Makutano Show: Exclusive Interview na Mhe. John Mnyika - Oct 06, 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makutano Show: Exclusive Interview na Mhe. John Mnyika - Oct 06, 2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makutano Show, Oct 5, 2012.

 1. Makutano Show

  Makutano Show Verified User

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana-JF

  Jumamosi hii katika Makutano nitakuwa na Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Mheshimiwa John Mnyika. Na kama kawaida ya kipindi tutagusa kuanzia maisha yake ya kawaida mpaka kwenye siasa. Kama ada, kipindi kinaendeshwa na maswali mengi kutoka kwa wananchi hivyo napenda kuchukua fursa hii kuomba kama una swali liweke hapa na Mhe Mnyika atajibu katika kipindi Jumamosi kuanzia saa tisa mchana hadi kumi na mbili jioni katika 92.9FM Dar, 93.3FM Dodoma, 98.6FM Arusha/Moshi, 101.7FM Mwanza na pia online kupitia www.ustream.tv/channel/makutanoshow


  Natanguliza shukrani.

  Karibu.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru sana.

  SWALI 1:
  Mhe. Mnyika ni Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA. Akiwa kama msemaji mkuu wa chama ni utaratibu gani unaotumika kupata wagombea Urais?

  SWALI 2:
  Kuna watu wameanza kujitangaza kugombea Urais ndani ya CHADEMA na hali hiyo imesababisha wanachama wengi kulaani hali hiyo kwani inazorotesha uhai wa chama na kusababisha malumbano yasiyo ya msingi. Akiwa kama msemaji mkuu wa chama anazungumziaje hali hiyo?

  SWALI LA 3
  CAHDEMA ni chama kinachokua kwa kasi kubwa lakini kimeshindwa kujitangaza vema kutokana na kutokuwa na vyombo vyake vya habari ambavyo vitakuwa vinatangaza kwa mapana sera zake na matukio mbalimbali yanayoihusu.

  Akiwa kama mkuu wa uenezi anatumiaje nafasi yake kushawishi chama kuwa na vyombo vyake vya habari kama TV, Radio na magazeti?

  Nashukuru sana na naomba maswali haya yajibiwe kwani yana maslahi mapana kwa Chama na Taifa.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Makutano Show ni nini kama ni kipindi kinafanyika wapi kwenye TV au JF au wapi tupe ufafanuzi tufahamu ili na sisi tuchangie.. samahani lakini.
   
 4. Sanene

  Sanene Senior Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi nina swali 1 tu:

  Bunge linaanza siku za karibuni umejipanga vipi kuhakikisha ile sheria mbovu ya SSRA inafanyiwa marekebisho stahili?
   
 5. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Swali:

  Katika kikao cha Bunge la bajeti kilichopita, John Mnyika aliwahi kutamka kwamba Serikali ya Rais Kikwete ni "Dhaifu". Je, anafikiri ni kwanini Serikali ya Rais Kikwete ni Dhaifu?
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,833
  Trophy Points: 280
  Kina fanyika kwenye radio studio(magic fm, kila j,mosi) mkuu
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Swali kwa Mh Mnyika:

  Baada ya kutueleza watanzania kuwa rais wetu ni dhaifu ulipata misukosuko mwingi na baada ya ile misukosuko hujasikika tena kuelezea udhaifu wa huyu rais wetu Kikwete, je wewe Mh ni mwoga?

  Je udhaifu wa Rais Kikwete unavyozidi kulighalimu taifa letu kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wewe na CHADEMA mmechukua hatua gani?
   
 8. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Swali la kwanza kwa mh Mnyika,

  Karibuni zimetokea tetesi kuwa chama chako kinapata misaada ya moja kwa moja toka mashirika na vyama vya kidini kama Jesuit na CDU, Je uko tayari kutuelezea ni misaada ipi na ina dhamira gani?

  Swali la pili,

  Siku za nyuma kwa nyakati tofauti viongozi wa CHADEMA waliwahi kutoa kauli kuwa nchi haitatawalika na sasa hivi tunashuhudia vurugu na mauaji sambamba na maandamano. Je, hii ni njia mojawapo ya kuhidhoofisha serikali iliyopo madarakani na nini hatima yake? Toa ufafanuzi...

  Ni hayo tu
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mingoi

  Majibu (ingawa mimi si Mnyika):

  Swali la kwanza misaada inayopokea CCM kutoka China na Russia na Korea ya Kaskazini watu wasiomtambua Mungu huwa ni ya nini? Ukijijibu hili automatically utakuwa umejibu swali lako mwenyewe.

  Swali la pili:
  Kuhusu mauaji, CHADEMA has nothing to do with it kwani wahusika wote wa mauaji wameshafikishwa mahakamani na CHADEMA kama chama hakiusiki. Serikali iliyopo madarakani ilishadhoofika siku nyingi na siyo kwa sababu ya CHADEMA bali kwa kushindwa kutimiza yale waliyoyahaidi kwa wananchi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. M

  Mndokanyi JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Swali la kwanza:
  CHADEMA inazungumziaje kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi? Je, inaona hatua zinazochukuliwa ni sahihi?.

  Swali la pili:
  Wanachama wengi wa CCM wanajiunga na CHADEMA, chama kimejipanga vipi ili kuzuia migogoro iliyoko CCM ikahamia CHADEMA?.

  Swali la tatu:

  Naomba kumuuliza Mh Mnyika, tumekuwa tukisia watu wakitangaza nia ya kugombea Urais nje ya mfumo wa kawaida wa chama, wengine mpaka wanaenda kutangaza kwenye vikao vya CCM. Je, CHADEMA ina msimamo gani kwenye jambo hili? Je, hamuoni kwamba kuna wengine wana malengo mabaya kukivuruga CHADEMA?
   
 11. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nina maswali mawili kwa mh JJM:

  1. Mnyika mmefikia wapi na swala la kugomea posho? Maana nasikia bado mnalamba kama kawaida.
  2. Na ni kweli mwenyekiti Mh F. Mbowe alikataa hadharani shangingi la kiongozi wa upinzani bungeni lakini akalichukua gizani?
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  [Isisomwe hewani hii]
  Hallo Sister Fina Mango (FM) nakutahadharisha mapema usimuulize Mh Maswali ya Personal mf kama ana mchumba au ameoa nk we muulize Diva (Loveness Luv) alivyoumbuliwa!!
   
 13. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi nataka kumuliza kwa nini viongozi wa chadema akiwemo yeye wanapenda kujilimbikizia mavyeo mengi, kwani hakuna wengine wa kufanya hizo shughuli?

  Na, Jee haoni kuwa yeye ni one term member of parliament?

  Ni hayo tu
   
 14. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  politiki

  Mkuu unaabika, unaingilia mambo yasiyokuhusu na uwezo wako wa kujibu maswali ni 0 hata kama unajaribu kumjibia Mnyika ni aibu ilioje kwa wewe kuja kukijibia chama.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. 2

  2015 Senior Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Swali:
  Kuna habari zipo mitaani kuwa Mh Mnyika hakufanikiwa kumaliza chuo kikuu hivyo basi hapo alipo hana degree, je kuna ukweli wowote juu la hili? Na kama ni hapana alimaliza lini?
   
 16. M

  MILLIONS MOVEMENT Senior Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina maswali mawili kwa JJM

  1) Chama kinakabiliwa na propaganda za Udini zinazoenezwa na wapinzani wenu kisiasa kuna mkakati gani maalum mmeuandaa kukabiliana na propaganda hizo na zibaki historia.

  2) CHADEMA kwa sasa inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo migogoro ndani ya chama, huoni sasa ni wakati muafaka wa kuanzisha kikosi kazi ambacho kitatatua migogoro iliyopo na kuhakikisha kazi yako ya uenezi inafanikiwa katika kipindi hiki kuelekea 2015
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  SWALI LANGU NI MOJA LAKINI LINA VIPENGELE A na B

  A: Tumekuwa tukiingia milango ya ubungo terminal kwa sh 200 mbaya zaidi unaingia kwa mguu wako yani hakuna chombo cha kukubeba uingie ndani...lakini tulikusikia mh mnyika ukipaza sauti wewe na wabunge wenzako baadhi wa Dar kuhoji swala la kupanda kwa nauli ya kivuko cha kwenda kigamboni kutoka tshs 100 mpaka 200, swali langu je hao wanaoishi huko kivukoni wana tofauti gani na sie wapiga kura wako ambao umekaa kimya tangu uingie bungeni? Ina maana kero zawana kigamboni zinakugusa kuliko zetu wapiga kura wako? Kama jibu ni hapana, sasa je, utatusaidiaje wana ubungo tuingie na sisi pale terminal ubungo kwa sh 100? Tena sisi wala hatutaki kubebwa tutaingia kwa miguu yetu wenyewe acha wa kigamboni wabebwe

  B: Swali la nyongeza, ni kwanini Kwa mfano, wakazi wa Kiluvya walioko katika Jimbo la Ubungo wanalipa nauli Sh. 900 kutoka Kiluvya hadi Ubungo wakati wakazi wa Mbagala wanalipa Sh 450 kutoka Mbagala hadi Mwenge. Je, wewe Mh. Mnyika kama mbunge wetu wa jimbo letu hili la Ubungo, ulipata wapi ujasiri wa kwenda kuwatetea wakazi wa Kigamboni wanaolipa Sh. 200 badala ya sisi wapiga kura wako tuliokutuma ukatuwakilishe bungeni ambao hulipa Sh 1,200 kutoka Kiluvya hadi Posta. Je, huoni kama umetutelekeza baada ya kupata ulichotaka (ubunge)?
   
 18. L

  Lekakui JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,411
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Swali:
  Katika siku za hivi karibuni msajili wa vyama vya siasa John Tendwa alisikika hadharani baada ya mauaji ya mwandishi wa habari wa channel ten kwamba kuna vyama vinavyosababisha mauwaji katika mikutano yao na yuko tayari kuvifutia usajili, ofcourse kila mtu alielewa alikuwa ana lenga chama gani. Je, nyie kama CHADEMA mmechukuliaje hilo tamko lake? Na nyie kama chama, kama itatokea kukifuta nyie mmejiandaa vipi kukabiliana na hali hiyo?

  Swali 2:
  Nimekisia kwenye manispaa nyingi ambazo CHADEMA mnaziongoza zimeanza kupata kashfa za aina tofauti tofauti, na hivi juzi tumesikia meya ya manispaa ya Mwanza/Nyamagana amechaguliwa wa CCM, je nyie kama chama mnalichuliaje hili suala ili basi watu waendelee kuwaamini kwamba mkishika nchi mambo hayatakuwa kama yanavyoenda sasa?

  Swali la 3:
  Kuna madiwani wenu walihongwa na chama fulani kule Arusha ili wampitishe meya, je suala hili limefikia wapi? Na je Arusha bado meya aliyeko sasa hivi mnashirikiana naye kuleta maendeleo?na je wale madiwani wenu mliowafukuza mbona hatujasikia kuhusu uchaguzi?

  Ni hayo tu and ningefurahi Fina kama maswali yangu yote yatajibiwa
   
 19. g

  gnsulwa Senior Member

  #19
  Oct 6, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Lilipokwisha bunge la budget ulifanya ziara na kuongea na wapiga kura wako karibu kila kata ya jimbo la Ubungo.

  Moja kati ya kero walizokutolea wapiga kura wako ni tatizo la maji.

  Wakati unafanya hiyo ziara maji Mbezi kwa Yusuph yalikuwa yakitoka angalau mara 1 kwa wk 2. Sasa hv yanatoka mara 1 kwa wk 3 au 4.

  Je tuseme umeshindwa kutatua tatizo la maji kwa Yusuph?
   
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lakini we fina na wenzako mnatusumbuaga tunajipinda kutafuta maswali jamaa wakija hapo hamuwagongi maswali yetu,kuweni kama waandishi wa marekani,urafiki pembeni
   
Loading...