Malecela and Dr. Salim - Into Oblivion?

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2006
Messages
2,368
Points
2,000

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2006
2,368 2,000
Mkapa alifanya kosa kubwa kumwachia JK Urais. Sijawahi kusema kwamba Mkapa hakuwa na dosari. Hata hivyo, ubora wake ambao ninauzungumzia ni mlinganisho kati yake na waliopita, na kujenga kwake uchumi. Udhaifu ulikuwepo vile ile.

Itabidi nikukumbushe kwamba umewahi kutusimulia kuhusu MTANDAO ambao ulimshinikiza Mkapa ampe JK Urais. Kama ulisema kweli, basi huenda Mkapa hakuwa na njia bali kumwachia nchi JK. Tulaumu huo mtandao ndani ya CCM.

Tumetumia takwimu za BoT na za wachumi wengine wa ndani na nje ya nchi kusema wamba Mkapa alijenga uchumi. Wewe unasema hakujenga uchumi bila takwimu. Zipo takwimu zinazoonyesha kwamba unachosema sio kweli.

Nimekuuliza unitajie hao viongozi unaosema JK amewafukuza kazi, na umenipa mapolisi waliofikishwa mahakamani baada ya kuua huko Sinza. Sasa kweli Mzee Es, hao makoplo ndio viongozi unaosema JK amewafukuza kazi?

Kupata mali baada ya kufanya kazi za ngazi za juu ndani na nje ya nchi kwa miaka kama 40 sio kupata utajiri wa haraka. Nadhani Mkapa alikuwa na fedha za kutosha kujenga jumba hata wakati alipokuwa waziri wa Nyerere. Sote tunajua kwamba angejenga ghorofa zito au apartment block wakati huo Mwalimu angemtolea mijimacho mikali ajabu. Angemuita mhuni. Mwalimu alipendezwa zaidi na viongozi aina ya Sokoine ambao walikamata mtu yoyote aliyejaribu kutajirika.

Wizi ni mbaya, lakini kuwa na mali sio vibaya. Kuna wakati Sumaye alianzisha shamba Dodoma, watu wakapiga kelele. Akija mzungu akafungua shamba kubwa na akaweka wazawa wamfanyie kazi za kimanamba, hakuna mtu anazungumza. Lakini akianzisha shamba Sumaye au Mzindakaya, watu chungu mzima wanasema ameiba! Hii hali inaturudisha nyuma. Lazima tujifunze kufurahia wazawa wanapoinuka. Tusione uchungu.

Mimi nafurahi ninapoona wazawa wanavyoangusha majumba kule Mbezi. Kama wameanza kuangusha apartment blocks za nguvu Ubungo na sehemu nyingine vile vle, basi tuwapigie makofi, ili wazidi kuwekeza. Ndiyo nchi inavyojengwa. Sio kwa kuambatia umasikini tu!

Nigependa nione mwaziri na viongozi wakuu wote waliostaafu wanaanzisha mashamba makubwa ya kilimo cha kisasa. Waweke vifaa vya umwagiliaji, na nyumba za nguvu zakuishi kwenye hayo mashamba. Huo uwezo wa kufanya hivyo kwa fedha taslimu au kwa mikopo wanao, lakini wengi wao wanawaogopeni. Mtakasirika! Masikini, wastaafu wetu wamebaki wanafanya vijibiashara vidogo vya kujifichaficha, kama vya kuwa na teksi bubu na bar zinazouza kreti tano, mbuzi wawili na nusu kuku sita kwa siku!

Augustine Moshi
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined
Feb 25, 2006
Messages
3,348
Points
1,250

Kitila Mkumbo

Verified Member
Joined Feb 25, 2006
3,348 1,250
Ujasiri hasa wa Kikwete kufukuza viongozi tutauona pale ambapo atawafukuza viongozi aliowateua yeye mwenyewe watakapovurunda. Na ingekuwa busara kama angeanza na yule Naibu Waziri wake aliyedanganya kazini kwake kule Botswana. So far aliowafukuza ni wale walioteuliwa na Mkapa. Na isitoshe mtu kama Mahalu waliokuwa na ugomvi naye miaka nenda na alishamshauri Mkapa amfukuze kazi siku nyingi akataa kwa sababu alizotoa hazikuingia akilini kwa Mkapa.
 

