Mama Ngina kanikamata leo........!!!!!

Mama Ngina kanikamata leo........!!!!!

Mtambuzi I hope ulimalizana na wa nyumbani salama. Jana nilikuhurumia sababu ni birthday ya mtoto nikasema ngoja niwaache watakaokushambulia wakushambulie mie nibaki kuona huruma tu. Watoto wa kileo wanajali sana birthday zao kutambulika na kusharehekewa.
 
Last edited by a moderator:
Jamani naomba kufahamu hii bday ni kitu gani?! yaani kwamba unamkumbusha mtu alivoingia kwenye mapambano ya dhiki, ufisadi na vurugu za mabomu ya machozi huku akitanguliziwa kofi la mgongoni kutoka kwa mkunga mzalishaji?!
 
Mama yangu....... jana 28 Feb ndiyo ilikuwa ya mama toto! Sasa sijui kama itaeleweka au nitaeleweka! Asante Mtambuzi kwa kushitua hata kama ni a day after! Najua kuna shida ila je ingekuwa ni Tarehe 29th Feb angefanyaje mwaka huu!
 
afadhali wewe umesahau kuwa ya mtoto....zali lake linaisha mapema tu. Rudi na zawadi nzuri ya birthday na useme kabisa kuwa ulikumbuka ila ulitaka kum-surprise.
mwenzio kuna mwaka nilisahau ya mzee.....kilichoniuma zaidi mpaka jana yake nilikuwa nakumbuka na nilikuwa nimeshaandaa cha kumfanyia hiyo siku.
huwa nina kawaida ya kumu-wish saa 6 usiku (ili niwe wa kwanza, lol!) hiyo siku niliwahi kulala na sijui ilikuwaje alarm haikuniamsha hiyo saa 6.
Asubuhi siku ya kazi mtu kajiandaa kwenda job ananiaga naondoka sasa, usingizini najibu "Uwe na siku na kazi njema".
Akaondoka. mara mtoto anakuja chumbani ananiambia "mum today is dad's birthday".......
kutoka nje kwani yupo! kwa mara ya kwanza nilienda ofisini kwake
angalizo!usijaribu tenamchezo huo bila taarifa
 
Hivi huu ni uzee au uzembe, nimetumiwa email jioni hii na mama Ngina. Naomba nikiri kwamba nilighafilika na sijui nijitetee vipi mpaka anielewe......

Sent:
Thursday, February 28, 2013 3:52 PM
To: xxxxxxxxxxx
Subject: Re:

hallo, leo umekumbuka hata birthday ya mtoto


I know I wont miss it.
 
Tafadhali EMT naomba maana ya signature yako, ni kiswahili lakini dah.

Tafadhali mkuu kwa heshima na taadhima.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Tafadhali EMT naomba maana ya signature yako, ni kiswahili lakini dah.

Tafadhali mkuu kwa heshima na taadhima.

Kwa msaada wa Gaijin

Nomino ya neno flirt kwa Kiswahili sanifu ni "hashuo"

Kwa hiyo kwa Kiswahili, ku-flirt ni "kujihashua" au "kuhashukwa"

Ukitaka kusema Rosa ana-flirt na Juma unaweza kusema hivi:

1. Rosa anajihashua/anamhashukia Juma (ikiwa ni Rosa tu anaetenda)

2. Rosa anahashukiana na Juma (ikiwa wote wawili wanatendeana)


Tanabahi 1
* Kwa hulka na tamaduni ya Kiswahili kuhashua/kuhashukwa hakubebi dhana kuwa kuna dhamira ya ngono kila wakati.

Unaweza kumhashua dada, kaka, mama, baba, bibi au babu yako (na bila ya shaka mke au mume wako).

Kwa hiyo mbali na kumaanisha ku-flirt, kunamaanisha pia kuonyesha mapenzi wazi wazi kwa mtu wako


Tanabahi 2
*Ukimsikia mtu kakuambia "hebu usinihashukie" jua umetukanwa tusi kubwa mno.
 
Last edited by a moderator:
Basi naomba tafsili ya mojakwamoja ya "hashuo" maaake umeweka na kidhungu (flirt), wakati mwedhio nikisikia kidhungu kichwa kinaanza kuuma EMT
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom