Makosa hatari yanayomgharimu Tundu Lissu!

Makosa hatari yanayomgharimu Tundu Lissu!

Wenye akili tu mjiulize

Kampuni imesajiliwa au haijasajiliwa??
Kama imesajiliwa kamati ilimdanganya Rais...
Kama haijasajiliwa Rais anafanyaje mazungumzo na Kampuni hewa???
Wewe kilaza umeeleshwa kua huyo aliekuja kwenye mazungumzo ni kutoka Barrick gold sio Acacia ...sikiliza au soma vizuri taarifa.hao wana hold 64% ya hisa za acacia ..nisalimie tundo Lisa.
 
Lissu hajawahi kumkosoa Mbowe au lowassa kwa mtindo huo pale walipo au wanapokosea!
Hajaona cha maana cha kuwakosoa watu hao. Ni vyema watu wengine hata wewe ufanye kazi hiyo kama unadhani inawezekana. Kwa mfano, mimi binafsi sifurahii kabisa Lowassa kuwa CHADEMA kwa vile namuona kama sehemu ya mfumo wa CCM uliohujumu na unaoendelea kuhujumu mustakabali wa Tanzania hadi leo hii tena ulioua demokrasia ya kweli nchini. Lakini sina kashfa maalumu nayoweza kuielekeza kwa Lowassa binafsi nje ya mtandao na uongozi wa CCM.

Hata hujuma kubwa kubwa zinazotajwa leo hii na wana-CCM wenyewe, hulisikii jina la Lowassa likitanabahishwa. Utasikia Chenge, Mkapa, Kikwete n.k. lakini sio Lowassa. Ndio maana naona jana na yeye kajitokeza kusanifu "utendaji mzuri" wa Magufuli kwenye makinikia. Tunasubiri kibwagizo cha Mkapa na Kikwete.

Kuhusu Mbowe, hakuna kiongozi aliyejenga chama imara cha upinzani na yeye binafsi kusimama kama nguzo ya uhakika ya upinzani Tanzania kama Mbowe. CHADEMA ilianza kama "club of gentlemen"; haikuwa na nguvu yoyote kisiasa hadi Mbowe aliposhika hatamu. Hadi leo hii anayo jeuri ya kusema kuwa HANA BEI - katika nchi yenye utawala unaoetegemea kuona kila mtu akijinyenyekeza na kujikomba kwake ili apate riziki. Ni ujasiri wa kipekee katika nchi hii ambayo kuwa mpinzani/mkosoaji unakuwa adui wa Rais, serikali na chama tawala. Kama ana makosa basi yanafunikwa kwa mbali sana na sifa yake hiyo. Unamkosoa nini mtu wa aina hiyo huku hujuma za kutisha zikiendelea kwenye sekta za madini, nishati, ujenzi, n.k.? Jaribu.
 
Ha
Swali lako halihusiani na makosa aliyoyafanya lissu..halina mantiki kwenye hoja hii.

Swali la kujiuliza je lissu anamkubali Nyerere?

Lissu anaukubali muungano?

Lissu anamkubali lowassa?

Lissu anaitetea Acacia?

Iwe amehusika au hajausika katika kupendekeza au kupitisha sera zilizotufikisha hapa.
Hata Mimi simkubali Nyerere,tuko wengi tu tusiomkubali.Hakuna mtu anayekubalika kwa watu wote,kwa nini unalazimisha watu wamkubali Nyerere?
 
Lissu ni hazina ya Taifa lipi tuache uyahawani. Tunajua maana ya hazina? Lissu kapotea tangu 2015 baada ya kula matapishi yake mwenyewe. Mpuuzi tu
 
Acha wivu.unafikiri bila lisu kumzodoa sizonje angeunda kamati ya pili??
 
Niliwahi kumpigia chapuo Ndugu Tundu lisu kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliotakiwa kushika Uongozi waTaifa hili mwaka 2015 kama kijana na kama mtu mwenye msimamo ulio thabiti..sikukosea bali yeye mwenyewe ameshindwa kujitambua na kujipanga na hatimaye kuipoteza sifa hiyo adimu kwa sababu zifuatazo na ambazo zitaendelea kujitanabaisha kadri muda unavyojiri.

1-Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.

2-Tundu lissu haamini katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar na huu ni uvunjifu mkubwa wa katiba.

3-Tundu lissu alikosea sana kukubali kuwa mmoja wa wanachadema waliompokea mtuhumiwa mkuu wa ufisadi lowassa na hatimaye kugeuka kuwa mtetezi wake...leo hii lowassa hii lowassa amempinga kuhusu swala la hatua za Rais dhidi ya makanikia.

