Mama kuanza kumwomba baba tendo la ndoa, mnaonaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama kuanza kumwomba baba tendo la ndoa, mnaonaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbunge wa CCM, Dec 3, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  katika mchango wangu leo kwenye thread moja nilitoa kisa hiki cha kweli kama mfano wa kile nilichochangia. kutokana na utata wake nimeona niweke hapa kama thread inayojitegemea ili great thinkers wa JF wapate fursa ya kuijadili kwa kina kwani inatugusa sote na hususani ndoa zetu tunazozienzi daima.

  kisa chenyewe ni hiki:

  kuna jamaa yangu mmoja mkewe alikuwa jeuri sana hadi akampiga talaka. kwa sababu ya mtoto, jama hakumwondoa nyumbani mara moja bali alimtegea aondoke mwenyewe kwa hiyari yake na wakati wote alimpa mtaumizi kamili bila kukosa. haukupita muda yule bwana alimhurumia kwa kumwona hana raha, akamhakikishia kuwa kama hataondoka kwa hiyari yake, kamwe yeye hatamfukuzza na kumtaka aondoe mawazo, waheshimiane na kulea mtoto wao mpendwa. mama akaanza kupata amani moyoni, mume akajiona hana tena uhalali na wife kwani alishamkana. akapata nyumba ndogo, na wife akabaki kulea mtoto tu. yalipomshinda wife aliomba na anaendelea kuomba kila anapotaka na sasa ni mwaka wa pili na majuzi wamebarikiwa mtoto mwingine! wanmpenda na kumlea kwa furaha.

  wasipokuambia habari yao, kamwe huwezi kujua kuwa wana talaka mikononi mwaao.

  kuna wengine alifikiri ni hadithi na wengine wakasema inafafanana na filamu moja ya kihindi, lakini ni kisa cha kweli na mimi niliyekileta si tu nilichangia na kushiriki kwa hali na mali katika harusi yao bali pia nimekuwa mshauri wao mkubwa katika maisha yao ya ndoa ndio maana ni mmoja wa watu wachache sana wanojua habari hii hapa duniani.

  kweli ndoa zina mambo. leteni maoni yenu tuwasaidie wenzetu na tujimulike nasi wenyewe tuko salama kiasi gani.

  Mungu zibarki ndoa zetu.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama ninavyosema kila siku, ubovu wa ndoa ni ile obligation inayoletwa, kama unavyoona hapo walivyoodoa obligation ya ndoa kwa talaka wanaendela kuishi vizuri.

  Si ajabu hata hiyo nyumba ndogo ikafa, wakaendelea vizuri.
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Ndoa nyingi za zamani nasikia zilikuwa zinakufa kama hivi, watu walikuwa wanaachana ila wanaendelea kuishi kwa ajili ya kuhofia malezi ya mtoto na heshima ya ndoa, lakini ndoa ilishakufa zamani.
  Hii yote ilikuwa inasababishwa kwa sababu mwanamke alikuwa anategemea pato kutoka kwa mwanaume.

  ..........Ndoa za siku hizi imekuwa tofauti, wanandoa wakiona ndoa haifanyi kazi kila mtu kivyake, hata kama ndoa ni ya kanisa au ya wapi. Hata kama ndoa ina week, mwezi, miezi au mwaka, mwanamke ana kipato chake hivyo hataki karaha na kuamua kuishi kivyake na kulea mtoto/watoto.
   
 4. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Haya ni matokeo ya kuendesha taasisi bila katiba, binafsi naamini kama ndoa ingekuwa wanandoa kabla ya kuamua kuishi pamoja waamue kuwa na rejea fulani ili pakitokea tatizo liwe ni suala la kukumbushana makubaliano ya msingi wa unganiko hilo (Ndoa).

  Kukosekana kwa katiba katika hili kukitokea tofauti yeyote katika hili kila mmoja hujichukulia maamuzi anayoona ni sahihi kwake, hapo ndipo chombo huenda mrama.
   
 5. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana nawe mkuu, baada ya obligation kuondoka , wameanza kuishi kama wapenzi japo taratibu bila wao kujua. sikumoja mama alinidokeza kuwa siku hizi baba nae taratibu na kwa uangalifu ameanza kuomba mara mojamoja! penzi limeanza upya na nyumba ndogo karibu inakufa sasa. kubwa zaidi tangu wameanza maisha yao haya mapya sijawahi kuwasuluhisha ugomvi wowote tofauti na kabla ya talaka ambapo kila siku hata usiku wa manane unagongewa, ugomvi tena!
   
