Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Mimi nina mtoto kama wewe anakaa na mama wa kambo, na mwanangu ana madai kama yako ni vitu ndivyo mnavyothamini na siyo utu hata kidogo, nilichokiona kwa umakini sana hukuwa na mapenzi na wala hukumpenda baba yako hata kidogo ila ulikuwa unamtumia kama nyenzo ya kufanikiwa kwako tu ndiyo maana kinachokuuma ni kukosa kodi ya nyumba na ada ya chuo ukipata hivyo sidhani hata kaburi la baba yako utalijenga. Mungu akinijalia vitu vyangu nakabidhi kanisa au msikiti nyie watu hamna mapenzi na baba zenu
Wewe ndo baba?
 
Unaulizwa BABA na MAMA YAKO walikuwa WAMEFUNGA NDOA?? au kwa namna nyingine elezea vizuri kivipi huyu ni MAMA WA KAMBO KWAKO?? isije ikawa mama yako ndio aliyeivuruga ndoa ya huyu unayemuita mama wa kambo. Sorry though
 
Alikua anathamini watoto wake kuwarithisha elimu kuliko mambo mengine. Ndugu wengine walikua hawajikita sana huko ndio kisa chakutengwa
Unatumia lugha ngumu na za picha, za nini hizo? Baba aliwekeza kwenye elimu ndo maana alitengwa, hapa unataka kusema nini?

Swali, je mzee kuna mali ameziacha? Kama ndiyo ongea na mama wa kambo kiupole, mwambie unaona kabisa huko mbele mtagombana, akugawie kitu kidogo kibinadamu tu ii usongeshe maisha yako, ikishindikana nenda mahakaman, maana hata ndugu zako wamekutenga kama unavyosema, ukiendelea kulia unazid kutengeneza giza, na giza likizid zaid itakuwa ngumu sana kujinasua
 
Nunua dumu la petrol choma kila kilicho cha maana alichoacha baba yako. Mkoswe wote kisha ingia mtaani pambana kama sisi
 
Mkuu Path Creator hutakiwi kurudia kila comment yako habari ya mama wa kambo,mwandiko wako unanionyesha kuwa unajificha kwenye mwavuli wa mama wa kambo sana.

1.mam yako wa kambo aliwezaje kujimilikisha mali bila kikao cha familia au hata wazee wa ukoo

2. Unasema baba yako aliwekeza kwenye elimu sana,sio,ni elimu ipi aliyoiwekeza

3. Wewe ni mtoto halali wa marehemu huyo baba

4. Unasema kuwa mama yako alianza kukubadilikia baada ya kuanza kuhangaikia mirathi sio!uliangaikia kwa namna ipi

5.kuna mkuu fulani hapo juu amejaribu kukuvuta akusaidie lakini kulingana na unavyocomment huonyeshi ushirikiano ipasavyo kwanini

6. Mpka umefikia hatua ya kwenda chuo maana umeshavuka umri wa kuwa mtoto,kwanini baba yako hakukupatia japo urithi ikiwa wewe ni mwanae?

7. Kama baba aliwekeza kwenye elimu,kwenye Bank ac kuna shilingi ngapi ya kuweza kukuendeleza kielimu

8. Ina maana kwenye ukoo wenu marehemu alikuwa hapatani na ukoo mzima kisa kupenda kwake elimu

9.kwahiyo nyie mlikuwa hamna japo ndugu mmoja ambae alikuwa anawatembelea na nyie mnamtembelea

Natamani kutichape bakora kidogo kustua akili yako itoke huko ilipomaana unatoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.

JF ni kubwa hii na inawatu wakubwa wengi ila huwezi kuwajua wengine kwa ajili ya fake idz.ondoa ukakasi katika mwandiko wako upate msaada kijana.sentensi zako zinapwaya sana.

Pole kama mwandiko wangu hauonyeshi yale uyategemeayo.jibu maswali niliyokuuliza tafadhali.

Poleni kwa gazeti na kutokupangilia vizuri maswali
Haya maswali kila mtu anajiuliza, akijibu haya maswali ndo tutapata picha kamili, maana uandishi wake ni changamoto, anadhan kama anaonge nasisi live wakat anaandika
 
Hayo maswali nimejibu yote mkuu
 
Habari za humu wa JF,

Mimi ni kijana umri 24 naishi Dar es salaam. Nilikua na baba ambaye alikua yupo katika mahusiano na mama mwingine (wakambo), kwa muda alianza sumbuliwa na cancer mpaka badae ini likawa infected na mwaka jana kwa bahati mbaya baba akanitoka nikiwa bado nasoma chuo, nakumbuka nilipigiwa simu nakupewa taarifa yakua kanitoka.

Nilipigwa na butwaa nakuchukua masalia yangu ya pesa nakukata ticket ili niwahi kumuona baba hata kwa mara ya mwisho. Nilifanikiwa kufika salama na mambo yote yakaenda salama japo moyoni nikiwaza baba kaniacha nani atakua msaada na chuo sijamaliza nikiangalia kodi pia nadaiwa mawazo mengi sana kichwani!!!

Familia yangu ilikua tofauti na za ndugu zangu kidogo kwakua baba aliwekeza sana katika elimu na ukiangalia ba mdogo na ndugu wakaribu walikua hawana support yoyote ile.

Baada ya mambo yote kuisha kuna baadhi ya mali ziliingia katika mkono wa mama wa kambo na alivyokutana na mimi akaona kama nafatilia akawa mkali na kuacha kabisa kunisaidia hata pesa za matumizi ambayo alikua awali ananisaidia, nimerudi nikitegemea ataweza nisaidia au ndugu jamaa na marafiki ila mambo yamegeuka na amesema hawezi japo uwezo anao wakufanya hivo.

Nipo katika kipindi ambacho sijui nini la kufanya vyuo vimefunguliwa ada sina pa kukaa sina kodi iliisha yaani naona mambo yameniharibikia kabisa na ndugu ndio walishanitenga sijui nifanye nini kwakweli nilichokua naweza nikua smart katika masomo yangu na nilipanga mambo mengi sana.

Naandika haya sipo sawa nimekaa na machozi yananilenga mtoto wa kiume sijui nifanye nini naona hakuna msaada I wish ningepata mtu wa karibu ambaye ange act kama baba, ndugu zangu hii hali inaumiza sana i wish ningepata msaada wowote.
Pole sana nimejarb kuvaa viatu vyako vimenishinda

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu pole sana kwa hali yako.
Tafakari upya na kwa hekima yawezekana ulimkwazwa omba msamaha. Husisha watu wake wa karibu au ndugu zake au ndugu zako wakushauri. Ikishindikana nenda ofisi za ustawi wa jamii kwenye ofisi za kata ili uweze saidiwa.

Lakini yoote tisa kumi ni kwamba wanawake nahisi kwenye kile kikao chao na shetani pale bustani ya edeni swala la mtoto wa kambo walilijadili na figisu zilipangwa pale pale.
Nimeishi na mama wa kambo. Nilimuheshimu yy na watoto wake. Baba alinieleza hulka za yule mama. Kwa hiyo kwenye kazi za nyumban tulikuwa tunajituma mm na dada yangu na wadogo zangu wawili ambao hatukuwa ni watoto wa kuzaa kwa yule mama. Lakini yule mama alikuwa anatuchukia. Kazi zoote zilikuwa zetu. Kuanzia kupika, kufua , kufanya usafi kulima bustani na za hapa na pale. Watoto wake wali starehe huku ss tunapigika. Majungu na fitina kama zoote kila saa kumtukana mama yetu ambae hakuwepo pale. Cha aajabu wanae ilikuwa mwendo wa kufeli madarasa sisi tunafaulu. Mwanae akifika chuo DISCO ilikuwa inamuhusu. Ajira sisi tumepata wanae bado wanamsubiri MAGU afungue neema. Sifurahii mtoso wake lakini laana zoote alizokuwa anatupatia zimemrudi.

Ndugu yangu pambana, muombe sana mungu akusimamie jamani mama wa kambo ni kiumbe wa tofauti sana emu tuseme na ukweli.
Baba wa kambo anaweza kuwa zaidi ya baba hata kwa asilimia elfu moja ilia mama wa kambo ni wachache wenye moyo ya utu
 
Habari za humu wa JF,

Mimi ni kijana umri 24 naishi Dar es salaam. Nilikua na baba ambaye alikua yupo katika mahusiano na mama mwingine (wakambo), kwa muda alianza sumbuliwa na cancer mpaka badae ini likawa infected na mwaka jana kwa bahati mbaya baba akanitoka nikiwa bado nasoma chuo, nakumbuka nilipigiwa simu nakupewa taarifa yakua kanitoka.

Nilipigwa na butwaa nakuchukua masalia yangu ya pesa nakukata ticket ili niwahi kumuona baba hata kwa mara ya mwisho. Nilifanikiwa kufika salama na mambo yote yakaenda salama japo moyoni nikiwaza baba kaniacha nani atakua msaada na chuo sijamaliza nikiangalia kodi pia nadaiwa mawazo mengi sana kichwani!!!

Familia yangu ilikua tofauti na za ndugu zangu kidogo kwakua baba aliwekeza sana katika elimu na ukiangalia ba mdogo na ndugu wakaribu walikua hawana support yoyote ile.

Baada ya mambo yote kuisha kuna baadhi ya mali ziliingia katika mkono wa mama wa kambo na alivyokutana na mimi akaona kama nafatilia akawa mkali na kuacha kabisa kunisaidia hata pesa za matumizi ambayo alikua awali ananisaidia, nimerudi nikitegemea ataweza nisaidia au ndugu jamaa na marafiki ila mambo yamegeuka na amesema hawezi japo uwezo anao wakufanya hivo.

Nipo katika kipindi ambacho sijui nini la kufanya vyuo vimefunguliwa ada sina pa kukaa sina kodi iliisha yaani naona mambo yameniharibikia kabisa na ndugu ndio walishanitenga sijui nifanye nini kwakweli nilichokua naweza nikua smart katika masomo yangu na nilipanga mambo mengi sana.

Naandika haya sipo sawa nimekaa na machozi yananilenga mtoto wa kiume sijui nifanye nini naona hakuna msaada I wish ningepata mtu wa karibu ambaye ange act kama baba, ndugu zangu hii hali inaumiza sana i wish ningepata msaada wowote.
Mama yako yuko wapi?
 
Back
Top Bottom