Nelsweeter
Senior Member
- Feb 17, 2012
- 141
- 68
Mimi nilikuwa najua Chama kinapokuwa na Jumuia zake kama ilivyo kwa utamaduni na muundo wa CCM ni kwamba unaposema Jumuia ya Wanawake basi, tunategemea kiongozi wa Jumuia hiyo atakuwa mwanamke, na vilevile kwa jumuia ya vijana basi kiongozi wake anakuwa ni kijana, vilevile kwa wazazi, nilijua atakuwa mtu mfulani mwenye umri wa makamo au mzee ndio atakuwa kiongozi wa jumuia. Anyway mimi si mwanachama wa CCM nitakuwa naelewa vibaya. Nikutakie mafanikio kanisa katika harakati zako Mh KigwangalaMimi siamini sana katika factor ya umri (mkubwa ama mdogo) kwenye uongozi. Mimi naamini zaidi kwenye uwezo wa kiuongozi. Tunategemea viongozi wenye umri mdogo wawe wabunifu sana kuliko wale wazee, lakini mara nyingi tumeona matokeo kinyume na matarajio haya. Tumeona pia mafanikio makubwa yakiletwa na viongozi vijana sehemu mbalimbali, ambako viongozi wazee wameshindwa. Mfano wa Joseph Kabila Kabange anavyoimarisha demokrasia kule DRC na pia anavyojenga mabarabara na viwanja vya ndege sasa hivi kule nchini kwake, anavyojenga mahospitali na anavyotetea nchi yake kufaidika na madini na rasmlimali - haya yaliwashinda baba zake akina Kabila Sr na Mobutu Sseseseko Kukungwendu wa Zabanga (aliyekuja kufa kidhalili kabisa), tunaona mambo makubwa aliyoyafanya Paul Kagame wa Rwanda. Tunaona mafanikio makubwa ya kuleta mabadiliko ya mahusiano kati ya watu weusi na weupe kule Marekani thru non-violence movements ya kijana Dr. Martin Luther King Jr, tunaweza pia kujifunza kutoka kwa akina Mwl. Nyerere na wenzake na makubwa waliyoyafanya kwa nchi yetu na Dunia kwa ujumla...and the list goes on! Tujiulize hawa wote walikuwa wazee?
Ukiwa muumini wa mabadiliko ya ukweli basi kwa vyovyote vile utatakiwa kuniunga mkono mimi na wanamapinduzi wengine wanaojitokeza kuomba nafasi za uongozi wa chama chetu, na kisha utanipa mawazo yako bila kujali ni kijana ama ni mzee kiasi gani. Sina nia nyingine yoyote ile zaidi ya kutaka kuingia kwenye vikao vya juu vya maamuzi ya chama changu ili kushawishi mabadiliko kutokea. Chama Cha Mapinduzi kinahitaji wanamapinduzi kama mimi kwa sasa, kwanza kwa ajili ya succession planning na pili kwa ajili ya nguvu mpya ya mabadiliko wanayoyahitaji waTanzania wa sasa. Kisipoamka na kuchukua nguvu mpya on board, kitayumba na hii itapelekea Taifa pia kuyumba. Tulio na nia nzuri na nchi yetu, na chama chetu tunachukua hatua kwa kuingia ndani na kushawishi mabadiliko! Wenzetu mjue kuwa tunachukua risk kubwa sana na mnachoweza kufanya si kingine tu bali kutuunga mkono na zaidi kututia moyo.
Najipanga kuomba kibali cha kugombea na nina imani kabisa chama changu kitanipa fursa hiyo ili nifike mbele ya wanachama wenzangu wa jumuiya hiyo kutafuta ushindi na ninaamini wapiga kura watanielewa na kunipa kura za ushindi ili tufanye kazi pamoja.