 6. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  kwa kifupi wote wawili wana kazi, tena kazi ya mama stable zaidi! wote wamesoma vizuri wana elimu ya juu!

  nadhani tatizo la ndoa za siku hizi ni maadili zaidi, na sioni kama ni uchumi. mwanamke anajitahidi kuondoka kwenye nafasi yake anasogelea nafasi ya mwanamme, matokeo yake anaonekana jeuri na anapoteza mvuto kwa mwanamme. anapoanza unyenyekevu kwa mumewe, mapenzi nayo yanarudi taratibu. kumbuka kwenye tread ya msingi nilisema mahali, mwanamme alipomwona mkewe anakuwa mnyonge alimhurumia akamhakikishia kuwa hana mpango wa kumfukuza ndipo mwanmke alipopata amani.

  kuna haja ya mwanamke ku-revisit nafasi yake ndani ya ndoa, wanaume naona wako tayari kuendelea kuwapenda wake zza ama watahesimu nafasi zao
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo tuseme walizini na kupata mtoto haramu? Maana alizaa na mwanamke ambaye sio mkewe ati!
   
 8. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sioni kama kuna uzinzi hapo, kilichowatenganisha ni sheria za nchi ambazo si mara zote hutenda haki, na mwenyezi Mungu kwa upande wake anafurahi kuona bado wako pamoja kwani anasema "anachukia kuachana"
   
 9. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wangapi wanaweza haya maisha?
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kwanza wewe unayaweza ?
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  he hata wewe mshauri wao una shughuli ya ziada
   
 12. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli mwanzoni nilipata usumbufu sana, sasa nashukuru kwa ushauri wangu nimemudu kuwashauri kuepuka kutengana na sasa wanarudisha mapenzi taratibu licha ya talaka waliyonayo.

  kama washwahili wasemavyo kabla hujafa hujaumbika, naamini hii ni moja ya ndoa stable zaidi hapa duniani kwa sasa kwani waliishakufa na sasa wanaumbika upya.
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  du!
  unajua ndani ya ndoa nyingi hakun amani japo mtu wa nje unaweza kuona kuan amani,
  nimewahi kushuhidia mtu na mkewe wanawasiliana kwa simu wakati wako nyumbani, nilishangaa sana, jamaa alipomuaga mkewe mida ya jion kuwa anatoka kidogo kwa sms. yule mama alinieleza kisa kizima. hata salamu asubuhi ni hivyo hinyo kwa sms japo wamelala kitanda kimoja. wanaenda kazini pamoja kwa gari moja lakini hawaongei kabisa.
   
 14. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  khabbar njema sana hii kwa makampuni ya simu.
   
 15. GP

  GP JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hapa bado wanchanganya kidogo, kama wamerudiana hiyo talaka si waifute/waichane/wa-undo au bado hawana uhakika??
   
 16. bht

  bht JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  GP hata mie napata utata, kama wataendelea kuishi hivo na mtafaruku ukaja kutokea sijui nani atasimama wapi

  wangapi wanafahamu wazazi wawili hao walitalikiana? (Mirathi inaweza kusumbua mmoja akifariki)

  je talaka bado itakuwa valid?

  kwa muda huu wafunge ndoa upya?(maana ndoa hamna hapo)

  ngoja tusubiri kupata precedent itumike kwenye sheria ya ndoa tz

  All in all sioni tatizo mama kulianzisha kwani kuna ubaya gani?? After all its my conjugal right.....
   
 17. bht

  bht JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  sasa hawa nao wanadanganya nani kama si wao wenyewe.....
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hivi kama hawa wanaweza japo kutumiana sms hata ya kuagana kaam anatoka nadhani wana uwezo mkubwa wa kuirudisha amani kwenye ndoa yao....ndoa hizi jamani...lo
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hakuna uzinzi hapo. Hao watu hawajaachana hata kidogo. Wamepeana mapumziko ili kuona kama bado wanapendana (if they still feel each other). Na sasa unaweza kuona ni jinsi gani wanafanya uvumbuzi kwamba wanapendana sana. Kwani kama hawapendani hawangeweza kuishi nyumba moja na kushiri meza ya bwana. Lile tendo kwa watu waliooana ni very special na ukizingatia jamaa tayari ulikuwa na nyumba ndogo. Kama hawa watu hawangekuwa wanapendana, hata mama angetafuta Serengeti Boy na kuanzisha league.

  Tatizo kubwa tulilonalo kwenye ndoa zetu ni kushindwa kugundua (mapema) kwamba tunapendana sana hadi mmoja wapo anapokuwa hayuko reachable! Nadhani dawa yake ni kuongea mara kwa mara kuhusu mahusiano yetu na nini kila mmoja angependa au asingependa kufanyiwa!
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Wanafanya mambo ya kitoto tu. They are just kidding!
   
Loading...