Mama aibiwa mafao yake yote NMB Kahama

Mama aibiwa mafao yake yote NMB Kahama

Utakuta Mama alikuwa na madeni na aliweka mafao collateral
 
Laini ya tigo pesa haiwezi kuiba milioni 20 mara moja, kiasi kina mwisho.. pili mtu hawezi hamisha pesa kwa sim banking bila namba ya siri kuijua . Mama atakuwa amefanya uzembe sehemu
Utakuta hao wastaafu wanawatumia watoto wao au wajukuu zao kwa kuwapatia neno la siri.

Huo wizi unatumika sana
 
Mwanamke mmoja mkazi wa Kahama mjini (Mstaafu)kwa jina Maghdalena Petro Kayilà,aliibiwa Fedha zake zote pale NMB Kahama kiasi cha million 24

Wizi iliotumika ni Fedha kuhamishwa kwa njia NMB Mobile kupitia laini ya Tigo.

Fedha zilipoisha Benki ndio akapewa taarifa na Uongozi wa Bank ya NMB Kahama Branch.

Kwa kifupi Uongozi wa NMB Kahama, Polisi Wilaya ya Kahama haijampa ushirikiano Mama yule hivyo kusababisha Mama yule kuishi maisha ya kifukara hadi leo.

Kuna baadhi ya Watuhumiwa walikamatwa na kuachiwa bila Mama yule kuwaona.

Mmoja ni mkazi wa Dodoma,Mwingine ni Mwalimu Segese na mwingine ni Mwalimu wilaya ya Ushetu.

Kwasababu Mama huyu hana Fedha za kufuatilia kesi hii, Serikali imetulia na hakuna kinachoendelea hadi leo.

Kumekuwa na vitendo vya Wizi kama huu NMB Kahama wakiibiwa wastaafu.

Niishauri Serikali kulifatilia hili maana wastaafu wanateseka sana.

Manager Branch bwana Chacha baada ya tuhuma, alihamishwa Kituo cha kazi na kupelekwa Mpanda.

Serikali fatilieni hili.
Pole zake.Ila kama kaibiwa zote,mbona ni kidogo sana?Au alisha kopa kopa?
 
Kinachoonekana hapa ni kuwa huenda mama alienda bank kuulizia kama pesa zake za mafao zimeingia. Wahuni wanaofanya kazi benki akili zikawacheza haraka namna ya kupiga pesa.

Wakamshawishi mama ajiunge Sim banking ili aweze kupokea ujumbe punde tu pesa zitakapoingia kuliko kujihangaisha kuja kuulizia mara kwa mara.

Mama akaona hapa ndiyo penyewe. Akachukuliwa karatasi akasainishwa. Lakini huenda namba iliyowekwa siyo yake. Ni hiyo iliyotumika kuchotea mpunga kwenye account ya mama..

Kikichofuata ni kilio kwa mama na shangwe kwa wahuni.

Tuwe macho.
 
Laini ya tigo pesa haiwezi kuiba milioni 20 mara moja, kiasi kina mwisho.. pili mtu hawezi hamisha pesa kwa sim banking bila namba ya siri kuijua . Mama atakuwa amefanya uzembe sehemu
Asilimia 99.999 ya wizi unaofanyika benki kupitia ATM au mobile banking, mhusika mkuu ni mteja mwenyewe. Inasikitisha ila ndiyo hivyo. Wastaafu wengi wepesi sana kuhadaika, kuanzia kwa watu watu wanaomzunguka (ndugu) mpaka kwa matapeli wenyewe. Huyo mama akienda Takukuru huenda akasaidiwa kupata pesa zake. Ila nini imani asilimia 100 benki wako innocent.
 
Back
Top Bottom