Uchaguzi 2020 Mambo Kumi niliyoyasikia leo kwa mara ya kwanza kuhusu Tanzania kutoka kwa Tundu Lissu akiwa Mbarali

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,117
2,000
MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro - MKAPA), Hale (Tanga - NYERERE), Pangani (Tanga - MWINYI), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro - NYERERE), Rusumo (Kagera- KIKWETE), Songwe (Mbeya - KIKWETE)

TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi. Anaijua migogoro yote ya mipaka ya hifadhi nchi hii, na ardhi za wananchi zilizopokwa bila fidia, kwa sababu alilifanyia utafiti katika kazi yake ya kwanza akitoka chuo.

NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU SIFURI SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki ekari 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali, ikiwemo NAFCO, kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu. Viongozi wengine na matajiri wenye ekari chini ya hapo, elfu 35, elfu 20, elfu 15, elfu 10, elfu 5 ni wengi, wengi, wengi mno. Ambao walipeana kama "wawekezaji" lakini wamezikalia tu. Na ni sababu moja kubwa na migogoro ya wakulima na wafugaji, kupungua kwa ardhi.

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo. Hoja kuu ya kitabu cha Nyerere inasema jamii inapimwa kwa maendeleo ya watu, sio ya vitu na miundombinu.

TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendelea kujenga vingine vyote nchini, Magufuli si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

-----------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
9,268
2,000
Hawafanyi wao, ni kwa niaba ya watanzania wote na kodi zetu na mali asili zetu na utekelezaji wa matakwa ya watanzania, kikubwa hapa ni usimamizi na uzalendo tu. Nchi hii ilikua inaelekea kubaya mkuu tuweke unafiki pembeni, Mzee Magu kajitahidi sana.
Yeye si malaika .....
Kwa kuficha mikataba ya manunuzi makubwa? Hivi mmelishwa nini wenzetu?
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
16,680
2,000
"Kufanya nyanda za juu kusini kuwa kituo cha kilimo cha biashara kusini mwa nchi za Africa"uwezo wa Lissu umeishia hapa.
hawezi,hawezi,hawezi kudadavua ataweka mfumo upi au mazingira yepi,pesa zitatoka mfuko upi,atawawezesha vipi wakulima,pembejeo,soko ili kufanikisha hili.
hawezi,hana icho kipaji.wakina Lipumba ni wabobezi wabobezi wa kuchanganua lakini kusema na kutenda nintofauti.
Acha kubwabwaja we ng'ombe ambae upo uchumi kati wa buku7......
Lissu atawanyoosha haki ya nani........ Huoni mgombea wako anakopi sera na ahadi za Tundu Lissu?
 
Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
3,092
2,000
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Hapo kawapotezea muda tu watu wa mbalali
Acha kuropoka kama punguani bwana alikuambia mambo 10 aliyosikoa siyo sera! Mbona yule PUNGUANI WENU anajibu ? Mbona yye anaongelea bima ya afya ipo kwenye ilani ya Ccm?
Usituletee ujuha wako hapa
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
320
250
Yanawahusu Nini watu wa Mbalali alipokuwa akihutubia? Kaanza kugeuza mikutano ya kampeni vijiwe vya story
Anayeweza kugeuza uwanja wa watu elfu kumi kuwa kijiwe na kuweza kupata kusikilizwa yeye,sii mchezo.Sasa tuambie wote hao umeona hawana akili.Au ujumbe hapa Nini.
 
Larson

Member
Dec 9, 2015
88
125
MOJA: Reli nyingine zilizopo na zenyewe ni standard gauge - TAZARA, RELI YA KATI, (DAR -KIGOMA) na ya TANGA-ARUSHA

MBILI: Marais wengine wote na wenyewe walianzisha mabwawa ya umeme, kuanzia Kidatu na Mtera (Nyerere), wengine wakajenga Kihansi (Morogoro - MKAPA), Hale (Tanga - NYERERE), Pangani (Tanga - MWINYI), Nyumba ya Mungu (Kilimanjaro - NYERERE), Rusumo (Kagera- KIKWETE), Songwe (Mbeya - KIKWETE)

TATU: Wakati wa uhuru kulikuwa na mbuga moja tu, ya Serengeti, iliyotengwa na Mkoloni. Nyingine zote zilianzishwa kwa amri za marais kwa kuhamisha watu, hizi za Magufuli wanahamisha wanyama, wanawapeleka Chato ambako naturally hakuna mbuga, hakuna wanyama. Na wanapounda mbuga mpya wanaingilia maeneo ya watu na hawawalipi fidia, wanasababisha maafa na migogoro ya ardhi. Anaijua migogoro yote ya mipaka ya hifadhi nchi hii, na ardhi za wananchi zilizopokwa bila fidia, kwa sababu alilifanyia utafiti katika kazi yake ya kwanza akitoka chuo.

