Mamba mkubwa auawa hotelini jijini Mwanza

Mijamaa ya TANAPA kweli mzingo yaani walishindwa kutumia njia zote kumrudishia kwenye makazi yake hadi wamuue??
 
Maliasili gani hao wamegeuka wauaji?
Mamba ambaye ameshaoneka na hakuwa ameshambulia mtu bado anapigwa risasi. Watanzania wengi wanapenda sana miteremko kazini so sad!
 
Hivi wanaosema wangemrudisha bila kumdhuru, akirudi tena siku nyingine na kudhuru watu? Mtalalamika kwanini maliasili walimwachia.

Mamba ni miongoni mwa viumbe wenye akili sana, whatever the reason, jua hajaja hapo kwa bahati mbaya.
Tulio ishi mbugani tunajua hilo. Maliasili wanajua hilo.

Kuna wanyama wa kuwaachia na kuna wengine risk ni kubwa mno wa kurudi tena na kudhuru watu.

Ukiwa mbugani wanyama wanahaki na inachukuliwa kuwa wewe ndo umemwingilia eneo lake kumuua mnyama ni last resort, akija kwenye makazi ya watu ni kinyume chake.
 
Hajamaanisha dawa kama ulivodhani, hiyo ni sumu mbaya sana, ujazo wa kifuniko cha chupa ya maji tu inatosha kuua zaidi ya watu 300, ndo maana wakati wa zoezi la kuteketeza mzoga wa mamba huwa kuna ulinzi mkali sana mkuu
Uko sahihi mkuu.
 
Mbona USA wanaingia mpaka swimming pool lakini wanawakamata na kuwapeleka sehemu za mbali?
Kwanini wamuuwe?
Hebu maliasili watoe mafunzo kwa wananchi kwamba pindi wanapoona mnyama wapigiwe na kuja kumkamata
Kumshika Mamba ni rahisi sana
Inasikitisha kwa kweli
Unaongea simple kwasababu hujaona timbwili la hawa wadudu, hapo angeachwa akudhuru raia mngekuja kulialia hapa
 
What a shame man!! Mijitusi mikubwa hivyo ya nini?? Kwani alikutukania mzazi hata wewe umtukane kihivyo?? Jamani, punguzeni stress, ka sivyo kuna siku mtu atafia juu ya key board kwa hasira
Nimecheka sana hapo uliposema, " ...atafia juu ya keyboard kwa hasiraa"

 
Ila vijana wa nchi hii sijui njaa zimekandamiza ubongo maana kutwa kulalamika, mamba kaja ktk makazi kauawa wanalalamika, angeachwa akadhuru raia wangelalamika humu na matu...daah kweli kizazi cha kulalamika kama watoto wa kambo
 
Kuna wataopinga hati kumuua mamba ni kosa.!!

Hii iko hivi wewe binadamu ukienda hifadhi kisha umuue mnyama wewe ndio unahatia yaani hata wale askari wa forest wakikuona huna uhai(unapigwa na kizito)

Mnyama nae akija huku makazi ya watu nayeye kama sio kurudishwa alikotoka kistaharabu atapigwa na kizito vivo hivo.

Afu huyo mamba pengine IN MYSTERIOUS WAY angeua binadamu kuna watu wangehoji "askari wa forest kazi yao ni nini mpaka wanyama wanatoroka na kuja kudhulu watu wao hawana habari?"
Mkuu vijana wa kizazi cha lawama washaanza kulaum tayari
 
Nyongo ya mamba ukitia kwenye tank au chanzo kikuu cha maji mf Ruvu juu...wakazi wote wa dsm wanaharisha kuanzia raisi mpak mpiga debe na wngine kibao kupoteza maisha ...nyongo yake ni sumu kali sana hakunaga....nyongo ya kenge ukitia kwenye kisima cha mtaa bas mtaa mzima wanahara
 
Back
Top Bottom