Spiderman

JF Admin
Joined
Jan 1, 1970
Messages
7,220
Points
1,250

Spiderman

JF Admin
Joined Jan 1, 1970
7,220 1,250
Mzee Es said:
Ahsante Mzee Bob, na heshima kwa wazee wote wa bodi hii, Wazee kumradhi ninapita tu sio mhamiaji, lazima niwe mkweli hii forum kwangu ni baridi mno, ni forum kali na ya heshima no Question or butts about it ila bado ninasubiri itakapotokea, yaani yenye fimbo na mawe na mavitu, bwana Filga kudos, ila nitapita tu ikibidi otherwise heshima mbele wakuu! bado niko US, mpaka mwisho wa wiki hii ndio nitarudi bongo tena baada ya kama miezi miwili huku majuu kusafisha macho,

Mzee Filga heshima Mkuu tena, ila tu nitoe salaam kwa wakuu wote wanaonitumia message mbali mbali kuwa zimefika na heshima kwenu wote, hatuna kijiwe kwa sasa, lakini ninaamini kinakuja karibuni na guess what? yaani nina mavitu mpaka yanataka kuniangusha ninasubiri kuyamwaga!

Haya mzee Filga na wazee wote heshima mbele!
Nafurahi kukuona Mzee Es Huku.. na nimatumaini yangu tutashirikiana katika kuiendeleza hii forum. Asante sana!
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Mzee Mwanasiasa,

Kitu kimoja ni clear kwa viongozi wote waliochaguliwa na Mzee JK, ukipaka hurudi tena, nenda mawizarani utaona huo ukweli hakuna anayecheza, ni waziri wa fedha peke yake ndiye untouchable, wengine wote ni Mungu nisaidie,

JK amefukuza viongozi wa Mkapa, na the message is very clear kwa viongozi wote kuwa ukicheza ni on your own risk, ndio uongozi I mean huenda Mzee JK ana mapungufu katika sehemu zingine kikazi lakini at least la muhimu kuliko yote ya kuoneana aibu na kuhamishana hiylo hana, nilikuwepo kwenye mkutano pale foreign wakati anamwambia Asha Rose kazi ya kuwarudisha mabalozi niachie mwenyewe, Mkapa dakika ya mwisho anawahamisha marafiki zake kina Moses kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine na wameshakaa huko nje miaka kibao! JK amesema mbele ya public kuwa maika minane ya ubalozi inatosha, watu warudi wengine waende nao!

Mzee Filga,

Ahsante sana, lakini ninaelekea ukingoni, lakini nitakuwepo nikiwepo au ikibidi!

Kwa wazee wote wa BCS, ndio kwanza tumeerudi bongo bado jua ni lile lile, sasa ngoja tutulie kidogo tuone njia iko wapi, maana kile kijiwe ni marehemu sasa ngoja tuone kwanza,

ahsanteni wazee!
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,848
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,848 2,000
Viongozi wawili ambao wote waliwahi kuwa Mawaziri Wakuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamebakia kuwa ishara ya "kilichotokea" CCM. Leo hata hivyo najiuliza kuwa kama Dr. Malecela na Dr. Salim wataenda katika historia kwa kumbukumbu nzuri au kumbukumbu ya kushindwa kujitetea mbele ya nchi yao. Wote wawili inadaiwa wanawafuasi wengi katika CCM na bila ya shaka kila mmoja wao alidhani atapewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania. Kwa jinsi mambo yanavyokwenda sidhani kama Dr. Malecela au Dr. Salim atakayepata nafasi hiyo tena.

Je, watanzania watawakumbuka vipi viongozi hawa? Ukiondoa kukumbukwa kwa kuwa Katibu Mkuu wa OAU na the tanzanian who almost became the UN Secretary General na kwa upande wa Dr. Malecela mtu aliyeshinda kwa asilimia 99 nafasi yake na kuchaguliwa kwa zaidi ya asilimia 90 jimboni kwake, watu hawa wawili watakumbukwaje na Taifa leo? Au ndio wanaenda into oblivion?
 

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
Kumbe na nyie waoga, sasa mnataka Slaa awe shujaa huku nyie mnaogopa kusema hata kwenye mtandao tu?

Sasa hapa mnamwogopa nani? Haogopwi mtu hapa bwana!
 

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
Bi Senti 50,

Usimsikilize Jasusi, yeye ni rafiki wa Salim na Malecela kwahiyo anataka wasiguswe, ni janja yake tu. Wewe jadili tu, ile ukilipukiwa na mabomu usije ukasema mimi nilikudanganya, afterall utajuaje ubaya wa mabomu bila kukuunguza japo vidole?
 

Kalamu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2006
Messages
874
Points
0

Kalamu

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2006
874 0
ok I'm lost here. mbona mnagwaya? nilitaka kuchangia kitu lakini ukiona wenzio wanakwepa kitu gizani na wewe kwepa.. so I'll wait.
...."Ukiona wenzio wanakwepa kitu gizanina wewe kwepa"
This must rank up there with the best of them we have seen in JF.

Thank you Bi. Senti, I had to reach for tissue on that!
 

Forum statistics

Threads 1,382,148
Members 526,283
Posts 33,820,716
Top