NNE: Daktari muanzilishi wa Hospitali ya Masana Mbezi, Dar es Salaam, alikufa kwa pressure baada ya kukutwa na mashine alizonunua kwenye mnada wa vifaa chakavu, Muhimbili, akasahau kufuta zile alama za MUHIMBILI MKWAJU SERIKALI MKWAJU HOSP MKWAJU RUFAA MKWAJU SIFURI SIFURI MBILI MKWAJU.... Alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi isiyo na dhamana, akafa na pressure halafu wakakuta ni kweli alinunua Muhimbili.

TANO: Mbunge wa CCM, Salim Hassan Abdullah Turki, amekufa na pressure baada ya kubambikwa madai ya kodi ya mabilioni. Mheshimiwa Turki ndie aliyekodi ndege ya kumpeleka Tundu Lissu Nairobi akiwa mahututi. Hii Tundu Lissu amesema ameambiwa na familia ya marehemu.

SITA: Mtoto wa Dada yake Magufuli, Doto James, ambae kwa sasa ndie ana saini miamala yote ya serikali, alirushwa vyeo ghafla kutoka kuwa afisa TANROADS mpaka katibu mkuu HAZINA pindi mjomba wake alipopata Urais; Na kwamba, sasa hivi kuna watu wawili tu nchi hii, Doto James na mjomba wake, ambao wanajua hela za kununua ndege na za Bwawa la Rufiji ni shiing ngapi na zimetoka wapi.

SABA: Familia ya Mwinyi, Mkapa kila mmoja anamiliki ekari 60,000, Sumaye 45,000 za ardhi ambazo awali zilikuwa mashamba ya serikali, ikiwemo NAFCO, kabla ya kujimilikisha wakiwa marais na wa mawaziri wakuu. Viongozi wengine na matajiri wenye ekari chini ya hapo, elfu 35, elfu 20, elfu 15, elfu 10, elfu 5 ni wengi, wengi, wengi mno. Ambao walipeana kama "wawekezaji" lakini wamezikalia tu. Na ni sababu moja kubwa na migogoro ya wakulima na wafugaji, kupungua kwa ardhi.

NANE: Miaka saba baada ya kuwa tushapata uhuru, Nyerere aliandika kitabu kuelekezea kwamba bado tunahitaji uhuru licha ya kuwa tulishawaondoa wakoloni, kinaitwa Uhuru na Maendeleo

TISA: Mkandarasi wa Uwanja wa Ndege Chato, Mayanga Construction (Steven Makigo), ni mme mwenza wa Magufuli, wameoa nyumba moja. Mme mwenza aliambiwa jenga uwanja! Mpwa (Doto James) akaambiwa toa hela!

KUMI: Kiwanja kimoja tu cha ndege kimejengwa na Mkoloni, Mwingereza, kile cha Air Wing, Ukonga. Nyerere alijenga Kilimanjaro na wakaendelea kujenga vingine vyote nchini, Magufuli si Mtanzania wa kwanza kujenga uwanja wa ndege.

--------------------------------------------------------------------------------------------------------------

WHAT'S THE POINT?
Anasema, wakati wote huu inajengwa hiyo miradi toka uhuru, airports, mbuga, reli, mabwawa ya umeme, mabarabara, hakuna Mtanzania aliyenyanyapaliwa, aliyeuawa kwa pressure ya kutishwa, kuhamishwa, kubambikwa kodi, kupigwa, kutiwa kizuizini miaka 5, au kumiminiwa risasi kwa kuhoji miradi au kwa kigezo kwamba nawaletea maendeleo.
Watanzania wampe kura kwa Sera gani hapo itakayowasaidia?. Yeye atafanya nini?. Chadema saccos sio ya kuwaamini kabisa.
 
stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
2,001
2,000
KUMI NA MOJA: chadema ilipokea ruzuku ya mil 300, michango ya wabunge lakini yote iliishia kwa mwenyekiti baada ya mmachame kujimilikisha chama
 
stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
2,001
2,000
Huu ni ukweli mchungu..Katika hoja hizi Mgombea wa Chama tawala lazma ajibu point moja baada ya nyingine na hii ndyo mana ya siasa. Haya sio matusi kisiasa unahitaji kujibu kublok hoja ya m pinzani wako..Vijana wa Chama fulani jitokezeni kujibu hoja hizi!!vingnevo mtajikuta mnaanza kudai eti ni matusi hili neno" matusi limegeuka mbinu ya kukwepa kumjibu "Machine Lissu "!!!

hakuna cha maana sasa apo cha kumjibu sasa, kama ni kuanzisha mbuga za wanyama, mapato ya watalii mpaka saahv yanaeleweka ni billions of money, the 2nd after south africa kwa mapato ya utalii and 3rd africa
- viwanja vya ndege obvious they are all success stories

so speech nzima ni pumba
 
Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
615
1,000
Huu ni ukweli mchungu..Katika hoja hizi Mgombea wa Chama tawala lazma ajibu point moja baada ya nyingine na hii ndyo mana ya siasa. Haya sio matusi kisiasa unahitaji kujibu kublok hoja ya m pinzani wako..Vijana wa Chama fulani jitokezeni kujibu hoja hizi!!vingnevo mtajikuta mnaanza kudai eti ni matusi hili neno" matusi limegeuka mbinu ya kukwepa kumjibu "Machine Lissu "!!!
Anachosema Lissu ni kweli kabisa na anayetakiwa kujibu ni Magufuli mwenyewe siyo hao vilaza wa CCM wanaojibu kwa niaba yake humu kwenye jf. Hawa vilaza wanaojibu tuhuma ambazo hawazijui mpaka wanamfanya mtuhumiwa kuonekana mbele ya Umma naye ni kilaza kwa kushindwa kujibu tuhuma zinazomkabili. Hii inaendelea kuonyesha kuwa Rais alioko madarakani hana uwezo wa kukabiliana uso kwa uso kwa hoja na wapinzani wake wote na Chama chake wanajua hivyo ndo maana hawataki kusikia mambo ya midahalo na mahojiano mubashara. Stiegler's Gorge ilikuwa Maradi wa Nyerere wala hakushindwa kutekeleza kama CCM wanavyodai bali aliheshimu mikataba ya Kimataifa ambayo nchi yetu iliridhia badala yake alijenga Mtera. SGR ni Mradi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yenye nia ya kuunganisha nchi wanachama na bahari ili nchi nne wanachama zisizo na bahari ziweze kutumia bandari mbili zilizopo. TAZARA ilijengwa na Nyerere na kuunganisha ya Kati na ya Tanga ambayo iliwezesha treni itoke Arusha mpaka Kigoma lakini, kama ATC ilivyokufa, ikafa Magufuli akiwa Waziri wa Serikali ya CCM. Kama Rais hawezi kujibu tuhuma mwenyewe, kuna Msemaji wa Serikali au Ikulu kuna Msemaji wa Rais na Chamani kuna Katibu Mkuu, hao wote wangeweza kutumika kujibu, kuhoji, kufafanua tuhuma zote kwa niaba yake badala ya hao vilaza watafuta uteuzi. Mtindo wa kuteua wafanyakazi Serikalini kwa kutegemea uungaji mkono juhudi ungeachwa ili watu wateuliwe kwa ujuzi, uwezo na uzoefu wao wanaopatijana kwa Search Team.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,597
2,000
Mikutano ya kampeni Sio sehemu ya maswali Ni sehemu ya kunadi sera na kuomba kura sehemu ya maswali na majibu Ni bungeni alikokuwa huko angeuliza maswali yote apewe majibu na serikali hakuuliza anakuja kuuliza Nani kwenye mikutano ya kampeni

Mkutano wa kampeni Hakuna Spika Wala waziri anapotezea muda watu tu

Anadi sera zake aombe kura . Aondoke aende Kwingine
Kwenye bunge kibogoyo atauliza maswali hayo apate majibu? Hapo yuko kwenye bunge la ukweli ambalo ni wananchi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom