ya kamati basi maamuzi yote "mazito" ya jana yasingetolewa.
 
Wana JF watu wa ajabu sana

Yaani kwenu this is the most important news of all?

You guys never cease to amaze me

watu wamekutana na chama chao kicha wanaamua who has to go and who has to stay kwenu hiyo big news?

Hivi kweli matatizo yote tuliyonayo kuanzia TRA, bandarini na uchafu ulikokithiri na matatizo ya elimu na afya yatatatulika baada ya kuondolewa watu wawili au baada ya kuvunjwa kamati kuu ya CCM?
 
JK, anapaswa kuachana na wazee wenye mawazo ya kikoministi. Inabidi safu hiyo aweke vijana wenye umri wa miaka 30-39.

ishu sio uzee bali ni uazelndo VS ubinafsi. kwani wakina masha , mwinyi, ngeleja etc ni wazee? na wakina mwakyembe , sitta , warioba etc ni vijana?
 
Ccm wamefika pazuri sana. Hawawezi onekana wana maana mbele za watz hadi RA na kina Chenge waondoke na JK abadili msimamo wake wa kuwashabikia kina Mramba kwa kuwakampenia. Ajifunze kwa kina McCain ambao walijidistance kabisa na Bush wakijua huyo jamaa alikuwa unpopular na wala hawakumkaribisha kwenye kamoeni zao. Kikwete hasomi kabisa?

Amesaidia sana kukichafua chama na kuwafanya watz waonekane wajinga ambao hawana lolote wanaloweza kufanya hata kama anaharibu namna gani. Jk anaamini kuwa yuko sahihi sana na ndio maana hata wakimweleza kupunguza safari za nje (na gharama kubwa) he doesn't care na sasa ndo anagundua Ccm haikubaliki.

Kwanza nani ataamini CCM na serikali yake kuwa makini kama wanaweza kutengeneza vituo 3 tu nchi nzima kutolea mawazo ya muswada wa katiba mpya. Hawako serious kabisa au nchi hiii inaongozwa na wapuuzi kweli kweli!
 
Watanzania watu wa ajabu sana

Yaani kwenu this is the most important news of all?

You guys never cease to amaze me

watu wamekutana na chama chao kicha wanaamua who has to go and who has to stay kwenu hiyo big news?

Hivi kweli matatizo yote tuliyonayo kuanzia TRA, bandarini na uchafu ulikokithiri na matatizo ya elimu na afya yatatatulika baada ya kuondolewa watu wawili au baada ya kuvunjwa kamati kuu ya CCM?


Most probably is not big news to you because you have no idea how this CCM NEC have costed our nations. The instability of our economy and you so called TRA, PTA etc. are caused by corrupt CCM NEC. And you know why? they hid in there in order to take advantage of the system and play their malicious games.
 
ishu sio uzee bali ni uazelndo VS ubinafsi. kwani wakina masha , mwinyi, ngeleja etc ni wazee? na wakina mwakyembe , sitta , warioba etc ni vijana?

Tatizo nafikiri hatufati kanuni za uadishi wa paper, ni lazima uli reference mahala fulani ili ku -justfy unachoongelea. Nani alikuambieni Sita, mwakyembe wanapigania masilahi yako. Fuatilia kwa makini mwanzoni mwa sakata la Richmord sita akiwa spika wakati huo wakiwa kundi moja na akina RA. Hoja alijaribu sana kuizima na kusema ulongo ulongo. Sita ameanza kupigana baada ya ku defect kutokana na kuzidiwa ujanja.

Tatizo wewe unaongea kama watoto wa Gadafi kumhasi baba yao na eti nao wamuite dictator baba yao, hasa unapowataja akina Mwinyi. Na vijana wachache waliopo wala sio wakutolea mfano kwa sababu wazee wamewa-abducted.

Tanzania hakuna mzee anayepigania haki ya Tanzania ila ni majambazi wawili wanapigania walichokipora, sasa mmoja anaonekana kulemewa. Na wengine wako pembeni wakitamani kuingia mahali hapo nao waibe.
 
No No no guys .... nothing serious here!!

The problem of this country is feeble and very weak-charactered JK

..if at all all was retained and only JK ..tossed out ...I would call it a day!!

I tell you on this day and come to remember it .... With smiling JK there ...nothing is constructive with this nation even with their party!!!!
 
Back
Top Bottom