Sijajua
NMB Tanzania wanakwama wapi ,mara nyingi Bank wana mifumo ambayo ina detect abnormal transactions ,sasa ushawahi kuona wapi mtu ana draw 24 mils zote kwa Sim Banking? Yaani hapo wazi kuna fraud....Nawashauri NMB waboreshe mifumo yao,watu wa kitengo cha risk management wawe na system ambayo inawapa sms alert kwa account yeyote ambayo itakuwa inafanya abnormal transactions na wawe na remote access the system na kuweza kublock account instantly mpaka mwenyewe avisit bank kuconfirm kama hizo transaction ni sahihi.
Waweke limit mtu akitransfer zaidi ya mili 3 kwenye sim bank itoe alert na waiblock kisha wampigie customer kuhakiki kama hiyo miamala anaitambua ,hiyo ndio huduma kwa wateja sio wanakaa mpaka account inakuwa zero ndio wanamtaarifu mteja.