mama salma huyoooo USA

Kwa nchi zilizoendelea huwezi kuta mwalimu kaferi form 4 au six anafundisha wanafunzi, ukienda Canada/UK/JAPAN/US/GERMAN/INDIA/CHINA, mwalimu lazima uwe na degree au zaidi ndo ufundishe primary/secondary etc. Hawa walimu wamesababisha wanafunzi wengi wa kitanzania kukosa confidence katika shughuli zao za kila siku akiwemo mkuu wa nchi. Lugha taabu tupu/ math ndo usiseme. Angalia mfano wa mkutano uliomalizika hapa nyumbani (World Bank/IMF), unatamani kufumba masikio na siyo macho.

Jamani,
Naomba kutofautiana na wanaosema kuwa hawana heshima kwa mwalimu wa primary na kuwa hao walimu ni wale waliofeli au sijui UPE.tUKUMBUKE TU KUWA SIYO WALIMU WOTE WA PRIMARY NI UPE au siyo kila mwalimu wa primary hajasoma vya kutosha.Hao wanaokandia walimu wa primary labda bahati mbaya sana walikumbwa na wimbi la hao walimu wa UPE ( most were indeed std seven leavers tena failures, na many started out as housegirls before "upgrading to teachers")...

Mimi binafsi nawaheshimu sana walimu wangu wa primary na wengine wao hadi sasa wana nafasi zao sehemu mbalimbali baada ya kubadili profession na hata kupandishwa vyeo.

Tukirudi kwa huyu mama yetu wa kwanza - mama Salma - binafsi namheshimu na sioni ubaya wa mwalimu wa primary kuwa na nafasi hiyo maana kila mtu kaandikiwa bahati yake.

Hata tukimkandia, tukamchambua, tukanuna..anabakia kuwa FL for the time being, na ataingia kwenye annals of history of this nation.
Kama vipi, basi tujilaumu kwa kuwachagua hao viongozi ambao hawatufai - tukaacha wale wanaofaa ( hii ni changamoto kwetu sote).
 
Last edited:
Aisee unafanya kazi yako vizuri kumpigia debe Mama Salma, hongera.
But unfortunately kama nilivyoandika huko juu, anahudhuria ex oficio lakini siyo kwa sababu anaelewa suala hili au ana anything to contribute to that meeting. So we know that this is truly just a shopping expedition.

Sikuiona hii,"Hapana wala simpigii debe Mama Kikwete,Mimi kama walio wengi humu naufahamu vizuri uwezo mdogo wa Mama wa kujieleza hata kusoma" Nia yangu ilikuwa ni kutaarifu tu kuwa Mama yupo US kwa ziara inayohusu masuala ya Afya,na si kama Mkuu PDiddy alivyoiweka thread na kuonekana kuwa kaja Kutalii.Ni kweli kuwa Mama atakuwa msikilizaji tu kwenye Mkutano huo,kwa sababu baadhi ya First Ladies walioalikwa, wanashiriki kikamilifu katika suala zima la kutokomeza ukimwi na kumuendeleza Mwanamke wa Kiafrika.

Hata hivyo Mama ameandamana na Dr.Fatma Mrisho (Mwenyekiti wa TACAIDS) kutoka ofisi ya waziri Mkuu na Dr Donan Mmbando anayetoka Wizara ya Afya (Mkurugenzi wa Magonjwa ya Maambukizi),ambao ni Wataalamu katika masuala ya Magonjwa ya maambukizi na wanaharakati wa akina MAMA.Kwa maana hiyo uwakilishi wake (Mama Kikwete) haujapwaya!
 
Mwawado mkuu: kumradhi maana niliona kama unatetea kuwa huyu mama ni true activist atakayeshiriki kikamilifu. Lakini naomba niulize kuwa baada ya kuweka bayana kuwa ameenda na wataalam na ya kuwa atakuwa msikilizaji tu, sasa kulikuwa na haja gani kwake kwenda? Maana sasa hivi serikali ina upungufu mkubwa wa pesa lakini tunaona pesa zinatumika hovyo. Hao wataalam wawili wanatosha lakini wengine kutoka hao 15 au zaidi wameenda kufanya nini?
Ndo maana naendelea kusisitiza kuwa hii ni shopping expedition except for the 2 -3 wataalam!
 
Mkuu Pdidy,Mama Salma Kikwete anakwenda Marekani katika jimbo la California,kwenye Mkutano wa Taasisi binafsi inayojulikana kama (USDFA),Mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 20/04 mpaka 22/04 katika mji wa Los Angeles,Licha ya First Lady wa Tanzania kuna First Ladies wengine 14 kutoka Africa (Kusini mwa Sahara) wamealikwa katika Mkutano huo ulioandaliwa na Celebrities Sharon Stone,Billy Zane na Danny Glover kwa kupitia Taasisi yao ya US Doctors For Africa (USDFA).Miongoni mwa watoa Mada katika Mkutano huo ni Mke wa Waziri Mkuu wa Uingereza Sarah Brown na Mke wa Governor wa California Maria Shriver Schwarzenegger.

Mkuu naomba kidogo angalia vyanzo vya habari yako,Nauli na Malazi kwa First Lady na ujumbe wake vimegharamiwa na USDFA.

Kwahiyo unanishawishi niamini JF kuna watu wanapotosha mambo?? so JF si sehemu salama kuna nzige vidudu mtu.au JF imekuwa kama maskani sehemu ya kupigia stories??
 
Kwahiyo unanishawishi niamini JF kuna watu wanapotosha mambo?? so JF si sehemu salama kuna nzige vidudu mtu.au JF imekuwa kama maskani sehemu ya kupigia stories??

Mkuu kwanza karibu sana hapa jamvini.!
Hapa mkuu watu wapo huru kujadili michango mbalimbali,fuatilia mijadala mingi watu watataka uambatanishe na uthibisho wako wa kitu unacho ongelea hapa si kijiweni eti unakurupuka tu na story za mitaani unakuja nazo hicho kitu hakipo utabanwa tu weka evidence.
 
Mama Salma ameongea jamani hata kama speech ameandikiwa kwa mujibu wa Gazeti la Daily News la leo , kasema wamewatrain watu wake kwa waume kwenye mambo ya kilimo bora, na pia wamesaidi wajawazito na magonjwa ya mama na mtoto mengine ni maelezo ya hayo hapo juu. na hao wakulima ni paprika farmers na wamesaidia watoto wa kike kupata elimu ya juu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom