Mama Kilango v/s Sophia Simba ndani ya uchaguzi wa UWT...

Lazima mtu atoe ulimi nje hapo... Hako kazee ka Anna Abdallah si kamekuwa kabunge ka kupewa kwa miongo kibao kanazidiwa hata na Halima Mdee ambaye amepambana kivyake...

Hoja ya msingi ni kufuta kabisa hivyo viti maalumu period!!

Ukomo ni sawa ingawa mtazamo wangu kuvifuta ingekuwa bora zaidi, si wanalilia usawa siku zote? tupambane basi majimboni wote ili tudhihirishe huo usawa wanaoulilia
 
Ni kweli hoja hiyo ilianzia kwa mama Anna Abdallah, Sophia ameikuta hiyo hoja. Lakini ni sawa, kwanini hawa wabunge wanawake wanang'ang'ania viti maalum? Kuna watu wamekalia viti maalumu kwa zaidi ya miaka 15 -20 kama vile Elizabeth Batenga, Mariam Mfaki, Maua daftari, Diana Chilolo, Zakia Meghji, Kidawa salehe na wengineo. Uzoefu walioupata unawatosha waende wakapambane majimboni, wanaogopa nini?

Kwa hiyo na sofia Simba next time anaenda jimboni? kwa sababu yuko viti maalumu zaidi ya kipindi kimoja.
 
Mkuu, nadhani Zakia Meghji sio mbunge wa viti maalu, ni mteule wa Rais kwenye nafasi zake 10 kama sijakosea. Daima huyu mama viti maalum huwa anashindwa na kuokoka katika kapu lakini kuanzia 2005 aliachana na viti maalum akabaki na jimbo lake la IKULU

Zakia Meghji amekuwa mbunge wa Viti maalum kwa miaka 15 (including kipindi 1 cha kwenye kapu), ni kuanzia 2010 ndio amekuwa Mbunge wa kuteuliwa na rais. Nimezungumzia waliokuwa viti maalum kwa miaka 15-20.
 
Kwa hiyo na sofia Simba next time anaenda jimboni? kwa sababu yuko viti maalumu zaidi ya kipindi kimoja.

Sophia Simba alikuwa Mbunge wa viti Maalum kuanzia 2000 - 2010. Akaenda jimboni (Ilala) ambako alishindwa. Ngekewa ya JK ikamuangukia kwa kuteuliwa ktk nafasi zake 10. Lakini kwa nafasi ya Mwenyekiti wa UWT anaingia Bungeni by virtue of her position. Kama hatachaguliwa tena kuwa Mkiti wa UWT hapo ndipo ngoma inogile...maana hana ujanja, ni kwenda jimboni au aanze!
 
Sophia Simba alikuwa Mbunge wa viti Maalum kuanzia 2000 - 2010. Akaenda jimboni (Ilala) ambako alishindwa. Ngekewa ya JK ikamuangukia kwa kuteuliwa ktk nafasi zake 10. Lakini kwa nafasi ya Mwenyekiti wa UWT anaingia Bungeni by virtue of her position. Kama hatachaguliwa tena kuwa Mkiti wa UWT hapo ndipo ngoma inogile...maana hana ujanja, ni kwenda jimboni au aanze!

Hapana Mkuu Sofia Simba sio mbunge wa kuteuliwa na Rais, yeye kaingia nankundi la viti maalum la UWT ambapo nafasi ya kwanza na ya pili huwa ni mwenyekiti na katibu wake kabla wengine hawajaanza kupigana vikumbo. Ila Meghji ndie ametumia jimbo la IKULU (uteuzi wa rais) kuanzia 2005 na sasa 2010 pia
 
Mwenyekiti wa UWT taifa Sofia Simba, ameanza kupangua shutuma zinazoelekezwa kwake na kumkwaza kutetea nafasi yake dhidi ya Anna Kilango ambaye anadaiwa kuiwania nafasi hiyo kwa udi na uvumba.

Hoja ambazo zinatumiwa na kundi la Mama Kilango kumuangamiza Sofia simba ni pamoja na ile ya kutaka kuwepo kwa ukomo wa wabunge wa viti maalum na kuwa miaka kumi, baada ya hapo wabunge hao wakatafute majimbo na sio viti maalum tena.

Sofia simba akiwa Dodoma, amewahutubia wenyeviti wa UWT wa mikoa na wilaya zote wanaohudhuria semina elekezi na ametumia jukwaa hilo amekanusha kuwa sio yeye aliyeanzisha hoja hiyo ya ukomo wa viti maalum, lakini akasema ni vema ukawepo ukomo huo.

