Watu wanasinzia tu sasa hovyohovyo kwenye daladala; ile mtu amekalia tu siti na gari kujitikisa kidogo tayari usingizi na mara kadhaa udenda pia.
Panda daladala za routes zote sasa hapa Dar hali ni hiyo. Mtu anapanda buguruni sheli anashuka sokota lakini hafiki bila kusinzia. Nenda nje ya Dar, Pwani, Dodoma, Lindi, Mtwara hali ni hiyohiyo. Kesi za watu kupitishwa, sorry, kujipitisha vituo zimekuwa nyingi sasa. Mtu anazinduka usingizini tayari kapita kituo.
Haya ni matokeo ya uchunguzi wangu wa miezi mitano sasa katika maeneo niliyoyataja kwani nipo humo karibu kila siku. Dar ndipo uchunguzi wangu kwa kiasi kikubwa umefanyika (nimeichunguza dar kuhusu hili kwa 98%). Siku za nyuma hali haikuwa hivi kabisa.....
Rais Samia, hali hii imenipatia majibu kuwa ni kutokana na ugumu wa maisha mama; hali ngumu mtaani si mchezo. Vyakula haviliki, kwani wengi hawana uwezo wa kununua mchele kilo tshs. 4,000/= wala kununua maharage 3000/=.
Ada hakuna lakini mfumuko wa hivyo vifaa vya shule si mchezo, wazazi hoooi.
Hali imekuwa tafrani kiasi watu wanaumwa lakini hata hawajui kama wanaumwa, wanatembea tu na kuhangaika.
Si mkulima, si asiye mkulima; wote hoooi.
Mama mswalie mtume, fikiria namna ya kutukwamua......kama vipi mazao yazuiwe tu kutoka nje kama zamani kwani kwa sasa hata wakulima wenyewe (nazungumzia hawa wadogo wadogo ambao ndo 99%) hawana hela wala chakula; kumbe wanaofaidika na ruhusa hii ni wafanyabiashara wa mazao ya chakula na wakulima wakubwa (ambao ni 1% tu).
Nawasilisha.