Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Path Creator

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
223
133
Habari za humu wa JF,

Mimi ni kijana umri 24 naishi Dar es salaam. Nilikua na baba ambaye alikua yupo katika mahusiano na mama mwingine (wakambo), kwa muda alianza sumbuliwa na cancer mpaka badae ini likawa infected na mwaka jana kwa bahati mbaya baba akanitoka nikiwa bado nasoma chuo, nakumbuka nilipigiwa simu nakupewa taarifa yakua kanitoka.

Nilipigwa na butwaa nakuchukua masalia yangu ya pesa nakukata ticket ili niwahi kumuona baba hata kwa mara ya mwisho. Nilifanikiwa kufika salama na mambo yote yakaenda salama japo moyoni nikiwaza baba kaniacha nani atakua msaada na chuo sijamaliza nikiangalia kodi pia nadaiwa mawazo mengi sana kichwani!!!

Familia yangu ilikua tofauti na za ndugu zangu kidogo kwakua baba aliwekeza sana katika elimu na ukiangalia ba mdogo na ndugu wakaribu walikua hawana support yoyote ile.

Baada ya mambo yote kuisha kuna baadhi ya mali ziliingia katika mkono wa mama wa kambo na alivyokutana na mimi akaona kama nafatilia akawa mkali na kuacha kabisa kunisaidia hata pesa za matumizi ambayo alikua awali ananisaidia, nimerudi nikitegemea ataweza nisaidia au ndugu jamaa na marafiki ila mambo yamegeuka na amesema hawezi japo uwezo anao wakufanya hivo.

Nipo katika kipindi ambacho sijui nini la kufanya vyuo vimefunguliwa ada sina pa kukaa sina kodi iliisha yaani naona mambo yameniharibikia kabisa na ndugu ndio walishanitenga sijui nifanye nini kwakweli nilichokua naweza nikua smart katika masomo yangu na nilipanga mambo mengi sana.

Naandika haya sipo sawa nimekaa na machozi yananilenga mtoto wa kiume sijui nifanye nini naona hakuna msaada I wish ningepata mtu wa karibu ambaye ange act kama baba, ndugu zangu hii hali inaumiza sana i wish ningepata msaada wowote.
 
Pole sana ndg! nimejaribu kuwaza kuhusu mirathi, ina maana wewe kama mtoto wa marehemu hukupata mgawo wa mirathi? umeshindwa nini kupigania haki yako ya mirathi? Pigania hilo la mirathi, ndo risasi pekee iliyobaki kukusaidia, vinginevyo utaangamia. Pole kwa mara nyingine
 
Pole sana, mali za baba yako umefuatilia kama alikuwa mfanya kazi, kazini kwake au katika biashara yake au pesa zake katika bank yake?

Unaweza ukafungua shauri la kusimamia mirathi ya mali za baba yako (kama alikuwa nazo) ili upate haki yako ikiwa ni pamoja na kulipiwa gharama za shule.
 
Da inasikitisha ,ila usikalili kuwa kila mama wa kambo ni mbaya,inawezekana ulimkwaza mahali muombe radhi muendelee na maisha, mama wakambo wenye ubinadam wapo
Sijawahi mkwanza ikitokea nikaona nimekosea hua naomba msamaha ila kwake alinichukia kisa kuanza kumfatilia
 
Pole sana ndg! nimejaribu kuwaza kuhusu mirathi, ina maana wewe kama mtoto wa marehemu hukupata mgawo wa mirathi? umeshindwa nini kupigania haki yako ya mirathi? Pigania hilo la mirathi, ndo risasi pekee iliyobaki kukusaidia, vinginevyo utaangamia. Pole kwa mara nyingine
haya mambo nilikua nikiyasikia tu mkuu ila ukiyaona kwa macho ndo utaelewa
 
Pole sana, mali za baba yako umefuatilia kama alikuwa mfanya kazi, kazini kwake au katika biashara yake au pesa zake katika bank yake?

Unaweza ukafungua shauri la kusimamia mirathi ya mali za baba yako (kama alikuwa nazo) ili upate haki yako ikiwa ni pamoja na kulipiwa gharama za shule.
Asante mkuu, nimefatilia nanikipindi ambacho outbreak imetokea nikaenda kama suprise kumbe yeye alichukizwa nakile kitendo nikimpigia simu kuomba hata matumizi naambiwa nitajua mwenyewe
 
Mimi nitakushauri kisheria nenda kaongee na ndugu wa baba yako muitishe kikao cha familia ukatengue uteuzi wa usimamizi wa mirathi ma mali zigawanywe upya kama bado zipo..ingawa utachelewa chuo kama vipi ahirisha masomo fanya mchakato huo mkuu
 
Nashukuru sana mkuu ila ukiangalia hapo juu niliandika baada ya Familia yetu nikimaanisha baba aliwekeza sana katika elimu ambapo familia ya baba mdogo ikatokea kututenga nikama hawakupendezwa. Nilipo masomo yamenipita nahizo mali zipo chini ya mama wa kambo
 
Labda niulize je ile karatasi ya uteuzi wa mirathi ipo? Mlifungua shauri la mirathi maana kama mali zipo chini ya mama unaweza kutengua mgawanyo wa mali kila mtu akapewa chake au niulize mlienda mahakamani kufanya maswala ya mirathi?
 
Mkuu muda ule nilikua namfikiria sana late baba nasikua nawaza mirathi na kijadi yetu hufata mila na desturi ila nadhan kuna mpango ulifanyika ambayo siyo yaki sawa

Mkuu hapo naona sina la kukushauri...itabidi upambane au ukamlambe miguu mama wa kambo akupe hela...
 
Nashukuru sana mkuu ila ukiangalia hapo juu niliandika baada ya Familia yetu nikimaanisha baba aliwekeza sana katika elimu ambapo familia ya baba mdogo ikatokea kututenga nikama hawakupendezwa. Nilipo masomo yamenipita nahizo mali zipo chini ya mama wa kambo
Mzee aliwekeza sana katika elimu kivipi? Na katika uwekezaji huo ikawaje ndugu wakutenge?
 
Alikua anathamini watoto wake kuwarithisha elimu kuliko mambo mengine. Ndugu wengine walikua hawajikita sana huko ndio kisa chakutengwa
 
Back
Top Bottom