Amesukuma zigo hilo kwa Anna Abdala, Anna Komu na Thabita Siwale kuwa wao ndio waasisi wa hoja hiyo ya ukomo na anachokifanya yeye ni kutekeleza aliyoyakuta.

Kambi ya Mama Kilango imeibeba hoja hiyo kama fimbo dhidi ya Sofia Simba ambapo wabunge wengi wa viti maalum CCM ambao wanaonekana kutokuwa na uwezo wa kwenda kuwania ubunge majimboni wamekuwa wakipinga wazo la ukomo wa vipindi viwili, na hivyo kwenda kinyume na mwenyekiti wao.

Uchaguzi wa UWT taifa unatarajia kufanyika baadae mwaka huu ambapo kuna mchuano mkali wa chini kwa chini kati ya mwenyekiit wa sasa Sofia Simba na Mama Kilango ambaye ameanza kampeni za chini kwa chini.
Hivi wanasiasa wa Tanzania watapata lini akili? KInachomfanya yeye aanze kuikana hiyo hoja na baadaye kuikumbatia nini. Kuna tofauti katika kuanzisha hoja na kuishabikia, kama anaishabikia, kwa nini akanushe kuwa yeye si aliyeianzisha wakati hoja haihusu nani alianzisha hoja?
nadhani sofia simba na wanasiasa wengine wanapaswa kujifunza kwua na tabia ya kusimamia hoja zao... hizi blahblah hazitawasaidia. wakiwa wanasimamia hoja fulani nduio itakuwa rahisi zaidi kwuapima
 
Lakini hawa wote si wabunge hawa, sasa na zile kanuni za NEC ya CCM iliyoisha zinafanyaje kazi hapa, maana naona wabunge wa CCM bado wanaendelea kujipanga tu kutafuta vyeo kwenye chama chao cha magamba. Dr. Hamisi Kigwangala naye tayari ameishatangaza nia kuutaka Uenyekiti wa Wazazi Taifa, anatumwa na Membe huyu kuingia kamati kuu ili amtetee kwenye vita ya Urais 2015. Sofia Simba naye anatumwa na Lowasa ili kumtetea 2015. Antony Mavunde naye anagombea uenyekiti vijana CCM Taifa, naye sijui anatumwa na nani...makundi, makundi, makundi na ccm

yetu macho tu, waacheni wafu wazikane
 
Wazazi hii mishangingi ya CCM isitupotezee muda dawa ya viti maalum ni kuvifuta kabisa maana imekuwa ni nafasi ya fedheha kwa wanawake; wote wanaoingia wamebebwa kiaina ushangingi mtupu hawanatija zaidi ya kula bure!kila mbunge achaguliwe na wananchi?
 
Wazazi hii mishangingi ya CCM isitupotezee muda dawa ya viti maalum ni kuvifuta kabisa maana imekuwa ni nafasi ya fedheha kwa wanawake; wote wanaoingia wamebebwa kiaina ushangingi mtupu hawanatija zaidi ya kula bure!kila mbunge achaguliwe na wananchi?
teh teh teh Kigwangala naye shangingi la CCM.........na Mavunde naye ouwiiii
 
hawa wanawake wawili wamekutana wote maneno mingi! sisi tunachoomba ni huo ukomo wa viti maalumu nimechoka kuwasikia kina Diana Chilolo, Maua Daftari...et el wanatumalizia pesa zetu bure
 
kwa mara ya kwanza nakubaliana na mama Sofia lion kuwa ni lazima kuwe na ukomo wa viti maalumu kwa hawa wapiga makofi wengi na wakinamama wa kura za ndio bungeni
 
Nimesoma kwenye thread nyingine kuwa Anne Kilango, ambaye inasadikiwa kuwa ni mfuasi mkubwa na wa karibu wa makundi yanayokubaliana ya wanaccm waliojipambanua kuwa waadilifu na wapinga ufisadi, atapambana na Mama Sophia Simba (ambaye ni mwenyekiti incumbent wa jumuiya hiyo na ambaye ni swahiba wa karibu sana wa Lowassa) kwenye kiti cha Jumuiya ya wanawake Tanzania.

Aidha kuna taarifa nimezisoma kwenye thread nyingine hapa JF kuwa Kigwangalla, ambaye imesemwa kule kuwa anatumwa na Membe (na kundi la akina Anne Kilango) kugombea wenyekiti wa umoja wa wazazi Taifa ili amtetee kwenye vikao vya juu vya chama wakati wa mchakato wa Urais 2015, je hapa Lowassa amejipanga kupandikiza nani wa kuchuana naye?

Vita za makundi ya CCM zinazidi kuwa interesting
 
Zul, ni kweli mimi niliishawahi kutangaza nia ya kugombea Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, na tena azma yangu hii ni ya siku nyingi na niliishawaambia wengi walio karibu yangu, na hii ni azma yangu binafsi na wala haina shinikizo hata ushawishi wa mtu yeyote yule!

Sijawahi kuwa na mazungumzo ya faragha na mtu yeyote yule anayetajwa kuwania Urais 2015 na mimi nadhani muda bado sana kuchagua ni nani nitakayemuunga mkono. wanaCCM wenzangu wenye uwezo wa kuwania Urais ni wengi sana tu na ni mapema mno kuchagua wa kumuunga mkono, vipi kama mimi mwenyewe nikiamua kugombea Urais?

Sasakwa nini ufikirie kuwa ninatumwa na mtu yeyote yule?!
 
Naona dr Hamis anajitahidi, ila siasa zinatakiwa uwe makini sana hata mambo unayoandika au kusema.
Namshauri ajaribu kufuatilia na kusoma vitabu mbalimbali vinavyoelezea mbinu mbali mbali zilizotumiwa na wanasiasa maarufu duniani kuleta mabadiliko ya jamii zao
Kwa sasa hivi ningekushauri tumia vyombo vya habari Kwa tahadhari kubwa sana; ndivyo vitamavyo kupandisha na baadae kukushusha !
 
Zul, ni kweli mimi niliishawahi kutangaza nia ya kugombea Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, na tena azma yangu hii ni ya siku nyingi na niliishawaambia wengi walio karibu yangu, na hii ni azma yangu binafsi na wala haina shinikizo hata ushawishi wa mtu yeyote yule! Sijawahi kuwa na mazungumzo ya faragha na mtu yeyote yule anayetajwa kuwania Urais 2015 na mimi nadhani muda bado sana kuchagua ni nani nitakayemuunga mkono. wanaCCM wenzangu wenye uwezo wa kuwania Urais ni wengi sana tu na ni mapema mno kuchagua wa kumuunga mkono, vipi kama mimi mwenyewe nikiamua kugombea Urais? Sasa kwa nini ufikirie kuwa ninatumwa na mtu yeyote yule?!

Kwa upande wangu ktk vijana ninao waheshimu ndani ya ccm nawe ni mmoja wapo,kwani wewe huwa ni mkweli na muwazi na hii imekuletea matatizo hata ndani ya chama kwa kusema ukweli,huwa naamini kuwa msema ukweli hapendwi daima unachotakiwa kukifanya ni kusimamia ktk ukweli kwani utakuweka huru na kamwe usikubari kutumiwa na wachache mwisho wa siku utajuta

nakuunga mkono ktk haraakati zako,ila ninawasiwasi sana sijui kama watakupa nafasi hiyo kutokana na kuwa umekuwa ukisema ukweli kila wakati

mungu akuongoze
 
Mhe. Hamisi Kigwangala, pengine unataka kulewa sifa hadi kuchafua hadhi yako. Bado hujafikia hatua kubwa kiasi hicho nawe tukuweke na kukufananisha na magwiji na wanasiasa maarufu hapa Tanzania. Na kama ni umri wa mtoto, basi umri wako ni kama mtoto anayetambaa. Ushauri wa bure ni kuwa kaa kwanza na ujipange vyema kisiasa na usome vyema mchezo, alama za nyakati zitakuambia na mwisho jaribu kuheshimu muda na hakika utafanikiwa daima. Vinginevyo nakutakia safari ndefu katika siasa za uvumilivu na stamina iliyotukuka.
 
Kigwangala mbona unaoneka umri wako bado mdogo kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi?. Mimi nilijua Jumuia hii ni ya wazee, kama ilivyokuwa kwa walipita akina, Gibons Mwaikambo, Idd Simba and Mhina mbao nawajua kwa umri wangu. Kumbe hamzingatii umri ni mvurugano tu. Sitashangaa mzee Ngombale akichukua form ya UVCCM akichuana na Beno Malisa LOL!
 
Back
Top Bottom