A
Anonymous
Guest
Watumishi wa Umma, Idara ya Elimu hasa Sekondari Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi hawalipwi fedha zao za likizo kwa wakati, wakati mwingine inaweza kuchukua hata miaka miwili ndio wanakuja kupata malipo.
Hata wakiomba kiwango fulani cha nauli, wahusika wanaolipa na malipo wanachofanya ni kukadiria tu na sio uhalisia wa ulichoomba, mbaya zaidi na kinachotia mashaka ni kiwango kinachoombwa kwenye mfumo wao (ESS, Elimu Sekondari), wanalazimisha waombe kwa kuandika kwa mkono wakati kila kitu siku hizi kinafanyika kidigitali.
Mwaka 2025 mwezi December walimu waliomba likizo zao za malipo kwenye mfumo wa ESS lakini zilipofika idarani zilikuwa "rolled back" (walirejesha nyuma) na wakasema ni sababu za kimtandao, hivyo walimu waombe likizo zao kwa kuandika kwa mkono.
Hili linatia mashaka na kuleta usumbufu pia na linashusha morali kwa walimu.