Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Hahaha my dear nimebaki mdomo wazi kama kaka yangu Ushimen,
Siku hizi jinsia ya mtu inatambuliwa kwa kuulizwa "sijui wewe ni Dada, Mama, Aunt au Bibi", lol

Huko juu alikujibu comment yangu hakuiona amesahau kua alinijibu yupo Dar,

Hapa anasema aliniita hivyo sababu hakujua jinsia yangu kulingana na jina, LMAO,

Ndio maana nikamtakia kheir apate wa kumsaidia lakini pia abadilishe attitude kama kweli ana shida hizo alizozisema.
Nimeamua kuwa msomaji wa comments pekee hapa, maana nikifunguka nahisi nitarushiwa tu mawe
 
Mzee aliwekeza kwenye elimu, halafu elimu aliwekeza kwako Inashindwa kukusadia ?

Unashindwaje kufata grounds za kisheria Kama ulivyo elekezwa huko juu na wachangiaji kadhaa kuhusu kupata haki yako ?

Hivi ndo unasema mzee aliwekeza kwenye elimu ?

Pili Kuna doubts nyingi kwenye maelezo yako hayaja nyooka ndo maana unaona maswali kutoka kwa wadau yanakua mengi
 
Mimi na mama wa kambo hatuna bifu kwakuwa sijawahi onesha dalili za kutaka mali yoyote. Mzee bado yupo sana na kwake hata sipajui, mali zake sizijui sasa nitadai nini.
Nishaacha kumuomba mzee lolote na hata hatuwasiliani tena, ada mwenyewe sijamalizia lakini naamini itaisha bila tatizo.
Mzee nimesave namba yake ili akinitafuta nisiulize 'we nani?'
Muhimu kwangu, nina strong bond na ukoo. Sasa ole wake mzee mimi niwe Naseeb, yeye ndo atakuwa mzee Abdul.
Duu!!
 
We have the same case mkuu. Nimelelewa na mama mlezi since nafuliwa nguo mpaka leo hii nimekua mtu mzima najitegemea. Since Mzee alipovuta mpaka leo sijawahi kudai hata kijiko, although nimefaidika kwa mengi sana kutoka kwa mama ila laiti ningekuwa na pua ndefu kudai mirathi basi hapa nilipo leo ingekuwa ni ndoto kupafikia.
Nimependa ulivyo mwita mama mlezi badala ya mama wa kambo,inaleta uzuri fulani
 
Jinsia yake ingekusaidia nini katika swala la msaada wa miradhi.

Hata kama anajinsia zote kwa pamoja hupaswi kuuliza maswali ya kipuuzi namna hiyo.

Next time pangilia maneno ya kuongea na watu wazima
Huyu ndo mzee wake aliwekeza kwenye elimu yake ?

Niseme tu huyu ndugu Kama hakuna ujanja ujanja basi atakua na uwezo mdogo Sana wa kufikiri
 
Huna ndugu wengine uliozaliwa nao tumbo moja?
Upande wa mama, kina anko je
Huyo mama sio mama yangu mzazi baada ya baba kuniacha alikua kidogo ananisaidia za matumizi ikafika muda nikipiga simu ananambia utajua utakachofanya
 
Uko sawa, maana ht historia ya mama yake mzazi hajasema. Haijulikani wao walizaliwa wangapi kwa mama yao mzazi kabla ya baba yao kuoa mke mwingine.
Mkuu Path Creator hutakiwi kurudia kila comment yako habari ya mama wa kambo,mwandiko wako unanionyesha kuwa unajificha kwenye mwavuli wa mama wa kambo sana.

1.mam yako wa kambo aliwezaje kujimilikisha mali bila kikao cha familia au hata wazee wa ukoo

2. Unasema baba yako aliwekeza kwenye elimu sana,sio,ni elimu ipi aliyoiwekeza

3. Wewe ni mtoto halali wa marehemu huyo baba

4. Unasema kuwa mama yako alianza kukubadilikia baada ya kuanza kuhangaikia mirathi sio!uliangaikia kwa namna ipi

5.kuna mkuu fulani hapo juu amejaribu kukuvuta akusaidie lakini kulingana na unavyocomment huonyeshi ushirikiano ipasavyo kwanini

6. Mpka umefikia hatua ya kwenda chuo maana umeshavuka umri wa kuwa mtoto,kwanini baba yako hakukupatia japo urithi ikiwa wewe ni mwanae?

7. Kama baba aliwekeza kwenye elimu,kwenye Bank ac kuna shilingi ngapi ya kuweza kukuendeleza kielimu

8. Ina maana kwenye ukoo wenu marehemu alikuwa hapatani na ukoo mzima kisa kupenda kwake elimu

9.kwahiyo nyie mlikuwa hamna japo ndugu mmoja ambae alikuwa anawatembelea na nyie mnamtembelea

Natamani kutichape bakora kidogo kustua akili yako itoke huko ilipomaana unatoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.

JF ni kubwa hii na inawatu wakubwa wengi ila huwezi kuwajua wengine kwa ajili ya fake idz.ondoa ukakasi katika mwandiko wako upate msaada kijana.sentensi zako zinapwaya sana.

Pole kama mwandiko wangu hauonyeshi yale uyategemeayo.jibu maswali niliyokuuliza tafadhali.

Poleni kwa gazeti na kutokupangilia vizuri maswali
 
Wewe Baba ambae unapitia uzi huu..
Na unamchepuko rasmi ama sio rasmi.
Tambua kuna siku utakufa na kuwaacha watoto wako wa kwanza wakiteseka duniani, heri Mungu angekunyima uzao.
 
