Mama Karume, hapa umechemka!

Mama Karume, hapa umechemka!

Lakini mwalimu hakukosea mwanzo kabisa alitamka kuwa kama angekuwa na uwezo basi hako kakisiwa angekasuumiza mbali sana baharini maana kwa ukaribu tulio nao basi katakuja kutusumbua sana siku za usoni,na haya ndio yanayotokea,mtu kama mama Karume alitakiwa kuwa kimya na kuwashauri viongozi kwa kuwaita nyumbani kwake,lakini yeye anaona kupayuka kwenye vyombo vya habari ndio labda atasikika,hamuoni mwenzie mama Maria?Sio kosa lake lakini nasikia yale matunda (yanaitwa madoriani yananuka kama kinyesi)wanayokula nasikia huwa yanawapunguzia uwezo wa kufikiri..
 
Njaa kweli kitu kibaya. Yeye alitaka atendewe kama Karume utadhani yeye ni Karume. Kuwa mke au mtoto wa Karume isiwe taabu. Kama serikali ya Muungano ilimtelekeza mbona serikali ya mwanawe ilimpa kila kitu? Huyu mama sijui uzee sijui kisomo. Hakupaswa kujiingiza kwenye upuuzi wa Uamsho ambao kimsingi si uamsho kitu bali uangusho. Anasema eti kati ya mabalozi 33 watatu ni kutoka Zanzibar. Alitaka nusu kwa nusu na kipande hichi cha nchi? Mbona Zanzibar ni dogo kuliko hata wilaya ya Lushoto? Mama Karume kweli umechemsha ile mbaya.
 
Khee..sasa anataka serikali impelekee vibua nfo aone inamtunza?
 
kuwa mke wa kiongozi haimaanishi una busara yawezekana alikupenda kwa sababu we ni mrembo ila kichwani hakujali. Kama si uroho ni nini na uhudumiwe vp ilhali wanao wamepewa 2 walikuwa na vyeo vya kupewa. Karume mwanao kapewa cheo badala ya mshindi wa kura Makamu wa rais Dr. Ghalib Bilal na yule mwanao balozi! unapaswa kushukuru na si kulaum. akili za Uamsho changanya na za kwako si kukurupuka tu
Bado natafuta button ya LIKE nikugongee.
 
Jamani mwacheni Mama wa watu. Uzee ni kama utoto. Bolt na nut za ubongo wake lazima zimelegea kutokana na umri na akiendelea hivyo hali itakuwa mbaya zaidi. Ni watu wachache sana ambao wakizeeka ubongo wao hubaki intact. Hao ni kama Baba yetu wa Taifa Mwl. Nyerere.
 
She wants red carpet...as far sa maslow's hierarchy of needs is concerned, she wants 'self actualization'
 
KUJUA KWINGI MBELE KIIZA! HAWA VIUMBE WA AJABU MADHARA YAO NI MADOGO KULIKO WANYAMA KAMA MBWA, NGURUWE , KIMA, MAMBA....... MUNANG'ANG'ANIA NINI KWA KITU KISO MASLAH ! TUKO KITU KIMOJA ZANZIBAR YETU KWANZA! UTAZAA KWA UCHUNGU! foolish is foolish he go to school!

Hahahahaaaaaa duh check nilipopigia mstari na kubold...... is that English or? Thanx 4 knowing dat yo messing with a bold elite. Kumbe uwezo wako mdogo kiasi hiki?????.......Take yo land bro we do not need it at all huh!
 
ukweli ni mmoja, wazanzibari walio wengi wawe viongozi au wa kawaida, wamechoka na aina hii ya muungano

sasa tunamtaka NAPE NNAUYE aliesema UAMSHO ni kikundi cha wahuni, amsikie mama wa muasisi wa taifa la Tanzania akifunguka.


ukweli muungano huu umewabana sana wazanzibari kila idara, bahati nzuri au mbaya wazanzibari ni wavumilivu na wamevumilia kwa mda mrefu.

zanzibar ni nchi sawa na Tanganyika, nchi mbili zilizohuru zimeungana kuunda taifa moja, iweje taifa moja lijigeuze kuwa yy ndio mwenye sauti na haki zaidi kuliko mwengine?


rwanda na Burundi ni nchi ndogo kwenye muungano wa EAC na tunaelekea kwenye Federation, twambieni ushiriki wake kwenye EAC uko chini kuliko Tanzania kwa kuwa ni kubwa, na ina uchumi mkubwa? hivi EAC wanapobadilishana uongozi wanaaangalia ukubwa au wataalamu na kusema kagame hamna ww huna uzoefu mwache JK aendelee?


wakati umefika tuweke mambo sawa kwenye muungano au tugawane mbao
 
Naona WaTanganyika kila mkiagwa mnajidai kama hamsikii au hamtufahamu .

Sawa mkuu, ila unafiki wa viongozi wengi wa visiwani sasa ni dhahiri.

Tanganyikans take note
 
Sasa kachemka nini.

Mseme nyinyi tu wakisema wao huo mwao?

Tusaidie unayeona kasema kitu, manake mie nimeona kuwa malalamiko yake muungano uvunjwe kwa kuwa hatunzwi!
 
[h=1]
4.JPG
[/h]Written by Foum // 16/07/2012 // Habari // 12 Comments


Mwananchi online version 16.07.2012
Monday, 16 July 2012 14:39
Mwandishi Wetu
WAKATI taifa likiwa katika mchakato wa kuelekea kupata Katiba Mpya, Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mama Fatma Karume ameibuka na kusema kama mumewe (marehemu Abeid Aman Karume) angekuwapo, baadhi ya mambo yanayofanywa na Serikali kuhusu Muungano sasa asingeyakubali.
Akizungumza katika mahojiano maalumu katika Kipindi cha Kutoka Zanzibar kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Channel Ten, mwishoni mwa wiki Mama Karume alisema kuwa, Muungano una kero nyingi ambazo sasa zinauingiza katika matatizo.
Alisema kero hizo hata mumewe marehemu Abeid Aman Karume angekuwa hai, asingezikubali.
Mama Karume, ambaye alijinasibu kama muumini mkubwa wa Muungano, alisema mumewe hakuiunganisha Zanzibar ili imezwe bali, alitaka nchi zote mbili za Muungano ziunganishwe na kunufaika kwa usawa.
“Mzee Karume alikubali Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa aliamini, kutatokea taifa moja lenye nguvu,” alifafanua Mama Karume na kuongeza:
“Alijifunza kutoka Marekani ambayo ni Muungano wa majimbo mengi na iliyokuwa Muungano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Sovieti (USSR). Alijua Tanzania nayo itakuwa na nguvu za kisiasa na kiuchumi.”
Mama Karume pia alifahamisha kuwa alikutana na viongozi wa Kundi la Uamsho lililoko Zanzibar na kuwasikiliza na kusema kuwa, anaunga mkono madai yao.
Hivi karibuni Kundi la Uamsho lilisababisha kuzuka kwa vurugu zilizoambatana na kuchoma makanisa na kuongoza mijadala mikali ya kupinga Muungano, kiasi cha kufanya baadhi ya viongozi wake kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
“Unajua vijana wa siku hizi wanajua mengi yanayoendelea kwenye Muungano. Kwa sasa na kwa kweli napenda kusema hawa watu wa Uamsho walinifuata nyumbani na wakanieleza kero zao kuhusiana na Muungano kwa kweli wana hoja,” alisema na kuongeza:
“Mimi naupenda sana Muungano lakini, kwa sasa nadhani una matatizo mengi, ambayo yanapaswa kujadiliwa kwa ukweli na uwazi. Nadhani hawa watu wa Uamsho wasikilizwe,” alisema Mama Karume, ambaye mumewe aliuawa Aprili 7, 1972 katika eneo la Kisiwandui Zanzibar.
Uteuzi wa watendaji Muungano
Pia Mama Karume alisema kuwa, uteuzi wa viongozi wa taasisi ambazo zinatakiwa kuwa za Muungano una walakini akisema; katika na uteuzi wa mabalozi, Zanzibar ina mabalozi watatu kati ya 33 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.
Pia alisema uongozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tangu ianzishwe mwaka 1966, hasa Gavana hajawahi teuliwa kutoka Zanzibar.
Alikiri kuwa kuna Naibu Gavana kutoka Zanzibar, lakini alidai chini yake amewekewa watu wawili kutoka Bara. Naibu Gavana, ambaye anatoka Zanzibar anaitwa Juma Reli (Anahusika na Utawala).
“Hivi ni haki kweli Zanzibar kuwa na mabalozi watatu wa Tanzania au kuwa na Naibu Gavana aliyewekewa wasaidizi wawili? Nadhani kuna tatizo hapa. Haya mambo lazima yaongelewe,” alisema mama Karume.
Alisema hakubaliani na jinsi suala zima la usimamizi wa fedha linavyosimamiwa na Serikali ya Muungano.
Alisisitiza hata mume wake, Karume angekuwa hai mambo hayo asingekubaliana nayo, kwani tangu mwanzo alikuwa anavutana na Muasisi mwenzake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
“Unajua, Mzee Karume alipokuwa hai alikuwa hataki masuala ya fedha na sarafu kuwa ya Muungano. Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kumtuma Waziri wake wa Fedha, Amir Jamal kuja Zanzibar na alikataa kutoa fedha za Zanzibar kwenda Benki Kuu,” alisema mama Karume.
Aliongeza; “Baada ya kitendo kile cha kumkatalia Jamal, nilimuuliza Mzee Karume inakuwaje anakataa kutoa fedha zile… Aliniambia kuwa kinachozalishwa Zanzibar kitabakia kuwa cha huku kwani haiwezekani kwa kisiwa kulisha nchi kubwa ya Tanganyika”.
Adai katelekezwa
Katika hatua nyingine, Mama Karume alidai kuwa pamoja na kuwa mke wa mwasisi wa Muungano lakini, bado hajanufaika nao.
Mama Karume alilalamika kuwa, ametelekezwa na Serikali ya Muungano licha ya ukweli kwamba, mumewe alifariki akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Alilalamika kwamba hajahudumiwa chochote na Serikali ya Muungano tangu mumewe afariki bali amekuwa akihudumiwa na Serikali ya Zanzibar na ndugu zake wa karibu.
“Hawa watu wa Serikali ya Muungano walinitelekeza maana hawajanisaidia chochote tangu Mzee Karume afariki.
“Kinachonishangaza ni wake za Makamu wa Rais wa Muungano waliofuata baada ya Mzee Karume wanaangaliwa na hata kupelekwa nje kwa matibabu,” alisema na kuongeza;
“Ninaendesha maisha yangu vizuri, lakini kwa kweli sijasaidiwa na lolote na Serikali ya Muungano pamoja na ukweli kuwa mume wangu ni mwanzilishi wa Muungano huu.”
Mtikisiko wa Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika siku za karibuni, umekuwa ukipita katika kipindi kigumu huku wanasiasa, wanaharakati na wananchi wakihoji muundo wake.
Wafuasi wa Kundi la Uamsho liliko Zanzibar walikamatwa hivi karibuni, wakihusishwa na uchomaji makanisa na uendeshaji wa mijadala ya kuelezea kero za Muungano.
Hata hivyo, malalamiko hayajaanza leo kwani yamekuwako miaka na miaka kiasi cha kufanya mwaka 1984, Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, Waziri Kiongozi Ramadhan Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Bashir Swanzey kulazimishwa kujiuzulu katika kile kilichoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa huko Zanzibar.
Tayari suala hilo la Muungano limeanza kuibua mjadala visiwani Zanzibar katika mchakato wa kupokea maoni unaofanywa na Tume ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba.
 
Tusaidie unayeona kasema kitu, manake mie nimeona kuwa malalamiko yake muungano uvunjwe kwa kuwa hatunzwi!

Na haya hujayaona?:

Fatuma ambaye ni mamam mzazi wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliitaka serikali ya Muungano kuwa na mgawanyao sawa wa fedha na madaraka.

"Mimi naupenda sana Muungano lakini, kwa sasa nadhani una matatizo mengi, ambayo yanapaswa kujadiliwa kwa ukweli na uwazi. Nadhani hawa watu wa Uamsho wasikilizwe,"

Pia alisema uongozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tangu ianzishwe mwaka 1966, hasa Gavana hajawahi teuliwa kutoka Zanzibar.

Amma kweli, mna macho lakini hayaoni.
 
Huyu mama huwa hana LUKU mdomoni mwake. Niliwahi kumuona kwenye TV akisimulia mkesha wa siku ya Mapinduzi. Alisema kwamba wakati akina John Okello and Co. wanafanya Mapinduzi, Yeye na Karume Sr. Walikuwa ndani wamelala usingizi wa pono. Karume Sr. alikuja kuchukuliwa asubuhi wakati Mapinduzi tayari yameshafanyika.

Ingawa ni kweli lakini sikutegemea mtu ambaye alishawahi kuwa first lady kuongea hivyo.
 
unguruma mama usikae kimya huna haja ya kufa na kijiba cha roho muungano utengeneze wewe wengine wafaidi lool usikubali mwanamke wee
 
Hivi yule mzee wetu Karume ana wake wangapi vile? Na kila moja anawatoto wangapi na akina nani na wako wapi? Nisaidieni
 
Mie nadhani kuna dhana ya mfumo kristo ndo inasababisha yote haya yatokee.
 
Back
Top Bottom