Uchaguzi 2020 Mambo Kumi niliyoyasikia leo kwa mara ya kwanza kuhusu Tanzania kutoka kwa Tundu Lissu akiwa Mbarali

MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro - MKAPA), Hale (Tanga - NYERERE), Pangani (Tanga - MWINYI), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro - NYERERE), Rusumo (Kagera- KIKWETE), Songwe (Mbeya - KIKWETE)

TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi. Anaijua migogoro yote ya mipaka ya hifadhi nchi hii, na ardhi za wananchi zilizopokwa bila fidia, kwa sababu alilifanyia utafiti katika kazi yake ya kwanza akitoka chuo.

NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU SIFURI SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki ekari 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali, ikiwemo NAFCO, kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu. Viongozi wengine na matajiri wenye ekari chini ya hapo, elfu 35, elfu 20, elfu 15, elfu 10, elfu 5 ni wengi, wengi, wengi mno. Ambao walipeana kama "wawekezaji" lakini wamezikalia tu. Na ni sababu moja kubwa na migogoro ya wakulima na wafugaji, kupungua kwa ardhi.

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo. Hoja kuu ya kitabu cha Nyerere inasema jamii inapimwa kwa maendeleo ya watu, sio ya vitu na miundombinu.

TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendelea kujenga vingine vyote nchini, Magufuli si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.

Kitabu Freedom and Unit ni mkusanyiko wa makala na hotuba mbalimbali za Julius Nyerere tangu miaka ya 1950s mpaka miaka ya 1960s mwanzoni.

Si kitabu kilichoandikwa kwa minajili ya hoja ya mtoa hoja.
 
mada apa ni kuhusu izo mbuga na airport so my point ni kwama

heck no

mada sio mbuga na airport

mada ni ujenzi wa miundombinu usioleta maendeleo ya watu, unaotumiwa kukanyaga watu, na usiofuata sheria na taratibu za zabuni na uwazi kwenye miamala ya fedha za umma pamoja na mamlaka ya mapato inavyotumika kupora mali za raia na kuua.
 
Halafu wale wenzetu wa UVCCM watasema haya ni matusi makubwa wametukanwa kufuatana na lugha yao ya mtaa wa Lumumba.
 
MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro - MKAPA), Hale (Tanga - NYERERE), Pangani (Tanga - MWINYI), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro - NYERERE), Rusumo (Kagera- KIKWETE), Songwe (Mbeya - KIKWETE)

TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi. Anaijua migogoro yote ya mipaka ya hifadhi nchi hii, na ardhi za wananchi zilizopokwa bila fidia, kwa sababu alilifanyia utafiti katika kazi yake ya kwanza akitoka chuo.

NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU SIFURI SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki ekari 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali, ikiwemo NAFCO, kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu. Viongozi wengine na matajiri wenye ekari chini ya hapo, elfu 35, elfu 20, elfu 15, elfu 10, elfu 5 ni wengi, wengi, wengi mno. Ambao walipeana kama "wawekezaji" lakini wamezikalia tu. Na ni sababu moja kubwa na migogoro ya wakulima na wafugaji, kupungua kwa ardhi.

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo. Hoja kuu ya kitabu cha Nyerere inasema jamii inapimwa kwa maendeleo ya watu, sio ya vitu na miundombinu.

TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendelea kujenga vingine vyote nchini, Magufuli si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

-----------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.

Msijisahaulishe jamani Magufuli alikuwa Kagera na maelfu walifurika katika viwanja vya Gymkhana
kg1 (12).JPG
kg1 (12).JPG
 
heck no

mada sio mbuga na airport

mada ni ujenzi wa miundombinu usioleta maendeleo ya watu, unaotumiwa kukanyaga watu, na usiofuata sheria na taratibu za zabuni na uwazi kwenye miamala ya fedha za umma pamoja na mamlaka ya mapato inavyotumika kupora mali za raia na kuua.

wewe tangia lini ushawahi ona maendeleo ya watu ambayo hayajaanzia na maendeleo ya vitu? ukitaka ajira nyingi, jenga miradi mipya watu waajiriwe, ukitaka mishahara iwe na hadhi then thibiti wafanya biashara! as simple as that. unataka rocket economics uelewe ama?
 
its wide open ACT na NCCR mageuzi ndo vyama vilivo rudi hewani kwa haraka sana, na kuvuna wanachama wengi sana! meanwhile chadema has been loosing tokea mwaka umeanza, na ndo hali ilivo hata mitaani,

-mind you anguko mtakua mmelisababisha wenyewe kwa kukosa sera nzuri za kuwashawishi wananchi, mgombea wenu anaona polisi wabaya, mahakama wabaya, tbc wabaya ! nssf wabaya, badala ya kujenga hoja kwenye tatizo anafoka, sasa anategemea serikali atakayoiunda atakua anazungukwa na nan iwapo mpaka polisi wenyewe unawatukana na wao ndo wenye mamlaka ya kukupindua
-- and the worst of all mpaka edwin mtei mwanzilishi wa chadema unamuona punguwani, something must be done
stakehigh bahati mbaya mpumbavu hajitambui ila wengine ndiyo wanakiona kuwa yeye ni mpumbavu. Yeye nadhani ni mjanja. Pole sana kwa kuandika utumbo
 
Enyi mamlaka za rohoni na mwilini tunaomba mumlinde kwa nguvu zote kijana wenu Lisu na mamlaka ya kuliongoza taifa hili mumpe yeye maana amestahili.
 
stakehigh bahati mbaya mpumbavu hajitambui ila wengine ndiyo wanakiona kuwa yeye ni mpumbavu. Yeye nadhani ni mjanja. Pole sana kwa kuandika utumbo

ivi hamnaga namna ingine ya kufikisha idea zenu bila kuita mtu mjinga ama mpumbavu?
alafu what i said ni fact, and i can assure you kuna watu wameshajiandaa kua chama kikuu cha upinzani, meanwhile mkiwa mnajipendekeza kwa maalim seif alafu wao wakina hawana shobo na nyie!

hakuna marefu yasio na ncha walisema wahenga
 
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Hapo kawapotezea muda tu watu wa mbalali
kumbe hela za kuajiri vijana wetu waliomaliza vyuo mjomba na mpwa wanazifuja
 
Hamjui mlicho nacho mpaka mkipoteze.
Pamoja na hiyo kelele hatoboi 2020 ni JPM tena.
 
Mikutano ya kampeni Sio sehemu ya maswali Ni sehemu ya kunadi sera na kuomba kura sehemu ya maswali na majibu Ni bungeni alikokuwa huko angeuliza maswali yote apewe majibu na serikali hakuuliza anakuja kuuliza Nani kwenye mikutano ya kampeni

Mkutano wa kampeni Hakuna Spika Wala waziri anapotezea muda watu tu

Anadi sera zake aombe kura . Aondoke aende Kwingine
Sera za nini?hii inaitwa operation fukua makaburi..mpaka Magu aseme poo..na jana Tunduma Lissu amesema mtu atakayechezea uchaguzi The Hague inamuhusu..sasa itakuwa wanalaumiana kwa nini mlishindwa kumuuwa...
 
We k kweli ndo umejibu nn hapo sasa.. mleta mada kasema lisu alisema tazara nayo ni sgr... Tazara ni 1067mm thats mean sio sgr... Mimi nimeuliza.
Acha mnduku mnduku msukule ni waliokuzaa
Acha Kupanic msukule wa lumumba ww... Hapo si umeeleweshwa maana ya sgr sa unataka nn zaidi..... 1067mm ndio nini we mnduku.... Ndio shida ya shule za kata ng'ombe ww
Hizo 1067 ni urefu Dar to Tunduma...... Ile ina 2,000km long mlamba makalio ww ili tu upate cheo
 
  • Thanks
Reactions: PNC
"Kufanya nyanda za juu kusini kuwa kituo cha kilimo cha biashara kusini mwa nchi za Africa"uwezo wa Lissu umeishia hapa.
hawezi,hawezi,hawezi kudadavua ataweka mfumo upi au mazingira yepi,pesa zitatoka mfuko upi,atawawezesha vipi wakulima,pembejeo,soko ili kufanikisha hili.
hawezi,hana icho kipaji.wakina Lipumba ni wabobezi wabobezi wa kuchanganua lakini kusema na kutenda nintofauti.

Kuna tofauti kati ya fasihi Andishi na Simulizi. Sera za vyama zimeandikwa na kuchambuliwa kwenye vitabu. Ukiachilia mbali kwamba sio wote wanaweza kupata vitabu hivyo lakini pia sio wote wanaoweza kusoma wakaelewa.

Tundu LISU anatumia muda wake mwingi wa kampeni kunadi sera zake kwa njia ya UHALISIA " Realities " .Jambo hili linawakera sana CCM kwa sababu anachofanya ni kama mwalimu anavyofundisha darasani.

Anaanza kueleza tatizo kwa kulitaja ..Kwa mfano ugomvi wa wakulima na wafugaji. Baada ya hapo anaeleza chanzo cha tatizo hilo..Mfano" Ardhi kubwa kumilikiwa na viongozi wakubwa au kampuni kadhaa na hapa anawataja kwa majina.

Baada ya hapo anaeleza jinsi walivyopata ardhi hiyo,kama ni kwa minajili ya vyeo vyao au kuuziwa isivyo halali au halali. Pia hueleza faida au hasara ya watu hao kujimilikisha ardhi hiyo.

Mwisho anarudi kwenye suluhisho kwa mujibu wa SERA za Chadema au kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuonyesha UDHAIFU na kutowajibika kwa viongozi waliopo.

Huu ni uwasilishaji BORA kabisa wa SERA mpya na ambazo wananchi hawajazizoea au kuzielewa vizuri.

CCM na Tume (CCM) hawakutegemea kuona uwasilishaji huu. Walitamani awe anasoma kama ilivyoandikwa kwenye kitabu. Lakini pia walipenda waone uwasilishaji huo uwe kama alivyofanya Lowasa(2015) ,Dr Slaa(2010) au Freeman Mbowe (2005) ambao walikua wanazisema juu juu bila mifano hai inayowagusa wananchi wa eneo husika.

Hongera Tundu Lissu! shikilia hapohapo watu wanakuelewa sana na pia unawavuruga watu wa Lumumba. Hawana uwezo wa kujibu hoja zako,wanaishia kuandika "Magufuli 5 Tena
 
Back
Top Bottom