Mambo machache bora ya kuirudisha CCM katika misingi yake

Mambo machache bora ya kuirudisha CCM katika misingi yake

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,433
Reaction score
4,996
Hakuna haja ya kuunda tume wala kamati
Hizi ni action zinazotakiwa kuchukuliwa
1. Zuia machawa katika chama

2. Rudisha mamlaka kwa wanachama wa chini ( wananchi), mambo ya watu wachache kukata majina na kuamua nani akagombee yasiwepo tena.

3. Zuia rushwa katika chama, hiyo ndio inaleta makundi na kusababisha tuwapoteze viongozi wazuri.

4. Uanzishwe mkakati wa kuwainua kiuchumi wanachama wa chini ( mambo ya chumvi na kanga wakati wa kampeni baada ya hapo wanatupwa sio kabisa ), ukiangalia kwenye mikutano robo tatu ya wahudhuriaji ni choka mbaya na wasio na nuru, hao ndio ninaowaongelea.

5. Uendelezwe utaratibu wa kuwakumbuka na kuwaenzi wazee na watangulizi waliokisaidia chama ikiwemo kuwapatia chochote kitu ili kuthamini mchango wao ( Lenga wale ambao maisha yao sio mazuri)

6. Urudishwe ule ushindani wa hoja na siasa za majukwaani, tumezimisi sana zile siasa za enzi za mzee JAKAYA.

7. Tukataze watendaji wa chama kuwaingilia watumishi wa umma, badala yake watendaji wa serikali ndio wahusike na watumishi wa umma kwa asilimia zote %

8. Mengine nitashauri kwenye vikao ( kubwa zaidi machawa wapigwe stop)
 
Back
Top Bottom