Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Alikua anathamini watoto wake kuwarithisha elimu kuliko mambo mengine. Ndugu wengine walikua hawajikita sana huko ndio kisa chakutengwa
Ooh basi sawa, kama upo Dar nita kulink kwa mtu flani kikubwa uwe na ushahidi wote wa chuo mpaka death certificate ya mzee, ikiwa bahati yako utasaidika, ni kumuomba Mungu tu.
 
Ooh basi sawa, kama upo Dar nita kulink kwa mtu flani kikubwa uwe na ushahidi wote wa chuo mpaka death certificate ya mzee, ikiwa bahati yako utasaidika, ni kumuomba Mungu tu.
Ndio nipo Dar
Nitashukuru
 
Mimi na mama wa kambo hatuna bifu kwakuwa sijawahi onesha dalili za kutaka mali yoyote. Mzee bado yupo sana na kwake hata sipajui, mali zake sizijui sasa nitadai nini.
Nishaacha kumuomba mzee lolote na hata hatuwasiliani tena, ada mwenyewe sijamalizia lakini naamini itaisha bila tatizo.
Mzee nimesave namba yake ili akinitafuta nisiulize 'we nani?'
Muhimu kwangu, nina strong bond na ukoo. Sasa ole wake mzee mimi niwe Naseeb, yeye ndo atakuwa mzee Abdul.
 
Nashukuru sana mkuu ila ukiangalia hapo juu niliandika baada ya Familia yetu nikimaanisha baba aliwekeza sana katika elimu ambapo familia ya baba mdogo ikatokea kututenga nikama hawakupendezwa. Nilipo masomo yamenipita nahizo mali zipo chini ya mama wa kambo
Ndo mana unaambiwa fuatilia mahakamani.kwani wewe sio mtoto halali wa marehemu?kama aliwekeza kwenye elimu sasa aliwekeza nini?kwa njia gani?ili hali sasa unapata shida.

Ni kweli baba alikuwa anaumwa mpka umauti unamkuta,nakupa pole kwa hilo mkuu.lkin hata kiwanja hana,alikuwa hafanyi kazi?kwanini hakukugawia japo kiasi kidogo wakati yuko hai ili hali wewe ni mwanae na huyo mwanamke sio mama yako mzazi?

Comment zako nikizisoma nipata ukakasi sana.
Pole kwa kuondokewa na mzazi uliyekuwa unamtegemea na pole kwa changamoto unazopitia.
 
Kwa hiyo hukushirikishwa wakati wa ugawaji mali? Baada ya msiba kumalizika hamkukaa kikao kujadili suala la mirathi? Nani alichaguliwa kusimamia mali zilizoachwa na marehemu?
 
Halafu ingekuwa vizuri thread kama hizi mnakuja na utambulisho halisi.
Mfano mimi John Frank mwanafunzi wa mwaka wa 2 chuo kikuu UDSM college ya ÙDBS nikichukua BCOM.
Unaweza ku-upload student ID, selfie(passport size) etc.
Sasa wadogo zetu mnataka msaidiwe ila identity zenu mnajifisha .
 
Pole sana mkuu ndo dunia ilivo
ila mzee wako naweza sema alikosea kujitenga na ndugu zake na kuwa mbinafsi(kulingana na maelezo yako) sasa hapo nizamu yako kutengwa pia na ndugu wa mzee wako.
tukibarikiwa kuwa na chochote tujitahidi kufikiria na kesho yetu na familia zetu
 
pole kabla ya kufatilia miradhi nikuulize hvi kwani mama ako mzazi alifunga ndoa na baba ako?ama we ni mtoto wa kambo kivipi? pia mama ako wa kambo alifunga ndoa (? kwa watoto wa kambo kama mi tusipo pewa urithi na baba zetu huwa ni tabu sana maana ata sheria aitutambui
 
Kaa chini kila siku lia kwa sanaaa na kila kitu kitaenda vizuri.
 
Mimi nitakushauri kisheria nenda kaongee na ndugu wa baba yako muitishe kikao cha familia ukatengue uteuzi wa usimamizi wa mirathi ma mali zigawanywe upya kama bado zipo..ingawa utachelewa chuo kama vipi ahirisha masomo fanya mchakato huo mkuu
Hili kisheria linawezekana kabisa
 
Nenda kwenye vyombo vya sheria au kwa mfumo wa sasa piga shortcut nenda kwa mkuu wa wilaya au mkoa.

