Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 41,983
- 12,702
Tabia ya kupiga mswaki ovyo bila utaratibu inakera sana hasa nyakati za asubuhi. Unakuta mtu kasimama barazani anasafisha meno na kutematema ovyo, na wengine wanaongea huku mswaki upo mdomoni. Akina dada wengine nao sijui vipi unakuta yupo na kanga moja mswaki mdomoni anaenda dukani au kwa jirani. Jamani tuwe wastaarabu, nimewahi fundishwa tendo la kupiga mswaki linahitaji ustaarabu na heshima kama lilivyo tendo la ndoa.......