mali zipo ,uwongo pia upo.kama'kweli yupo mtu ambaye anasema ameona sehemu kuna ,mali za mjerumani iwe sanduku ma kingine chochote lakini hakuingiliki ama kuna simba,fimbo,joka au mauza uza yoyote;sisi tupo tunatoa kiulainiiil,ila wengi waongo .kama mtu ana uhakika call 0717 292726,tukapige hela,onyo muongo akae mbali,kwa walio ona tu suala la kusikia kaa mbali.
Ipo dhana ya kwamba wajerumani wakati wapokuwa wakikurupushwa na waingereza Tanganyika baadhi ya mali zao walishindwa kuondoka nazo,hivyo inasadikika mali nyingi walidhihifadhi chini ya ardhi kwa utaratibu maalumu ambao ktk mazingira ya kawaida si rahisi kuzitoa au kuzihamisha.
Inasadikika mali hizo zitakaa hapo zilipo mpk wao wenyewe watakapoamua kuzifuata,pia inasadikika walitumia "runic rituals"ktk kudhihifadha utaratibu unaoendana na utoaji kafara binadamu.
Yapo maeneo mbalimbali ambako inasadikika masanduku haya yalihifadhiwa, baadhi ya maeneo hayo ni Tanga (usambara), Morogoro, Singida, Lindi, Kilimanjaro na nk.
Yeyote mwenye taarifa zaidi aweza kutujuza zaidi juu ya suala hili, kwani maeneo haya yatakapo julikana vema huenda yakawa chanzo kizuri cha utalii kutokana na historia yake kusisimua.
Nawasilisha.
Hapo umesema kweli hizi hadithi ni uzushi hakuna aliyefanikiwa hata mmoja. Ni utapeli tu na kiini macho kuna mzee jirani yangu mstaafu wa jeshi alimaliza kiinua mgongo chote kwenye hizo issue hakuna alichoambulia.Bahati alichimba kisima cha maji ndio anauza ndoo mia walau anajikimu kimaishaMbona hakuna anayeleta ushahidi pasi na mashaka kuwa wamefanikiwa kupata hizo
Mali kwa mfano mtu aseme
Sehemu mfano Iringa wamepa sanduku lenye mali pia na aina mfano dhahabu
almasi n.k
Nahisi kuna kamtandao kamefufuka kanataka kumtapeli mtu..zege gani duniani isiyoripuka kama sio uzushiKuna jamaa yangu Rukwa pembeni na ziwa tanganyika alichimba akafika kwenye zege, hiyo cementi sijui ni aina gani haitoboki kwa kwa sururu wala nyundo, alinunua Conc. HCL lita 100 , zina uwezo wa kuyeyusha jiwe lolote hata chuma, walipomwaga palichemka sana, kesho yake walikuta majivu juu ila zege liko palepale, walijaribu kutumia baruti, hamna kitu. Ameishia kulitafutia hati miliki na kuendelea na shuguli zake.
Hivyo kama unadhani umefika mwisho basi jua ngoma bado mbichi
Hakuna kitu kama hicho hapa TZ. Ni story tu za kutaka kupata utajiri wa haraharaka!
Biashara hii iliwafanya wazazi wangu nusra wanifunge kamba kunipeleka Milembe wakidhania nimekuwa mwehu 1999😡 Sitaki hata kuisikia,nilikuwa nasafiri asubuhi hadi kwa usiku natembelea vijiji vitatu lakini kila mji ukiwauliza wanakujibu uende kijiji jirani kwa mzee fulani kama bado yuko hai unaweza pata maana yeye alishiriki vita ya Mjerumani! ukifika hapo unaambiwa tena nenda kijiji jirani kuna babu mmoja alizikwa nazo yaani hadi nywele zangu zikawa nyekundu kwa vumbi na jua hadi nikaja kujistukia 2003!!