Angalizo:Utakapofanikiwa heshimu mali za mzazi wako ziendeleze miaka mitano ijayo watu watataka mrejesho.
 
Habari za humu wa JF,

Mimi ni kijana umri 24 naishi Dar es salaam. Nilikua na baba ambaye alikua yupo katika mahusiano na mama mwingine (wakambo), kwa muda alianza sumbuliwa na cancer mpaka badae ini likawa infected na mwaka jana kwa bahati mbaya baba akanitoka nikiwa bado nasoma chuo, nakumbuka nilipigiwa simu nakupewa taarifa yakua kanitoka.

Nilipigwa na buutwa nakuchukua masalia yangu ya pesa nakukata ticket ili niwahi kumuona baba hata kwa mara ya mwisho. Nilifanikiwa kufika salama na mambo yote yakaenda salama japo moyoni nikiwaza baba kaniacha nani atakua msaada na chuo sijamaliza nikiangalia kodi pia nadaiwa mawazo mengi sana kichwani!!!

Familia yangu ilikua tofauti na za ndugu zangu kidogo kwakua Late baba aliwekeza sana katika elimu na ukiangalia ba mdogo na ndugu wakaribu walikua hawana support yoyote ile.

Baada ya mambo yote kuisha kuna baadhi ya mali ziliingia katika mkono wa mama wa kambo na alivokutana namimi akaona kama nafatilia akawa mkali na kuacha kabisa kunisaidia hata pesa za matumizi ambayo alikua awali ananisaidia, nimerudi nikitegemea ataweza nisaidia au ndugu jamaa na marafiki ila mambo yamegeuka na amesema hawezi japo uwezo anao wakufanya ivo.

Nipo katika kipindi ambacho sijui nini lakufanya vyuo vimefunguliwa ada sina pakukaa sina kodi iliisha yaani naona mambo yameniharibikia kabisa na ndugu ndio walishanitenga sijui nifanye nini kwakweli nilichokua naweza nikua smart katika masomo yangu nanilipanga mambo mengi sana.

Naandika haya sipo sawa nimekaa namachozi yananilenga mtoto wa kiume sijui nifanye nini naona hakuna msaada I wish ningepata mtu wa karibu ambaye ange act kama baba, ndugu zangu hii hali inaumiza sana i wish ningepata msaada wowote.

Siku ukijua umepoteza na ukaamini umepoteza utakuwa na uwezo wa kupata kila kitu na zaid ulivyopoteza
 
Mkuu umesema baada ya mambo yote kuisha kunabaadhi ya Mali ziliingia kwenye mkono wa mama wa kambo, nani alimkabidhi?au alijichukulia tu kienyeji? maana taratibu za ugawaji mali za marehemu unafanyika pindi msiba unapoisha , ndugu wa marehemu wanakaa pamoja na kila kitu hugawanywa kwa utaratibu fulani
 
Da inasikitisha ,ila usikalili kuwa kila mama wa kambo ni mbaya,inawezekana ulimkwaza mahali muombe radhi muendelee na maisha, mama wakambo wenye ubinadam wapo
mama wa kambo akifika stage hii hapo huyo ni mnyama wazazi wetu tunawakosea sana mbona hawafanyi hivi
 
Mimi na mama wa kambo hatuna bifu kwakuwa sijawahi onesha dalili za kutaka mali yoyote. Mzee bado yupo sana na kwake hata sipajui, mali zake sizijui sasa nitadai nini.
Nishaacha kumuomba mzee lolote na hata hatuwasiliani tena, ada mwenyewe sijamalizia lakini naamini itaisha bila tatizo.
Mzee nimesave namba yake ili akinitafuta nisiulize 'we nani?'
Muhimu kwangu, nina strong bond na ukoo. Sasa ole wake mzee mimi niwe Naseeb, yeye ndo atakuwa mzee Abdul.
Mkuu mimi huyu mama wa kambo sikuwa na habari naye mpaka mzee aliponiacha kwasababu mambo mengi alikua akifanya mzee
 
Back
Top Bottom