Akina mama wengi dawa yao ni kuwasikiliza na kuwaheshimu basi, ingawa kuna wachache wamekuwa vivuruge by nature ila wengine huwa wana react na kureciprocate vile tunawa treat wao.
Nimependa ulivyo mwita mama mlezi badala ya mama wa kambo,inaleta uzuri fulani
 
Huyu ndo mzee wake aliwekeza kwenye elimu yake ?

Niseme tu huyu ndugu Kama hakuna ujanja ujanja basi atakua na uwezo mdogo Sana wa kufikiri
💯 kweli kabisa mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: a45
Uko sawa, maana ht historia ya mama yake mzazi hajasema. Haijulikani wao walizaliwa wangapi kwa mama yao mzazi kabla ya baba yao kuoa mke mwingine.
Ni mjanja mjanja sana aise.na watu kama hawa huwa siwapendi wenye kupindisha mambo
 
Akina mama wengi dawa yao ni kuwasikiliza na kuwaheshimu basi, ingawa kuna wachache wamekuwa vivuruge by nature ila wengine huwa wana react na kureciprocate vile tunawa treat wao.
Kweli kabisa
 
Habari za humu wa JF,

Mimi ni kijana umri 24 naishi Dar es salaam. Nilikua na baba ambaye alikua yupo katika mahusiano na mama mwingine (wakambo), kwa muda alianza sumbuliwa na cancer mpaka badae ini likawa infected na mwaka jana kwa bahati mbaya baba akanitoka nikiwa bado nasoma chuo, nakumbuka nilipigiwa simu nakupewa taarifa yakua kanitoka.

Nilipigwa na butwaa nakuchukua masalia yangu ya pesa nakukata ticket ili niwahi kumuona baba hata kwa mara ya mwisho. Nilifanikiwa kufika salama na mambo yote yakaenda salama japo moyoni nikiwaza baba kaniacha nani atakua msaada na chuo sijamaliza nikiangalia kodi pia nadaiwa mawazo mengi sana kichwani!!!

Familia yangu ilikua tofauti na za ndugu zangu kidogo kwakua baba aliwekeza sana katika elimu na ukiangalia ba mdogo na ndugu wakaribu walikua hawana support yoyote ile.

Baada ya mambo yote kuisha kuna baadhi ya mali ziliingia katika mkono wa mama wa kambo na alivyokutana na mimi akaona kama nafatilia akawa mkali na kuacha kabisa kunisaidia hata pesa za matumizi ambayo alikua awali ananisaidia, nimerudi nikitegemea ataweza nisaidia au ndugu jamaa na marafiki ila mambo yamegeuka na amesema hawezi japo uwezo anao wakufanya hivo.

Nipo katika kipindi ambacho sijui nini la kufanya vyuo vimefunguliwa ada sina pa kukaa sina kodi iliisha yaani naona mambo yameniharibikia kabisa na ndugu ndio walishanitenga sijui nifanye nini kwakweli nilichokua naweza nikua smart katika masomo yangu na nilipanga mambo mengi sana.

Naandika haya sipo sawa nimekaa na machozi yananilenga mtoto wa kiume sijui nifanye nini naona hakuna msaada I wish ningepata mtu wa karibu ambaye ange act kama baba, ndugu zangu hii hali inaumiza sana i wish ningepata msaada wowote.
Mimi nina mtoto kama wewe anakaa na mama wa kambo, na mwanangu ana madai kama yako ni vitu ndivyo mnavyothamini na siyo utu hata kidogo, nilichokiona kwa umakini sana hukuwa na mapenzi na wala hukumpenda baba yako hata kidogo ila ulikuwa unamtumia kama nyenzo ya kufanikiwa kwako tu ndiyo maana kinachokuuma ni kukosa kodi ya nyumba na ada ya chuo ukipata hivyo sidhani hata kaburi la baba yako utalijenga. Mungu akinijalia vitu vyangu nakabidhi kanisa au msikiti nyie watu hamna mapenzi na baba zenu
 
Nashukuruni wakuu kwa kila idea ya mtu mmoja japo mpaka sasa solution ya kunisaidia ni bado sijaipata,kuna baadhi walijitokeza bahati mbaya mmoja akapata ban mwingine akanisaidia pesa ya chakula kwa siku hiyo.
Nilikuja kuomba msaada ila kuna mambo yameniumiza moyo kwa baadhi ya comments. Binafsi nilikua niko tayari kuja na details zote mkononi na ushahidi ila kuna baadhi wamenitafsili ndivo sivo na ndio kitu kilicho nifanya kujisikia mtu ambaye asha telekezwa tayari na lolote nitakalo ongea hakuna wakunisikiliza. Hii kitu inauma sana kama ikitokea upande wako binafsi kwasababu naamini kila mmoja ana ndoto zake katika haya maisha.
Kiukweli bado sijapata solution mpaka sasahivi nakama kuna mtu anaeweza nisaidia nikatimiza masomo yangu ya chuo pamoja na ndoto zangu au kwa lolote PM yangu ipo wazi au naweza kufika physically popote alipo hapa Dar es Salaam na evidence zote ninazo. Nanikipata kitu chochote nitarudi kwa ajili ya mrejesho. Natanguliza Shukrani.
 
Mdogo angu ww sio mtto tena ni mtu mzima tena msomi

Unaposema hujapata msaada nashindwa kuelewa unahitaj msaada wa namna gan

Hapa jf msaada unaopatikana ni msaada wa kimawazo utapokea mawazo tofauti tofauti kaa chin tumia akili yako chambua kizuri kitumie

Zipo secta mbali mbali zinazo husika na mambo haya nenda ukawaeleze

Kuna mmoja alikuambia kama huelewi pakuanzia nenda mahakaman utapata mwongozo huko huko

Back
Top Bottom