Malalamiko kuhusu kuvunjwa msikiti, uhamisho wa wahadhiri Waislam UDOM

unasema hivyo kwa kiburi kwa kuwa ni dini ya kiislaam..Hivi ingekuwa ukristo hasa catholic ungesema maneno hayo ya kiburi??..

Uislaam unapigwa sana vita! mkuu acha chuki dhidi ya uislaam..Kukosoa ni jambo jema ktk jamii lakin tumia lugha ya staha!

Ni vema tukaishi kwa kuvumiliana, kuheshimiana na tushirikiane pamoja na uwepo wa tofauti zetu za kidini..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiwa mkweli uwe mkweli. Unaowatolea mfano, wakatoliki hata siku moja hawafanyi makosa ya aina hiyo. Katoliki ni taasisi. Hujiridhisha kabla ya miradi yao. hata siku moja hawawindi kujenga mijini maana wanahitaji maeneo makubwa ili kuweka taasisi zao.

Kosa la wenzetu kutaka kuwa exclusive. kujiona ni wakipekee. hata chuo kikuu wawe wa kipekee wakati ni sehemu ya taaluma. Kwa nini uhangaike kujenga msikiti ndani ya eneo la chuo? Yaweza kuwa ni sawa lakini njia hiyo iliyotumika ni sahihi? ekari 20!!
 
Mbona document za kuruhusiwa wanazo.
Mkuu,
Tatizo letu kubwa nchi hii ni unafik. Likija jambo ambalo linagusa upande wangu ni lazima nitetetee upande wangu hata kama najua sio sawa. Tutawezaje kuondoa utawala mbovu wa kinafiki unaolikumba Taifa hili iwapo sisi wenyewe tuko hivo hivo? Kwa sababu tu hii kitu inagusa dini nyengine ambayo hatukubaliani nayo ndio kisa cha wengi kuukataa ukweli.....jamani! hebu tujiulize tutafika kweli??? Tunatafautiana vipi na watawala ambao kila uchao tunawapigia kelele ni wabinafsi?
Kuweni serious jamani, kwenye ukweli usemwe hata kama utakuumiza lakini utakuweka huru!!
 
Mwanzoni uongozi wa chuo ulitoa eka kumikumi kwa Waislamu na Wakiristo wajenge nyumba zao za ibada!

Waislamu wakafuata taratibu zote za ujenzi ikiwemo kupata vibali vya ujenzi

Wakaanza Ujenzi huku chuo kikiwa na taarifa zote kwa mujibu wa sheria

Lakini uongozi mpya wa UDOM baada ya ule wa mwanzo kwa sababu zinazoonyesha dalili za UDiNI za uongozi huu mpya wakavamia na Kuvunja Msikikti uliokuwa ukijengwa

Hata uvunjwaji haukufuata sheria za kuvunja majengo yaliyojengwa bila taratibu maana lazima ingetanguliwa na stop order

Na ili kulizima Jambo Hilo Wakafukuza Watumishi Waislamu hapo UDOM na kubakisha wanne tu katika nafasi za Uongozi huku Zaidi ya Asilimia 88 waliobaki ni WAKIRISTO

Huu Udini ni Kansa kubwa mno na ninavyowajua Waislamu hawatokubali huu Udhalimu maana ni Uonevu wa wazi!
Sikiliza clip hii halafu nielimishe kama kuna taarifa iliyopotoshwa. Kama ni kweli basi kuna tatizo kwa ushabiki huu. Tukizungumzia mambo ya kidini lazima tuwe wakweli kama dini zinavyotaka. Hasa sikiliza kuanzia 7:40

 
Yes, but usiombe jambo la kijinga na kutpitiswha na watu wajinga halafu mwelevu akiliona ulalamike. That is illogical! Hakuna cha dini wala kingine. Ni suala la uelewa.

Unaandika barua kama hiyo isiyojieleza nini ni tatizo. Ni kuhamishwa waislamu au msikiti kuzuiliwa? Kama ni kuhamishwa kote, UD, SUA, NIMR staff wamehamishwa tena seniors. La kujiuliza ni kwa nini seniors hao wa UDOM wote ni waislamu? waliingiaje wote wakiwa waislamu watupu. Hapo ndo utajua historia ya kijinga ya UDOM. Tusipende kuficha upuuzi wa watu walioshindwa kubadilika.

Ukisoma ubadilike. Usipobadilika unaitwa mpuuzi. Hadi level ya Chuo kikuu bado dini na kabila na ukoo ni tatizo kwako? Kama unaona dini ni muhimu kuliko kingine hama chuo kikuu. Dodoma imejaa mapori, peleka sadaka zako huko ujenge madrassa na himaya yako, kuliko kuomba ekari 20 za msikiti mmoja uwe na himaya ndani ya eneo la serikali.
nonsense!!!!
 
Yaani hapa ndo nayaonaga maafrika kama ni matahira...
Dini za mapokeo.. dini za kuletwa na meli.. Lakini zinatugawa na kutuhabiria uwezo wa kuyaendeleza mazuri tunayoweza kufanya tukiwa wamoja..!!
Shameful!
 
Mkuu hilo eneo walipewa wao na wenzao wakristo kwa ajili ya matumizi gani?
Lilitolewa kinyume na utaratibu (na watawala wa UDOM waisilamu), na ndio maana waliolitoa eneo la chuo wametawanywa ili wasipange mikakati kwa pamoja
 
Tatizo hawa watu ni watu wakulalamika tu. Chuo cha tanesco morogoro waliomba kuazimwa majengo wafungue chuo baadae wajenge chao lakini hadi leo wameshabinafsisha.

