Mama Samia ni Amir jeshi Mkuu au Amirat Jeshi Mkuu?

Zakamwamoba

Senior Member
Jul 28, 2016
166
1,000
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi.

Kwa kiarabu kiongozi wa kiume huitwa Amir na wakike huitwa Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat?

Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi

====

BAKITA yatoa ufafanuzi wa Amiri Jeshi na Amirat

Ibara ya 33(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inabainisha kwamba kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

Hata hivyo, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuapishwa kushika nafasi hiyo kubwa zaidi ya uongozi nchini, kuliibuka utata katika matumizi ya neno 'amiri', hoja kuu ikiwa ni kwamba neno hilo linatumika kwa mwanaume na kwa mwanamke anapaswa kuitwa 'amirat'.

Baada ya kutafutwa na Nipashe jana kuzungumzia suala hilo, baraza hilo kupitia kwa Katibu Mtendaji wake, Consolata Mushi, lilibainisha kuwa neno ‘amiri’ limechukuliwa kutoka lugha ya Kiarabu na halina mgawanyo wa kijinsia.

"Haina tofauti kati ya mwanamume na mwanamke, wengi wamekuwa na maswali. Unapochukua neno katika lugha uliyoichukua maana yake haiwi mbali katika ile maana ya msingi ya lugha yako.

"Amiri Jeshi Mkuu maana yake unamzungumzia kiongozi mkuu, yaani ni kiongozi mkuu wa jeshi, ambaye anasimamia majeshi yote nchini. Ana mamlaka ya kusimamia majeshi hayo. Tulilichukua kwa lengo moja, si kuligawanya kijinsia.

"Haina tofauti kati ya mwanamume na mwanamke, wengi wamekuwa na hili swali. (Mwandishi) si wa kwanza kuuliza hili swali, kwamba aitwe amirat? Hapana!

"Tulipolichukua neno 'amiri', tulimchukua kwa maana mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. Hatukuchukua kama Kiarabu, amiri ni kwa wote. Awe mwanamume au mwanamke," alisema Mushi.

Alisema neno hilo linabeba maana moja kwa lugha ya Kiswahili na jamii inapaswa kuzingatia uongozi uliopo na cheo chake na si kuangalia neno lilikotoholewa na jinsia.

Kumekuwa na maswali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu namna ya Rais Samia atakavyoitwa kijeshi huku baadhi ya vyombo vya habari vikianza kutumia neno 'amirat' kwa kiongozi huyo.


Chanzo:
Gazeti la Nipashe 25 MAR 2021
 

bwana fundi

New Member
Dec 17, 2016
3
45
Wewe ndugu hilo neno amirijeshi na amirati jeshi si dogo kama mnavyosema, hao wanaong'ang'ania hicho cheo kiwe cha kike wana maana yao mbaya sana usiwabeze hiyo nafasi wameitafuta kwa muda mrefu.

Elewa amir kweli ni neno la kiarabu lakini lilipoingizwa kwenye kiswahili lilitoholewa kutoka lugha mama na kuwa amiri jeshi kama neno moja kwenye kiswahili hatutumii neno amir ila limebaki tu kama jina la watu kwa mfano, sultan, amri, amiri na mfaume ambapo ni mfalme watu katika baadhi ya makabila waliita hivyo, ubaya wake sasa cheo hicho kikiitwa kwa kike unakuwa ni ushahidi kuwa nchi ni ya kiislam

Tanzania tuna cheo chetu kimoja tu kwa kiswahili kwa jinsia zote amiri jeshi, maana sisi si waarabu
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
757
1,000
Nami natamani kumuona Mama ndani ya gwanda.
Tujiulize yafuatayo: Je, Mwinyi alikuwa anapiga gwanda?! What about Mkapa and later JK?! Binafsi sina jibu lakini kama hawajawahi basi tufahamu tu kwamba Bwana yule kupenda kupiga gwanda kunatokana sana na ile tabia yake ya kupenda kujikweza na kuwa na elements zake kidikteta na ndo maana alipoingia tu Ikulu, mashoga zake wakawa Kagame na Museven ambao ni ex-military wanao-excircise udikteta vizuri kama ilivyo kwa majority ya African ex-military wanaochukua Ikulu! Na mimi naamini Hayati JPM alitamani sana kama nae angekuwa ex-military na utaona refelction ya hii jindi alivyokuwa anapenda kuteua wanajeshi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom