Mama Karume, hapa umechemka!

Mama Karume, hapa umechemka!

Anataka msafara na pikipiki nini ili ajue tunamtambua? Haka kanchi bana kana vuimbe wa ajabu kama konokono, ngiri, mende, fisi, na jamii flani ya binadamu....
KUJUA KWINGI MBELE KIIZA! HAWA VIUMBE WA AJABU MADHARA YAO NI MADOGO KULIKO WANYAMA KAMA MBWA, NGURUWE , KIMA, MAMBA....... MUNANG'ANG'ANIA NINI KWA KITU KISO MASLAH ! TUKO KITU KIMOJA ZANZIBAR YETU KWANZA! UTAZAA KWA UCHUNGU! foolish is foolish he go to school!
 
pamoja na mapungufu yake huyu mama kama binadam mwengine, anaetaka kumuelewa bila ya kuvuta upande wake atamuelewa, tatizo ni mtoa mada na wengi wenu hamjafurahia kusikia yale yanayopendeza nafsini mwenu, swala la marupurupu ya muungano hata kama smz inamuona lkn kwake ni jambo la lazima kutokana na cheo chake, kuh muungano huo vilevile ni mtazamo wake, nawe toa wa kwako sio kumkejeli tu.
 
[h=1]
4.JPG
[/h]
ka11-300x225.jpg

Written by Foum // 16/07/2012 // Habari // 3 Comments

Monday, 16 July 2012 14:39

Mwandishi Wetu

WAKATI taifa likiwa katika mchakato wa kuelekea kupata Katiba Mpya, Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mama Fatma Karume ameibuka na kusema kama mumewe (marehemu Abeid Aman Karume) angekuwapo, baadhi ya mambo yanayofanywa na Serikali kuhusu Muungano sasa asingeyakubali.
Akizungumza katika mahojiano maalumu katika Kipindi cha Kutoka Zanzibar kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Channel Ten, mwishoni mwa wiki Mama Karume alisema kuwa, Muungano una kero nyingi ambazo sasa zinauingiza katika matatizo.
Alisema kero hizo hata mumewe marehemu Abeid Aman Karume angekuwa hai, asingezikubali.
Mama Karume, ambaye alijinasibu kama muumini mkubwa wa Muungano, alisema mumewe hakuiunganisha Zanzibar ili imezwe bali, alitaka nchi zote mbili za Muungano ziunganishwe na kunufaika kwa usawa.
“Mzee Karume alikubali Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa aliamini, kutatokea taifa moja lenye nguvu,” alifafanua Mama Karume na kuongeza:
“Alijifunza kutoka Marekani ambayo ni Muungano wa majimbo mengi na iliyokuwa Muungano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Sovieti (USSR). Alijua Tanzania nayo itakuwa na nguvu za kisiasa na kiuchumi.”
Mama Karume pia alifahamisha kuwa alikutana na viongozi wa Kundi la Uamsho lililoko Zanzibar na kuwasikiliza na kusema kuwa, anaunga mkono madai yao.
Hivi karibuni Kundi la Uamsho lilisababisha kuzuka kwa vurugu zilizoambatana na kuchoma makanisa na kuongoza mijadala mikali ya kupinga Muungano, kiasi cha kufanya baadhi ya viongozi wake kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
“Unajua vijana wa siku hizi wanajua mengi yanayoendelea kwenye Muungano. Kwa sasa na kwa kweli napenda kusema hawa watu wa Uamsho walinifuata nyumbani na wakanieleza kero zao kuhusiana na Muungano kwa kweli wana hoja,” alisema na kuongeza:
“Mimi naupenda sana Muungano lakini, kwa sasa nadhani una matatizo mengi, ambayo yanapaswa kujadiliwa kwa ukweli na uwazi. Nadhani hawa watu wa Uamsho wasikilizwe,” alisema Mama Karume, ambaye mumewe aliuawa Aprili 7, 1972 katika eneo la Kisiwandui Zanzibar.
Uteuzi wa watendaji Muungano
Pia Mama Karume alisema kuwa, uteuzi wa viongozi wa taasisi ambazo zinatakiwa kuwa za Muungano una walakini akisema; katika na uteuzi wa mabalozi, Zanzibar ina mabalozi watatu kati ya 33 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.
Pia alisema uongozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tangu ianzishwe mwaka 1966, hasa Gavana hajawahi teuliwa kutoka Zanzibar.
Alikiri kuwa kuna Naibu Gavana kutoka Zanzibar, lakini alidai chini yake amewekewa watu wawili kutoka Bara. Naibu Gavana, ambaye anatoka Zanzibar anaitwa Juma Reli (Anahusika na Utawala).
“Hivi ni haki kweli Zanzibar kuwa na mabalozi watatu wa Tanzania au kuwa na Naibu Gavana aliyewekewa wasaidizi wawili? Nadhani kuna tatizo hapa. Haya mambo lazima yaongelewe,” alisema mama Karume.
Alisema hakubaliani na jinsi suala zima la usimamizi wa fedha linavyosimamiwa na Serikali ya Muungano.
Alisisitiza hata mume wake, Karume angekuwa hai mambo hayo asingekubaliana nayo, kwani tangu mwanzo alikuwa anavutana na Muasisi mwenzake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
“Unajua, Mzee Karume alipokuwa hai alikuwa hataki masuala ya fedha na sarafu kuwa ya Muungano. Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kumtuma Waziri wake wa Fedha, Amir Jamal kuja Zanzibar na alikataa kutoa fedha za Zanzibar kwenda Benki Kuu,” alisema mama Karume.
Aliongeza; “Baada ya kitendo kile cha kumkatalia Jamal, nilimuuliza Mzee Karume inakuwaje anakataa kutoa fedha zile… Aliniambia kuwa kinachozalishwa Zanzibar kitabakia kuwa cha huku kwani haiwezekani kwa kisiwa kulisha nchi kubwa ya Tanganyika”.
Adai katelekezwa
Katika hatua nyingine, Mama Karume alidai kuwa pamoja na kuwa mke wa mwasisi wa Muungano lakini, bado hajanufaika nao.
Mama Karume alilalamika kuwa, ametelekezwa na Serikali ya Muungano licha ya ukweli kwamba, mumewe alifariki akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Alilalamika kwamba hajahudumiwa chochote na Serikali ya Muungano tangu mumewe afariki bali amekuwa akihudumiwa na Serikali ya Zanzibar na ndugu zake wa karibu.
“Hawa watu wa Serikali ya Muungano walinitelekeza maana hawajanisaidia chochote tangu Mzee Karume afariki.
“Kinachonishangaza ni wake za Makamu wa Rais wa Muungano waliofuata baada ya Mzee Karume wanaangaliwa na hata kupelekwa nje kwa matibabu,” alisema na kuongeza;
“Ninaendesha maisha yangu vizuri, lakini kwa kweli sijasaidiwa na lolote na Serikali ya Muungano pamoja na ukweli kuwa mume wangu ni mwanzilishi wa Muungano huu.”
Mtikisiko wa Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika siku za karibuni, umekuwa ukipita katika kipindi kigumu huku wanasiasa, wanaharakati na wananchi wakihoji muundo wake.
Wafuasi wa Kundi la Uamsho liliko Zanzibar walikamatwa hivi karibuni, wakihusishwa na uchomaji makanisa na uendeshaji wa mijadala ya kuelezea kero za Muungano.
Hata hivyo, malalamiko hayajaanza leo kwani yamekuwako miaka na miaka kiasi cha kufanya mwaka 1984, Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, Waziri Kiongozi Ramadhan Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Bashir Swanzey kulazimishwa kujiuzulu katika kile kilichoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa huko Zanzibar.
Tayari suala hilo la Muungano limeanza kuibua mjadala visiwani Zanzibar katika mchakato wa kupokea maoni unaofanywa na Tume ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba.
 
Sasa analalamikia muungano wa nini; si awashawishi BlW walete mswada wa kura ya maoni au waamue tu kujitangaza kuwa hawataki tena Muungano; amuambie mwanae Ali aachie ubalozi wa JMT na Wazanzibari wote watoke kwenye huduma ZOTE za Muungano. JWTZ halitawavamia kuwalamisha kubaki.. mbona ni rahisi sana kutoka kwenye Muungano?
 
abdulahsaf;425 Written by [URL="http://www.mzalendo.net/author/kimara" said:
Foum[/URL] // 16/07/2012 // Habari // 3 Comments

Monday, 16 July 2012 14:39

Mwandishi Wetu

Alikiri kuwa kuna Naibu Gavana kutoka Zanzibar, lakini alidai chini yake amewekewa watu wawili kutoka Bara. Naibu Gavana, ambaye anatoka Zanzibar anaitwa Juma Reli (Anahusika na Utawala).
"Hivi ni haki kweli Zanzibar kuwa na mabalozi watatu wa Tanzania au kuwa na Naibu Gavana aliyewekewa wasaidizi wawili? Nadhani kuna tatizo hapa. Haya mambo lazima yaongelewe," alisema mama Karume.
Alisema hakubaliani na jinsi suala zima la usimamizi wa fedha linavyosimamiwa na Serikali ya Muungano.
Alisisitiza hata mume wake, Karume angekuwa hai mambo hayo asingekubaliana nayo, kwani tangu mwanzo alikuwa anavutana na Muasisi mwenzake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
"Unajua, Mzee Karume alipokuwa hai alikuwa hataki masuala ya fedha na sarafu kuwa ya Muungano. Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kumtuma Waziri wake wa Fedha, Amir Jamal kuja Zanzibar na alikataa kutoa fedha za Zanzibar kwenda Benki Kuu," alisema mama Karume.
Aliongeza; "Baada ya kitendo kile cha kumkatalia Jamal, nilimuuliza Mzee Karume inakuwaje anakataa kutoa fedha zile… Aliniambia kuwa kinachozalishwa Zanzibar kitabakia kuwa cha huku kwani haiwezekani kwa kisiwa kulisha nchi kubwa ya Tanganyika".
Adai katelekezwa
Katika hatua nyingine, Mama Karume alidai kuwa pamoja na kuwa mke wa mwasisi wa Muungano lakini, bado hajanufaika nao.
Mama Karume alilalamika kuwa, ametelekezwa na Serikali ya Muungano licha ya ukweli kwamba, mumewe alifariki akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Alilalamika kwamba hajahudumiwa chochote na Serikali ya Muungano tangu mumewe afariki bali amekuwa akihudumiwa na Serikali ya Zanzibar na ndugu zake wa karibu.
"Hawa watu wa Serikali ya Muungano walinitelekeza maana hawajanisaidia chochote tangu Mzee Karume afariki.
"Kinachonishangaza ni wake za Makamu wa Rais wa Muungano waliofuata baada ya Mzee Karume wanaangaliwa na hata kupelekwa nje kwa matibabu," alisema na kuongeza;.

Hizi post nyingine mbona zinatia kichefuchefu! hapo kwa red ndo nini sasa? kwahiyo mnataka mtu apewe nafasi eti kwavile tu ni mzanzibari, hivi nani aliwaambia tunapeana madaraka kwa zamu?

Halafu kuhudumiwa na serikali ya zanzibar hakutoshi hadi na ya muungano nayo imuhudumie, baseless complains!!!
 
Muungano ukifa mama, sidhani kama utapata tena nafasi ya kuongea kama sasa hivi, bahati yako umesha zeeka, kwa kuwa hao waliokutuma wanakutumia kama toilet paper au kondom, shughuli ikishamalizika wewe unakuwa kinyaa hakuna anayetaka kukutizama tena. Mimi siunge wala sipingi muungano, lakini siku ukivunjika wewe mama na kizazi chako ni lazima msulubishwe tu, kwani mume wako kuna jambo alilolifanya likaudhi watu hadi wakaamua kumuua. bado naamini wapo wenye kisasi moyoni. Mungu akituongezea miaka 20 haya niliyosema utayaona kwa macho yako. tuombe MUNGU muungano usivunjike.
 
Mama Karume hajachemka. KATOKOTA! Nilisikiliza yale mahojiano yake mwanzo mwisho..nadhani kama wasemavyo mtu ukizeeka unarudia akili za utotoni!

Anaamini Amani alipata uraisi kwa jitihada na uwezo wake, si shukrani kwa familia yake!

Anaamini anayotendewa na Serikali ya Zanzibar, serikali ya Muungano haipaswi kujivunia ila inatakiwa nayo iangalie kumlipa fadhira independently!

Ana-question Deputy Gavana wa BOT kuwa na wasaidizi wawili kua ni kama kuonesha kwamba hana uwezo, anasahau kwamba DG huyo anaendesha vitengo vikubwa na nyeti vya utawala (Miradi yote hupitia hapa) , Komputa na Finance! Na hiyo ni structure uya benki regardless DG ni nani!
 
Kaingia kwenye kumi na nane za Uamsho jamaa wakamuweka kati wakatwanga mbele na nyuma kujashtuka anaimba wimbo wao.Hata hivyo sisi tunaangalia katiba yetu ya Tanganyika.
Nilimsikia live akihojiwa kwenye kile kipindi kilichorushwa na chanel ten, Ni kama nilikua naona harufu ya kiuamshoamsho katika mazungumzo yake! Kwa nafasi yake madai aliyoyatoa angeweza kumwita hata Kikwete nyumbani kwake, wacha yeye mwenyewe kwenda na kukutana na Kikwete kuzungumzia madai yake. Angeweza hata kumtuma Amani aende kuonana na Kikwete kulizungumzia hili kama kweli jambo hilo lilimkera hivyo! Kulisemea pale alikuwa antufumbua macho, kuwa UAMSHO INAFADHILIWA NA SERIKALI
 
Huyu mama is a typical Zanzibari. Kimsingi ana-represent hao jamaa walivyo. Kwa nafasi yake alitakiwa atulie apumzike na sio kuanza kujiingiza katika masuala ya kisiasa. Anachofanya ni siasa. Kama alivyo-comment mdau mmoja hapo juu, huyu mama ashukuru uhuru wa kutoa mawazo na kuropoka jinsi anavyofanya na hata kuwa 'mwanachama wa maisha' wa Yanga ni kwa sababu ya Muungano.

Hao Uamsho wakishamtumia wapendavyo mwisho atalia na kusaga meno. Aulizie Somalia mwanamke wa mwisho kuongea hadharani alikuwa nani na kilimpata nini. Ni ushauri wa bure tu.
 
Yes, Makamu wa Rais wa Tanzania, mbona Jumbe anapewa?

Kumbeeeeee! Ndio maana mnapendaga sana muungano. MARUPURUPU - ngojeni turejeshe Tanganyika muone nani atawapa marupurupu. Wavivu wakubwa, mmeshaanza kufungiwa LUKU na shirika la umeme ZNZ lisilozalisha hata wati moja?
 
Luku zimeanza Zanzibar kabla ya Tanganyika. halafu mimi ni Mtanganyika wewe Mtanzania acha kunipeleka visiwani.
 
Anasema serikali ya muungano haina muda wa kumliwaza???? Anataka twanga pepeta wawe wanalala barazani kwake au?
 
Wengi tuu hatuamini kama hayo alosema ni yake toka moyoni. Swala ni je alikuwa wapi kuzungumza hivo wakati sasa Muungano unatimiza miaka 48?????????
Mama Karume anaheshimika sana si tu kwa umri wako, bali hata kwa kuwa mke wa Mzee wetu, Mzee Abeid Amani Karume,mmoja wa waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Nimesoma leo magazeti kadhaa juu ya malalamiko yake kwa Serikali ya Muungano na pengine nitanukuu toka magazeti mfano la Tnzania Daima lal leo Julai 16 2012, linasema:
Mjane wa Rais wa Kwanza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Abeid Aman Karume, Fatma Karume, amesema haoni faida za muungano kwa kuwa serikali hiyo imemtelekeza.
Alisema hadi mauti yanamkuta mumewe alikuwa mkamu wa Rais wa Serikali ya Muungano lakinihakuna kiongozi wa serikali hiyoaliyemkumbuka kwa lolote jambolimalomfanya kuona Muungano huo hauna faida kwake.
........

Fatuma alieongeza kuwa serikali ya Muungano inamkumbuka kidogo sana lakini si kumliwaza na kwamba wakati wa Karume Muungano ulikuwa afadkhali kidogo.
..........

Fatuma ambaye ni mamam mzazi wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliitaka serikali ya Muungano kuwa na mgawanyao sawa wa fedha na madaraka.

Gazeti lingine , Mwananchi leo vile vile linaenda mbali zaidi na kusema🙁page 4)

Mama Karume pia alifahamisha kuwa alikutana na viongozi wa Kundi la Uamsholililoko Zanzibar na kuwasikiliza na kusema anaunga mkono madai yao.

Maoni yangu:
Imeanzan kthibitika kuwa masualaya uamsho na fujo za Zanzibar zilikuwa na baraka zote za SMZ na pengine baadhi ya viongozi wake.
Sio rahisi Mama Karume akutane na Uamsho ilhali mwanawe Abeid Karume asifahau hilo, na hivyo basi viongozi wa SMZ.
Tanganyika tusijejikuta tuna twanga maji kwenye kini katika hili.

Juu ya Muungano kulalalmikiwa kutomtunza Mama Karume hili linastjaabisha , hasa ukitilia maanani kuwa SMZ ipo na haijafa, na mwanawe alikuwa RAISI WA ZANZIBAR.

Maneno ya huyu mamam nayachukulia kuwa ya kupandikizwa mdomoni na uamsho na si vinginevyo.
Huku Dar es salaam tunajua kuwa wanawe wana biashara kubwa tu,mfano AMANI HOUSE(Mbele ya Serena/Movenpick hotel), huyo mama si wa kulalalama magazetini juu ya kutotunzwa wakti wenye jukumu hilo lwapo, wanabiashara kubwa na hawajafa.

Hulka ya Mama Karume vile vile ina question mark, hivi karibuni kulikuwa na habari ya kurejeshwa kwa kiwanja cha serikali alichokipata kwa ulaghai na hatimaye kuwauzia wafanyabiashara wa ki-asia huko Zanzibar.
Huu ni utapeli.

Kwa muelekeo wa Muungano hatuna haja kwenda mbali zaidi kuchokonoa historia yake na Wazanzibari wanaoheshimika kama kina Diria na wengine, lakini kwa ujumla mchango wa Mama karume sijaupenda.
 
Huyu mama ni YANGA tupu......muungano ungivunjika watani mnaenda nae Zanzibar!

Huyu mama ni anachonga sana kama Mwenyekiti wa Simba na Makamu wake na hatofautiani na shabiki wa Simba Prof.Maji Marefu
 
Wengi tuu hatuamini kama hayo alosema ni yake toka moyoni. Swala ni je alikuwa wapi kuzungumza hivo wakati sasa Muungano unatimiza miaka 48?????????
Pamoja na ukweli kuwa MTOTO WAKE alikuwa Rais wa Zanzibar, Mama Karume hapati au hspati ushauri mzuri wa kila siku, namna ya kuishi kama kiongoxi.
 
Muungano ukifa mama, sidhani kama utapata tena nafasi ya kuongea kama sasa hivi, bahati yako umesha zeeka, kwa kuwa hao waliokutuma wanakutumia kama toilet paper au kondom, shughuli ikishamalizika wewe unakuwa kinyaa hakuna anayetaka kukutizama tena. Mimi siunge wala sipingi muungano, lakini siku ukivunjika wewe mama na kizazi chako ni lazima msulubishwe tu, kwani mume wako kuna jambo alilolifanya likaudhi watu hadi wakaamua kumuua. bado naamini wapo wenye kisasi moyoni. Mungu akituongezea miaka 20 haya niliyosema utayaona kwa macho yako. tuombe MUNGU muungano usivunjike.
Namsikikitia sana Mama Karume kwa maana anachezea nafasi adimu na muhimu sana katika histria ya nchi yetu, Tanzania.Nafasi aliyonayo, hata akiandika kiyabu kidogo tu ya yale yaliyowasibu wazanzibari siku ya mapinduzi, ni historia tosha kwa vizazi vijavyo
 
bot_tabimg.gif

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Monday, 16 July 2012 14:39[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

​
0000001mamakarume.jpg

Mwandishi Wetu

WAKATI taifa likiwa katika mchakato wa kuelekea kupata Katiba Mpya, Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mama Fatma Karume ameibuka na kusema kama mumewe (marehemu Abeid Aman Karume) angekuwapo, baadhi ya mambo yanayofanywa na Serikali kuhusu Muungano sasa asingeyakubali.

Akizungumza katika mahojiano maalumu katika Kipindi cha Kutoka Zanzibar kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Channel Ten, mwishoni mwa wiki Mama Karume alisema kuwa, Muungano una kero nyingi ambazo sasa zinauingiza katika matatizo.

Alisema kero hizo hata mumewe marehemu Abeid Aman Karume angekuwa hai, asingezikubali.

Mama Karume, ambaye alijinasibu kama muumini mkubwa wa Muungano, alisema mumewe hakuiunganisha Zanzibar ili imezwe bali, alitaka nchi zote mbili za Muungano ziunganishwe na kunufaika kwa usawa.

"Mzee Karume alikubali Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa aliamini, kutatokea taifa moja lenye nguvu," alifafanua Mama Karume na kuongeza:

"Alijifunza kutoka Marekani ambayo ni Muungano wa majimbo mengi na iliyokuwa Muungano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Sovieti (USSR). Alijua Tanzania nayo itakuwa na nguvu za kisiasa na kiuchumi."

Mama Karume pia alifahamisha kuwa alikutana na viongozi wa Kundi la Uamsho lililoko Zanzibar na kuwasikiliza na kusema kuwa, anaunga mkono madai yao.

Hivi karibuni Kundi la Uamsho lilisababisha kuzuka kwa vurugu zilizoambatana na kuchoma makanisa na kuongoza mijadala mikali ya kupinga Muungano, kiasi cha kufanya baadhi ya viongozi wake kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

"Unajua vijana wa siku hizi wanajua mengi yanayoendelea kwenye Muungano. Kwa sasa na kwa kweli napenda kusema hawa watu wa Uamsho walinifuata nyumbani na wakanieleza kero zao kuhusiana na Muungano kwa kweli wana hoja," alisema na kuongeza:

"Mimi naupenda sana Muungano lakini, kwa sasa nadhani una matatizo mengi, ambayo yanapaswa kujadiliwa kwa ukweli na uwazi. Nadhani hawa watu wa Uamsho wasikilizwe," alisema Mama Karume, ambaye mumewe aliuawa Aprili 7, 1972 katika eneo la Kisiwandui Zanzibar.

Uteuzi wa watendaji Muungano

Pia Mama Karume alisema kuwa, uteuzi wa viongozi wa taasisi ambazo zinatakiwa kuwa za Muungano una walakini akisema; katika na uteuzi wa mabalozi, Zanzibar ina mabalozi watatu kati ya 33 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.

Pia alisema uongozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tangu ianzishwe mwaka 1966, hasa Gavana hajawahi teuliwa kutoka Zanzibar.

Alikiri kuwa kuna Naibu Gavana kutoka Zanzibar, lakini alidai chini yake amewekewa watu wawili kutoka Bara. Naibu Gavana, ambaye anatoka Zanzibar anaitwa Juma Reli (Anahusika na Utawala).

"Hivi ni haki kweli Zanzibar kuwa na mabalozi watatu wa Tanzania au kuwa na Naibu Gavana aliyewekewa wasaidizi wawili? Nadhani kuna tatizo hapa. Haya mambo lazima yaongelewe," alisema mama Karume.

Alisema hakubaliani na jinsi suala zima la usimamizi wa fedha linavyosimamiwa na Serikali ya Muungano.

Alisisitiza hata mume wake, Karume angekuwa hai mambo hayo asingekubaliana nayo, kwani tangu mwanzo alikuwa anavutana na Muasisi mwenzake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

"Unajua, Mzee Karume alipokuwa hai alikuwa hataki masuala ya fedha na sarafu kuwa ya Muungano. Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kumtuma Waziri wake wa Fedha, Amir Jamal kuja Zanzibar na alikataa kutoa fedha za Zanzibar kwenda Benki Kuu," alisema mama Karume.

Aliongeza; "Baada ya kitendo kile cha kumkatalia Jamal, nilimuuliza Mzee Karume inakuwaje anakataa kutoa fedha zile... Aliniambia kuwa kinachozalishwa Zanzibar kitabakia kuwa cha huku kwani haiwezekani kwa kisiwa kulisha nchi kubwa ya Tanganyika".

Adai katelekezwa

Katika hatua nyingine, Mama Karume alidai kuwa pamoja na kuwa mke wa mwasisi wa Muungano lakini, bado hajanufaika nao.

Mama Karume alilalamika kuwa, ametelekezwa na Serikali ya Muungano licha ya ukweli kwamba, mumewe alifariki akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Alilalamika kwamba hajahudumiwa chochote na Serikali ya Muungano tangu mumewe afariki bali amekuwa akihudumiwa na Serikali ya Zanzibar na ndugu zake wa karibu.

"Hawa watu wa Serikali ya Muungano walinitelekeza maana hawajanisaidia chochote tangu Mzee Karume afariki.

"Kinachonishangaza ni wake za Makamu wa Rais wa Muungano waliofuata baada ya Mzee Karume wanaangaliwa na hata kupelekwa nje kwa matibabu," alisema na kuongeza;

"Ninaendesha maisha yangu vizuri, lakini kwa kweli sijasaidiwa na lolote na Serikali ya Muungano pamoja na ukweli kuwa mume wangu ni mwanzilishi wa Muungano huu."

Mtikisiko wa Muungano

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika siku za karibuni, umekuwa ukipita katika kipindi kigumu huku wanasiasa, wanaharakati na wananchi wakihoji muundo wake.

Wafuasi wa Kundi la Uamsho liliko Zanzibar walikamatwa hivi karibuni, wakihusishwa na uchomaji makanisa na uendeshaji wa mijadala ya kuelezea kero za Muungano.

Hata hivyo, malalamiko hayajaanza leo kwani yamekuwako miaka na miaka kiasi cha kufanya mwaka 1984, Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, Waziri Kiongozi Ramadhan Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Bashir Swanzey kulazimishwa kujiuzulu katika kile kilichoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa huko Zanzibar.

Tayari suala hilo la Muungano limeanza kuibua mjadala visiwani Zanzibar katika mchakato wa kupokea maoni unaofanywa na Tume ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Huyu mama tamaa itamtoa roho. mapesa yote anayopewa kila siku bado anasema mbovu?.
 
Back
Top Bottom