Kwani udom kuna makanisa?? Kwanini wao wanalazimisha kujenga msikiti??
Ujue kuna kipindi Udom kilifanywa kama chuo cha Dini na visheria vya kidini vikaanza kupenyezwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ipo hivi, hao wahadhiri wa waislamu waliohamishwa walipaswa kufukuzwa kazi kabisaa na kufungwa jela na wala si kuhamishwa tuu kwani kosa walilofanya la kubadili matumizi ya ekari10 za eneo la chuo cha UDOM ( ambacho kimsingi eneo la serikali) na kulibadili kinyemela kwa ajili ya kujenga 'msikiti wa UDOM' bila kulishirikisha baraza la chuo UDOM ni kosa kubwa sanaa! ..........tena mkiendelea na uchochezi wenu tutafunguka kisawa sawa
HEBU FUNGUKA NAO WAFUNGUKE.
 
Mkuu,
Tatizo letu kubwa nchi hii ni unafik. Likija jambo ambalo linagusa upande wangu ni lazima nitetetee upande wangu hata kama najua sio sawa. Tutawezaje kuondoa utawala mbovu wa kinafiki unaolikumba Taifa hili iwapo sisi wenyewe tuko hivo hivo? Kwa sababu tu hii kitu inagusa dini nyengine ambayo hatukubaliani nayo ndio kisa cha wengi kuukataa ukweli.....jamani! hebu tujiulize tutafika kweli??? Tunatafautiana vipi na watawala ambao kila uchao tunawapigia kelele ni wabinafsi?
Kuweni serious jamani, kwenye ukweli usemwe hata kama utakuumiza lakini utakuweka huru!!

Ahsante sana kwa hii post
 
Sikiliza clip hii halafu nielimishe kama kuna taarifa iliyopotoshwa. Kama ni kweli basi kuna tatizo kwa ushabiki huu. Tukizungumzia mambo ya kidini lazima tuwe wakweli kama dini zinavyotaka. Hasa sikiliza kuanzia 7:40


umeona sasa, huu ulikuwa uhalifu ambapo watuhumiwa walioshiriki 'kughushi' walipaswa kupelekwa jela kabisa na wala si kuhamishwa
 
babaaa babaaaa fojaliiii babaaaa......wanakaaa watu2 na kuamua maamuzi ya barazaa! ndiyo maana nimekwambia busara ya hali ya juu imetumika apo ku-neutralize 'wizi' uliofanywa na hao 'wahadhiri'
nguvu na rasimali kubwa sana zilitumika kukijenga hicho chuo lakini output quality bado haiendani na uwekezaji uliofanyika, ngoja safisha safisha ipite kwanza apo, kama mtakumbuka vizuri kipindi nyuma adi wa waalimu wa shule za msingi walikuwa wanapelekwa kufindisha apo .....
Duuh ni hataree

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Dhana za dini naona znaanza kupenya taratibu tu na impact yake ni maangamizi ya wasio na hatia

Hili ni la kuangalia kwa jicho la nne if possible c la kupuuza!

Wakristo, Waislamu wote ni binadam na wote wanaamn katika Mungu alie mmoja kila mtu apewe heshima yake tu!
 
Nanukuu:
" Sisi hatusemi kabisa kwamba uhamisho na uvunjaji wa Msikiti vilifanywa kwa sababu ya udini. Lakini kukosekana kwa umakini katika hatua hizo kunaweza kukatengeneza fursa ya dhana hiyo kupenya."
Mwisho wa kunukuu.

Naona awamu hii maustadhi mnatoa malalamiko yenu kwa lugha laini sana, iliyojaa unyenyekevu , adabu na ustaarabu mno.
Nafikiri mmesoma upepo mkaona aliyeko juu pale Jumba jeupe ni sampuli gani, mkikinukisha na yeye anakinukisha tena kwa risasi za moto kama uncle Ben wa Masasi alivyowafanya wapemba mwaka ule wa utawala wake.

Poleni sana aiseee.
Ila amri ikishatoka juu kushuka chini huwa hairudi tena juu ilikotoka.
Chief hawamu hii wanapaiga risasi yeyote yule...awaangalii Dini gani

,,C umeskia ya itigi ndani ya kanisa wamemtundulisu mchungaji,,yani hawa watawala hawa,,,!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu fafanua vizuri walibadilije matumizi ya hizo heka kumi?,
kwani mwanzo walipewa za kufanyia nini?.au ilikua ni kwajili ya kufugia mbuzi au ile mbuzi katoriki.
ipo hivi, hao wahadhiri wa waislamu waliohamishwa walipaswa kufukuzwa kazi kabisaa na kufungwa jela na wala si kuhamishwa tuu kwani kosa walilofanya la kubadili matumizi ya ekari10 za eneo la chuo cha UDOM ( ambacho kimsingi eneo la serikali) na kulibadili kinyemela kwa ajili ya kujenga 'msikiti wa UDOM' bila kulishirikisha baraza la chuo UDOM ni kosa kubwa sanaa! ..........tena mkiendelea na uchochezi wenu tutafunguka kisawa sawamk
 
Unafikiri. Kwanini usitafute uhakika wa taarifa? Ukifikiri bila taarifa unaweza ukakosea ikiwa kweli msikiti umenjwa hata kama ujenzi haukukamilika
Hii "issue " niliifuatilia sana hasa baada ya taarifa kutoka kwenye social media, mwanzo nilifikiri wamevunja msikiti nikashangaa mbona hivyo?! Lakini ktk taarifa iliyotolewa na baraza la chuo, ni kuwa yalifanyika makosa ya kutoa eneo la chuo na watu wasiokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo, inasemekana mamlaka ya kumega eneo la taasisi na kulipangia matumizi mengine ni ya Baraza la Chuo (?!) hivyo kibali kilitolewa kifigisu figisu na watu wasiokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom