Mama aibiwa mafao yake yote NMB Kahama

Mama aibiwa mafao yake yote NMB Kahama

Siku akisikia wale top 3 wa nchi wapo kahama abebe bango kwenda nalo mkutanoni Mama alisema bango moja tu viongozi waliopo eneo husika watakuwa hawana kazi kwa kushindwa kutatua kero za wananchi hasa kwa mambo ambayo siyo ya kitaifa
Mama la mama ...bango moja tu mmekwisha wote
 
Kiukweli kwa tulipofikia kwa sasa simu yako ni kama benki yako.Ni hatari sana kumpa tu mtu simu yako hata akisema anataka kumpigia mtu.
Na bahati mbaya wa Tz wengi kwenye mambo ya internet na simu bado tupo kizembe sana.Watu watapigwa sana bahat mbaya.Ukweli mchungu
 
Jee kama staff wa Bank wamefanya changing of mobile number kwenye akaunti ya mama wa kaweka wanayoitaka wao kwa ajili ya kupiga!?

Mteja hapata alerts na huku pesa zinatoka kadri ya limit ya siku inavyoruhusu. Mpk hela yote inaisha.

Na mara nyingi hela inapoisha ndio mteja anagundua au ndio anapewa taarifa

Staff wa bank hapewi hizo access kwa urahisi kama unavyofikiria... makosa kayafanya mama mwenyewe ndio maana mtoa uzi haelezi kwa undani wala hajibu hoja za watu tuliowahi fanya kazi bank.. sababu tunajua hawezi kutudanganya...
 
Asilimia 99.999 ya wizi unaofanyika benki kupitia ATM au mobile banking, mhusika mkuu ni mteja mwenyewe. Inasikitisha ila ndiyo hivyo. Wastaafu wengi wepesi sana kuhadaika, kuanzia kwa watu watu wanaomzunguka (ndugu) mpaka kwa matapeli wenyewe. Huyo mama akienda Takukuru huenda akasaidiwa kupata pesa zake. Ila nini imani asilimia 100 benki wako innocent.
Huu ndio ukweli mchungu ambao wengi hawakubali,Ili ujiunge Nmb mobile ni lazima vitu viwili vihusike,kadi yako ya benki na simu yako,na hapo ni lazima ufike kwenye ATM mashine ili uigize kadi na ujiunge na kuweka namba yako ya siri,sasa kama Mama aliteleza akamwamini mtu baki kumpa kadi na namba zake za siri ili amtolee hela basi hapo ndio alipojichanganya,maana mtu atakutolea hela na atakuletea ila atajiunga na huduma ya simu kwa namba yake.

Kwa Pesa hizo mil 24 itamchukua mwizi siku 24 tu kuhamisha kwa njia za simu(kumbuka limit ya kuhamisha kwa simu ni 1,000,000 kwa siku) huku akiwa amekaa kweye kochi na kwenda kuzitoa kwa wakala.

Hapo mwenye akaunti hawezi kupata taarifa yoyote kwamba hela imetoka labda kama awe ameunganishwa kwenye SMS banking(ni huduma tofauti).

Hapo benki sidhani kama ina lawama labda kama kuna mengine tusiyoyajua ambayo yanahusishwa watumishi wa ndani ya benki.
 
Jee kama staff wa Bank wamefanya changing of mobile number kwenye akaunti ya mama wa kaweka wanayoitaka wao kwa ajili ya kupiga!?

Mteja hapata alerts na huku pesa zinatoka kadri ya limit ya siku inavyoruhusu. Mpk hela yote inaisha.

Na mara nyingi hela inapoisha ndio mteja anagundua au ndio anapewa taarifa
Benki mambo hayapo kiholela hivyo..

Probably huyu maana alijiunga na simbanking bila ya yeye kujua kinachofanyika na namba ikawekwa ambayo siyo yake.
 
Huu ndio ukweli mchungu ambao wengi hawakubali,Ili ujiunge Nmb mobile ni lazima vitu viwili vihusike,kadi yako ya benki na simu yako,na hapo ni lazima ufike kwenye ATM mashine ili uigize kadi na ujiunge na kuweka namba yako ya siri,sasa kama Mama aliteleza akamwamini mtu baki kumpa kadi na namba zake za siri ili amtolee hela basi hapo ndio alipojichanganya,maana mtu atakutolea hela na atakuletea ila atajiunga na huduma ya simu kwa namba yake.

Kwa Pesa hizo mil 24 itamchukua mwizi siku 24 tu kuhamisha kwa njia za simu(kumbuka limit ya kuhamisha kwa simu ni 1,000,000 kwa siku) huku akiwa amekaa kweye kochi na kwenda kuzitoa kwa wakala.

Hapo mwenye akaunti hawezi kupata taarifa yoyote kwamba hela imetoka labda kama awe ameunganishwa kwenye SMS banking(ni huduma tofauti).

Hapo benki sidhani kama ina lawama labda kama kuna mengine tusiyoyajua ambayo yanahusishwa watumishi wa ndani ya benki.
Yes..hii ndo best probable source ya huyu mama kupigwa tunayoweza kuiwaza.
 
Yes..hii ndo best propable source ya huyu mama kupigwa tunayoweza kuiwaza.
Mimi sijui kwanini watu wanakua so careless na hela zao. Mimi huwa nina account mbili..moja inakua haijaungwa na sim banking wala internet banking na wala haina ATM card..na huko ndio nawekaga akiba yangu. Halafu account ya pili ndio inakua na sim banking na ATM card..hii ndio natumiaga kwa matumizi ya day to day..so mshahara ukiingia huwa hela za akiba na transfer kwenye ile account ya kwanza halafu hii nyingine zinakua zimebaki hela ndogo tu za matumizi. Na uzuri inanipa discpline maana hela za akiba siwezi kuaccess kirahisi..lazma niende bank. Sasa mama huyu pensheni yote kaweka kwenye transactional account? Angeweza hata kutupia kwenye fixed deposit ikamzalishia riba kidogo
 
Yes..hii ndo best propable source ya huyu mama kupigwa tunayoweza kuiwaza.
Naamini hii ishu ingekuwa ni benki ndio imehusika wala usingeisikia humu,angerudishiwa hela mara moja baada ya kuripoti maana wanajua jinsi gani itaharibu image yao wateja wakijua kwamba hela zao haziko salama
 
Nmb mobile Ina namba ya Siri na Kila kinachofanyika mhusika hupata taarifa . Huenda mama alimuachia mtu simu na namba ya Siri akampa . Kila wakati Benki na polisi wanajitahidi kuelimisha kuhusu namba ya Siri . Kuna uzembe uliofanyika ama wa mama au Benki .
...I we ni Uzembe ama la sio issue. Issue hapa kwamba Mama Mstaafu amribiw Milioni 24 take kutoks akaunti take NMB.

kuna uwezekano mama amechanyikiwa hajui hata pa kuanzia.
Mliopo huko mpeni msasda mama. Safari ya kwanza iwe kwa meneja wa Tawi na kumueleza kilichotokea na aende hstua kwa hatua...kuna mahali lazima stapata Msaada wa Uhakika wa kupata hela yake ...!
 
Mama kapigwa na watu wake. Narudia mama kapigwa na watu wake.
Siku hizi mtu anahamisha 2.5M kwa airtelmoney.

Hii lazima mtu atumie laini yake akijua TIN namba yake.
 
Kwanini haya madai yasipelekwe mahala sahihi kama kweli kadhulumiwa akapewe haki yake, aanzie kwa mkuu wa wilaya ikibidi, nadhani huyo mama alikuwa mwalimu kama alikopa hao jamaa ndio wakachukua pesa yake juu kwa juu hiyo ndio tabia yao.
Akishindwa hapo aende ofisi za Takukuru watamsaidia.
Sahihi kabisa Mkuu wa Wilaya ya Kahama ni Mr Macha mbona sasa hivi ataamka nalo na km ni mtoto aliyekimbilia Dodoma au ni mwizi atarudishwa na pesa wataitapika.
huyo Mama asaidiwe na tuone mrejesho kabla ya TAKUKURU hawajaingilia kuzirejesha zote
 
Staff wa bank hapewi hizo access kwa urahisi kama unavyofikiria... makosa kayafanya mama mwenyewe ndio maana mtoa uzi haelezi kwa undani wala hajibu hoja za watu tuliowahi fanya kazi bank.. sababu tunajua hawezi kutudanganya...
Either mama ka share Mobile banking password na jamaa zake wa karibu na ndio wamemliza. Or bank staff wamefanya yao. Najua kama staff wa Bank hawapewi excess kiarahisi za kulink lkn pindi wakipewa wapo wanaozitumia vibaya.

Wakati mwengine inawezekana staff wa Bank wamemlink mama kwa namba ya simu ya mteja mwengine kwa bahati mbaya, akafanikisha changing of one time password na kufanikiwa kutoa.

Kazi za bank nazo ni risk, bahati mbaya zinatokea lkn pia na staff wa Bank kwa makusudi hufanya yao
 
Benki mambo hayapo kiholela hivyo..

Probably huyu maana alijiunga na simbanking bila ya yeye kujua kinachofanyika na namba ikawekwa ambayo siyo yake.
Ulichosema ni possible.

Lkn na staff wa Bank pia wanaweza wakawa wanahusika either kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Kuna vijana dot com huko.
 
Mwanamke mmoja mkazi wa Kahama mjini (Mstaafu)kwa jina Maghdalena Petro Kayilà,aliibiwa Fedha zake zote pale NMB Kahama kiasi cha million 24

Wizi iliotumika ni Fedha kuhamishwa kwa njia NMB Mobile kupitia laini ya Tigo.

Fedha zilipoisha Benki ndio akapewa taarifa na Uongozi wa Bank ya NMB Kahama Branch.

Kwa kifupi Uongozi wa NMB Kahama, Polisi Wilaya ya Kahama haijampa ushirikiano Mama yule hivyo kusababisha Mama yule kuishi maisha ya kifukara hadi leo.

Kuna baadhi ya Watuhumiwa walikamatwa na kuachiwa bila Mama yule kuwaona.

Mmoja ni mkazi wa Dodoma,Mwingine ni Mwalimu Segese na mwingine ni Mwalimu wilaya ya Ushetu.

Kwasababu Mama huyu hana Fedha za kufuatilia kesi hii, Serikali imetulia na hakuna kinachoendelea hadi leo.

Kumekuwa na vitendo vya Wizi kama huu NMB Kahama wakiibiwa wastaafu.

Niishauri Serikali kulifatilia hili maana wastaafu wanateseka sana.

Manager Branch bwana Chacha baada ya tuhuma, alihamishwa Kituo cha kazi na kupelekwa Mpanda.

Serikali fatilieni hili.
Toa namba ya simu ya mama hapa tumsalimie au hata kapicha kake ili tumwombee
 
Back
Top Bottom