The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 324
- 909
Angalizo Mods naomba huu uzi usiunganishwe na uzi mwingine tafadhali.
Juzi walikusifia Jana walikuchoka Leo wanakuzomea kesho watakufukuza lakini hao hao kesho kutwa watarudi tena kwako hivyo wazoee endelea kupiga kazi.
Walianza wanaojiita wanaojiita wanaharakati kupinga baadhi ya vipengele katika Mkataba huu wa BANDARI kwangu sikua na shida Sana sababu ni haki yao kuhoji matumizi sahihi ya rasilimali zao well kwakua ile tumeambiwa ni makubaliano Mkataba bado ninategemea Yale mapungufu yoote utayafanyia kazi katika Mkataba husika.
Mashaka yakaanza pale hao wanaojiita watetezi wa Bandari kuanzia kuingiza udini na ukanda katika Jambo muhimu la Kitaifa Kama hili na mbaya zaidi wakaanza kutumia Uhuru wao vibaya kwa kauli zisizo na staha hata kidogo.
Hali ikawa mbaya zaidi pale watetezi wa Bandari walipoanza kutoa vitisho kwa mamlaka nikajiuliza hii nguvu yote inayoumika katika makubaliano ambayo siyo Mkataba inatoka wapi.Sikutaka kuamini maneno ya mwanzo kuwa wanaopinga Mkataba wa Bandari ni wale wale wa karibu yake yaani wapo katika circle ya Amiri Jeshi Mkuu na kila siku wanamshauri Mambo mbalimbali,daah Mwanadamu ni wa kuogopwa Sana.
Sishangai sababu hata Mpendwa wetu JPM aliwahi kulalamikiwa kuchomekewa baadhi Watu/masuala nyeti kwa makusudi ili kuangusha Utawala wake pale alipoenda kinyume na maslahi ya Baadhi ya Watu katika system.
Nikapata mashaka sana ushabiki uliokuwa ukitumika kwa baadhi ya watetezi wa Bandari mbwembwe mahakamani kule mbeya kauli za vitisho kwa mamlaka nikaunganisha dot picha halisi nikaanza kuipata kuwa Kuna Watu kwa makusudi wameamua kumtengenezea Samia ajali ya Kisiasa na mbaya zaidi wengi wao ni miongoni mwa Watu wa karibu anaowaamini mnoo tena mnooo.
Nami kiaanza kuamini kuwa hili suala la Bandari halijaja kwa Bahati mbaya Kuna mawili
1.Mkataba ulisukwa ovyo makusudi ili kumuangusha Kisiasa kuelekea 2025
2.Mkataba ni Mzuri ukiondoa mapungufu machache yanayorekebishika Ila kwakua hauna maslahi kwao wameamua kuipa sifa mbaya kwa makusudi ili lengo lao litimie.
Kwanini nasema hivyo tukumbuke mpaka Sasa TICTS hawajapenda kutolewa Bandarini je Ni Nani anawafahamu wahusika Wakuu wa TICTS na miongoni mwao hakuna vigogo wanaohudumu serikalini? Na je hakuna miongoni mwao wenye nafasi nyeti hata katika Uongozi wa awamu hii ya Mama Samia? Na je Kama wapo na wanaona kabisa maslahi yao kupitia kampuni yao ya TICTS yanaenda kutamatishwa rasmi unadhani hawawezi kufanya usaliti kwa makusudi hata kwa kuzusha uongo unaofanan na ukweli?
Kama JPM aliwahi kulalamika waziwazi tena wengi tunamfahamu kwa hulka yake ya ukali sembuse kwa huyu Mama? Siungi mkono Mkataba mbovu lazma tulinde maslahi lakini kabla ya yote lazma tuujue ukweli halisi tusije tukaona tunamkomoa Samia sababu mwekezaji ni mwarabu halafu tukarudi kule kule JPM alipokuwa anatutoa kumbuka.
Sasa mashaka yangu yamekua maradufu baada ya Jana kuona waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC)nilijiuliza maswali kadhaa:
1.RC ina Mamlaka ya kusimamia rasilimali zetu na kushurutisha mamlaka kamili iliyowekwa na Wananchi wenye dini na wasio na dini je walikua wanazungumza kwa niaba ya Waumini wao au Nani nyuma ya pazia? Na Kama ni kwa niaba ya Waumini wao yaani wakatoliki kwanini wawe na tamko lenye amri kwa Mamlaka iliyopo Kikatiba wakati Katiba yetu haitambui mamlaka yao juu ya Serikali ya JMT?
2.RC wanapokea ruzuku kila mwaka toka serikalini kwa Mkataba wa Siri ambao hawataki huwekwe wazi wakati shule na hospitali zao Wananchi wanatozwa gharama Kubwa na kamwe TEC hawajawai kulizungumzia hili Wala kulitolea ufafanuzi sababu Ina maslahi kwao?
3.kwanini Padri Kitima na TEC yake anayoijua yeye analazimisha Mkataba kufutwa badala ya kurekebishwa penye kasoro ili kuuboresha kwa maslahi mapana ya Taifa letu sababu kila uchwao tunatafuta wawekezaji kwa Maendeleo ya Nchi yetu nani yupo nyuma ya hili?
4.Kwanini hawa Maaskofu wasingetumia haki yao Kikatiba Kama Watanzania wwngine Kuukosoa/kuupinga Mkataba wa Bandari badala ya kujivika vyeo vya kidini ambavyo kwa namna moja ama nyingine italeta mtafaruku katika Jamii ambayo Serikali yake haina dini kwa mujibu wa Katiba na pengine kuzua hatari mbaya zaidi kwa Wananchi ambao Wana dini na badala ya kuwaunganisha Watanzania itaendelea kuwagawa zaidi kwani ikitokea Mkataba mwingine Watu wakitaka kuupinga watatumia kofia ya dini ambayo haina Afya kwa Mustakabali wa Taifa letu naona wanarudia makosa ya wale mashehe wa mbeya na mwanza wakati mjadala ulipoanza hakuna kuleta Udini na Ukanda kwa maslahi ya Taifa la sivyo tutajua mnatetea maslahi yenu na waliowatuma.
Mwisho niseme tu kwa Haya machache ukweli umeshajulikana Pamoja na mapungufu ya Mkataba lakini Kuna Watu kwa makusudi Wana Jambo lao na haya yanayoendelea Nchini hayapo kwa Bahati mbaya Kuna Jambo.
suala lolote linalohusu maslahi mapana ya Taifa tuepuke kuingiza udini,ukabila,ukanda,rangi wala jinsia ni Mambo ya hatari yanayoweza kuleta machafuko ndani ya Taifa.
MAMA SAMIA MIMI NAKUOMBEA KWA MWENYEZI AKUTANGULIE KATIKA SAFARI YAKO NANAKUFIKISHE SALAMA SALIMINI UKABIDHI KIJITI KWA MWINGINE,MUNGU IBARIKI TANZANIA🇹🇿