Mama Samia ni Amir jeshi Mkuu au Amirat Jeshi Mkuu?

... Rais Samia akitoa order za kijeshi kwa subordinates wake jeshini kwa lugha ya Kiingereza watamwitikiaje? Yes Sir! Au Yes Madam? Au? Lete jibu.
Tumia kiswahili ndo uhoji watajibuje, wataitikia kwa kwa kiswahili, SAWA AFANDEE! Iwe kwa Samia au Mwinyi.
 
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi.

Kwa kiarabu na uislamu kiongozi wa wa kiume huitwa Amir na wakike huitwaw Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat?

Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi

Amirat Mkuu.
 
JAMANI NENO MFALME NALO NI KUTOKA LUGHA NYINGINE AMBAYO NIYA KIBANTU,KIARABU NI MAALIK KAMA NI MWANAMUME NA MAALKIYA NI MTAWALA WA KIKE.ITOSHE TU TUELEWE KUWA KWA KISWAHILI SAFI NI MFALME KWA KIINGEREZA KING,KUNA NAMNA NYINGI ZA KUFAFANUA VYEO HIVI LAKINI PIA NENO SULTAN NI LA KIARABU PIA LENYE MAANA ILEILE YA MAALIK NA NDILO JINA AMBALO WAZUNGU WANAPENDA KULITUMIA ZAIDI WANAPOTAKA KUELEZEA JUU YA MFALME KWA KIARABU,WAO WAZUNGU HUMWITA SULTAN
Kuna Sultan (Mwanaume)
na Sultana (Mwanamke)
 
Kuvaa hilo gwanda sahau Mzee, huyo mama anajitambua,anajiheshimu na anamuogopa Mola wake, unadhani huyo ni kama wale wavaa vimini, vichupi vikionekana na minywele yote ikionekana! Aise hahahahaaaa

Kwahiyo wanawake wote wanaohudumu ndani ya jeshi la polisi, JKT, JWTZ, SUMA na ulinzi na usalama wote hawamuogopi Mungu na wote ni wavaa vimini na vichupi vikionekana?
 
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi.

Kwa kiarabu na uislamu kiongozi wa wa kiume huitwa Amir na wakike huitwaw Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat?

Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi
Rais ni Rais tu awe wa jinsia ya kike au ya kiume, kwa tafsiri hiyo Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Usitafute sababu za kujichanganyisha. Isitoshe Kiswahili hakina jinsia kwenye nomino zake kama kiarabu unachopigia mfano. :oops:
 
Nimetoa tofauti ya maneno inavyotumika.
Je ni sahihi kumuita samia .MFALME SAMIA?

Hatuna Amirat kwenye Lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Kwa hiyo swali lako halina kichwa wala miguu.
Pia Tanzania haina mfumo wa Kifalme au Kimalkia.
 
Kwahiyo wanawake wote wanaohudumu ndani ya jeshi la polisi, JKT, JWTZ, SUMA na ulinzi na usalama wote hawamuogopi Mungu na wote ni wavaa vimini na vichupi vikionekana?

Hivi wewe kwa akili ya kufikiri tu, mama samia avae trouser na koti lake, huo unene alionao unadhani litamkaa vipi!!!! Si litaonyesha body yake alafu mwanze kumsema tena ooh mama samia amebadilika sikuhizi. Kwanza co lazima kuvaa hilo gwanda. Mama yetu aendelee na vazi lake la kiislamu, na ndio vazi bora na la heshma.
 
Ulimuona jana Dodoma? Alikua amevaaje?

Hilo body unalozungumzia umebahatika kuwaona wale wanawake wa JWTZ Dodoma?

By the way hakuna vasi rasmi la “KiIslam” bali Uislam unaagiza kujistiri tupu na haiba!
 
Kwa hyo ni sahihi kumuita samia kwa cheo cha KIUME?
unasema vipi hakuna amirat wakati kuna AMIR? na kinyume cha amir ni amirat?
Hatuna Amirat kwenye Lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Kwa hiyo swali lako halina kichwa wala miguu.
Pia Tanzania haina mfumo wa Kifalme au Kimalkia.
 
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi.

Kwa kiarabu na uislamu kiongozi wa wa kiume huitwa Amir na wakike huitwaw Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat?

Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi
Who cares? Magufuli akiitwa jiwe jee sasa Samia una suggest tumwite saruji au zege? Masuali mengine hayana msingi, Samia ni Kiongozi mkuu wa nchi mwite utakavyo haimbadilishi kitu!
 
Kwa hyo ni sahihi kumuita samia kwa cheo cha KIUME?
unasema vipi hakuna amirat wakati kuna AMIR? na kinyume cha amir ni amirat?
Lugha yetu ni lugha ya kiswahili, hatuashirii kwa kutofautisha kama kiarabu, english n.k. Neno amir limetoholewa kama yalivyotoholewa maneno mengine na tunayatumia tutakavyo. Mfano mzuri ni neno awamu ni neno la kiarabu "awam" lakini kwa kiarabu linatumika kumaanisha mwaka, huku kwetu ni kipindi anachotawala rais kutoka uchaguzi mmoja hadi wa pili i.e miaka mitano.
 
Hilo neno la kiswahili amiri jeshi mkuu.
La kiarabu Ni amir.
Sisi tunalitumia kwa wote awe mwanamke au mwanamme.

RIP Magufuli,RIP Ben Saanane, RIP Azory Gwanda hii ndiyo maana halisi ya kila nafsi itaonja mauti.
Ha Ha Ha Ha. Sure sure sure
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom