nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
HIYO SIYO KWELI; NDANI YA CCM wanataka kuondoa Ubunge wa viti Maalumu toka UWT kwahiyo sidhani kama Kilango ataacha Jimbo anende kwenye JUMUIA...
Soma Habari Chini...
[h=2]Sophia Simba awashukia wabunge viti maalumu[/h]JUMATANO, 14 MACHI 2012 07:34 NA DEBORA SANJA, DODOMA.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba, amedai kushangazwa na baadhi ya wabunge wa viti maalumu kumtuhumu kuwa ni yeye aliyeanzisha suala la kuwapo kwa ukomo wa ubunge wa viti maalumu vya CCM.
Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana, wakati akifungua semina elekezi kwa wenyeviti wa UWT wa mikoa na wilaya za Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema suala la kuwapo kwa ukomo wa ubunge wa viti maalumu hakulianzisha yeye ndani ya UWT, lakini alisema si vibaya likawepo.
"Ni kweli kuwa mimi ni muumini wa uwapo kwa ukomo wa ubunge wa viti maalumu lakini siye niliyeanzisha.
"Suala hili lilikuwapo tangu mwaka 1995 na lilianzishwa na waasisi wa UWT kwa nia njema tu, akiwamo Anna Abdalah, Anna Komu na Thabita Siwale.
"Lakini nashangaa baadhi ya wabunge wa viti maalumu wakipita mikoani wanalalamika wakisema kuwa mimi ndiye niliyelianzisha suala hili la ukomo wa ubunge wa viti maalumu.
"Kauli hizi za wabunge zinanishangaza kwa kuwa si ukweli kuwa mimi ndiye niliyelipeleka suala la ukomo wa ubunge wa viti maalumu katika Baraza Kuu la UWT, wakati ukweli unajulikana," alisema Simba.
Alisema wapo baadhi ya wabunge wa viti maalumu waliopo sasa anawafahamu awali walikuwa wanataka kuwapo na ukomo wa ubunge huo kabla hawajawa wabunge, lakini kwa sasa wanapinga.
Alisema pamoja na malalamiko hayo bado ukomo ni muhimu, kwa kuwa unawezesha wengine nao kushika nafasi za ubunge kupitia viti maalumu.
Alisema lengo la kupendekeza kuwapo kwa ukomo wa kugombea ubunge wa viti maalumu lilikuwa ni kuwajengea uwezo wanawake ili nao baada ya muda fulani waweze kusimama wenyewe kugombea.
"Kama wewe umesoma umefika darasa la saba bado tu unang'ang'ania hapo hutaki kutoka, hao wa darasa la sita waende wapi sasa," alisema Simba.
Aidha, aliwataka wanawake hao kulijadili suala hilo la ukomo wa viti maalumu kwa makini na kutoa uamuzi unaofaa.
Aliwataka wanawake nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za chama na jumuiya zake.
Mbali na kujitokeza kugombea nafasi hizo, aliwataka kujitokeza kutoa maoni kuhusiana na uundwaji wa Katiba mpya.
"Nia ni kuhakikisha mambo yote muhimu ambayo mwanamke anastahili kulindwa katika Katiba yanapata nafasi ya kuingizwa kwa manufaa ya akina mama wa Tanzania," alisema Simba.