Wengi walikuwa wanatumia biblical signs kama wahispania na wagiriki
Wajerumani wametumia ishara za compass
Inataka akili kubwa kuelewa Mali zilipohifadhiwa
Zipo sehemu nyingi duniani na moja iliyonishangaza sana ni wale wapambanaji walioenda kutafuta mali huko kwenye kisiwa cha majoka Ilha da Queimada Grande huko Brazil
Kisiwa ambacho nyoka wamejaa kiasi ambacho kila hatua unayopiga unaona nyoka aidha chini au juu ya miti
Lakini bado jamaa wakaendelea kutafuta na kufuata ishara zote
Hawakufanikiwa ingawa waliamua kulala hapohapo kisiwani kwenye majoka
Usiku kuna nyoka walikuwa wakianguka toka juu ya miti yaani ilikuwa ni tafrani tupu na yote hiyo ni kutafuta utajiri