SWALI LANGU NI MOJA LAKINI LINA VIPENGELE A na B
A: Tumekuwa tukiingia milango ya ubungo terminal kwa sh 200 mbaya zaidi unaingia kwa mguu wako yani hakuna chombo cha kukubeba uingie ndani...lakini tulikusikia mh mnyika ukipaza sauti wewe na wabunge wenzako baadhi wa Dar kuhoji swala la kupanda kwa nauli ya kivuko cha kwenda kigamboni kutoka tshs 100 mpaka 200, swali langu je hao wanaoishi huko kivukoni wana tofauti gani na sie wapiga kura wako ambao umekaa kimya tangu uingie bungeni? Ina maana kero zawana kigamboni zinakugusa kuliko zetu wapiga kura wako? Kama jibu ni hapana, sasa je, utatusaidiaje wana ubungo tuingie na sisi pale terminal ubungo kwa sh 100? Tena sisi wala hatutaki kubebwa tutaingia kwa miguu yetu wenyewe acha wa kigamboni wabebwe
B: Swali la nyongeza, ni kwanini Kwa mfano, wakazi wa Kiluvya walioko katika Jimbo la Ubungo wanalipa nauli Sh. 900 kutoka Kiluvya hadi Ubungo wakati wakazi wa Mbagala wanalipa Sh 450 kutoka Mbagala hadi Mwenge. Je, wewe Mh. Mnyika kama mbunge wetu wa jimbo letu hili la Ubungo, ulipata wapi ujasiri wa kwenda kuwatetea wakazi wa Kigamboni wanaolipa Sh. 200 badala ya sisi wapiga kura wako tuliokutuma ukatuwakilishe bungeni ambao hulipa Sh 1,200 kutoka Kiluvya hadi Posta. Je, huoni kama umetutelekeza baada ya kupata ulichotaka (ubunge)?