Mimi naona ni kwasababu ya kutokua na hofu ya Mungu pia. Mtu mwenye hofu ya Mungu na aliyelelewa vizuri anakua na
Uvumilivu
Huruma
Kusamehe
Upendo
Ukishakua na hivi vitu automatically utaweza kudumu katika ndoa hata kama PESA imeyumba katika familia.
Hofu ya Mungu itakufanya umvumilie mwenzio kukiwa na matatizo ya kiafya au mwenzio akishindwa kuperform no 2.
Hofu ya Mungu itakupa hekima ya kudeal na in-laws.
Ndio maana biblia imesema mlee mtoto katika njia ipasayo nae hataiacha hata atakapokua mzee (nimesahau ipo wapi ila ni kitabu cha Mithali).
Mkikutana wote wenye hofu ya Mungu kwelikweli changamoto za hizo 1,2 na 3 itakua rahisi kuvumilia.