4-Tundu lissu amekosea tena kutokana na hulka yake ya jazba na arrogance kwa kukinzana na swala la kitaifa la juhudi za Magufuli katika kuliondoa Taifa kutoka mikono ya wizi wa mabepari.

5-Tundu lissu ameshindwa kuwa na msimamo thabiti na wa kiadilifu dhidi ya viongozi wa chama chake mfano Mbowe ambao ametuhumiwa kwenye ukwepaji kodi,madawa ya kulevya na uzinzi.

Kwa hayo machache nasikitika kumuona Tundu lissu akipoteza talanta na fursa adhimu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Pengine Tundu lissu angekuwa ndani ya CCM ingewezekana kufichwa kama hazina ili asiingie kwenye makosa ya kijinga ambayo yamemgharimu.

Iam sorry my broda TL but these are bitter medicines and we all have to swallow!


Niliwahi kuandika juu ya Tundu lissu....mwaka 2015 kabla ya gia za angani....Tofauti yangu mimi na yeye kwa sasa imekuja kwenye msimamo aliouchukua dhidi ya fisadi mkuu kwani naamini ndicho kilichombadilisha Tundu Lissu na ambacho kimembadilisha forever and ever!

Again sikukosea kutokana na muda niliokuwa nikiandika thread ile lakini pia kutokana na aina ya wagombea waliokuwa wakipigiwa upatu ndani ya CCM(Ukimuondoa Magufuli) na ndani ya Ukawa Original.

Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)
Tundu lissu ni mkweli asie na chembe ya unafiki na kwa kawaida wasema kweli huwa hawapendwi popote palee
 
Lissu ni hazina ya Taifa lipi tuache uyahawani. Tunajua maana ya hazina? Lissu kapotea tangu 2015 baada ya kula matapishi yake mwenyewe. Mpuuzi tu
Kapotea wapi bwege,waliopotea na kutupoteza ni hao mafisiemu kwani wamewapa wazungu madini kwa dezo Leo inakuwa shida kwa sababu ya mikataba ya kibwege iliyowekwa na mafisi
 
Tundu Lissu alishasema tunaibiwa kabla hata Rais Wetu Magufuli hajaingia madarakani!Hapa sio Rais magufuli au Lissu kasema nini? Science doesn't lie and has no boundarie and countties as well?
Mikataba ina wamilikisha kila kitu!
Ili mgodi uanzishwe lazima kuwe a mineral or minerals that is commercially viable! Kwa maana nyingine a mineral that can be extracted at profit under current economic factor and technology!na si kila kitu kinakuwa extracted at profit.
Mfano ukichukua jiwe(stone) au mchanga barabarani you will find different minerals(silicon,aluminium,gold ect) sio kwamba ni economic!our gold is not a placer one that is not free kwa hiyo inakutwa ipo kwenye miamba(miamba imundwa na madini ya aina tofauti tofauti) ambayo kati hayo madini moja au mbili zinaweza kuwa economic?
Asilimia 75 ya dhahabu inachenjuliwa migodi..hayo mabaki mengine ni uchafu(after processing) kama yangekuwa na kiwango hicho tulichoambiwa yangekuwa tailing dumps?
Huwezi kumbadilisha MTU anachoamini!cha kukusaidia tafuta geological formation ya maeneo hayo itakupa picha utaanza kuelewa mambo haya.
Ukweli utabaki kuwa ukweli
Hoja yako ni tofauti na wataalamu wa barick ambao wanakubali kuwa faida ya madini ya rare elements ipo lakini si kwa kiwango cha kupewa status ya uchimbwaji.
 
Pointless,

a) Sio lazima mtu akubalike na kila mtu. Halazimishwi kumkubali hayati, na kama binadamu ana mistakes nyingi alifanya so kumkosoa pia ni sawa

b) Wanzanzibari wenyewe hawautaki muungano maana unawanyonya na sisi sote twajua hilo.
Hizo hoja mbili hata mimi niliwahi kuziignore lakini ni valid...vipi kuhusu hoja zilizobakia?
 
Kalale ukue,labda miaka Kumi ijayo utajua kuwa kinachokosolewa ni MTU au hoja ma sio umbile la MTU.
Tundu Lissu kama hakumkubali Hayati Nyerere ni kwenye Falsafa zake na sio kwa umbo la mwili wake. Hata Mimi katika maisha yangu nimeishi nyakati za Nyerere pia sijawahi kubaliana na namna falsafa zake zilivyokuwa zinatekelezwa
Hujakubali utekelezwaji wa falsafa za Nyerere.
Lisu hazikubali falsafa za Nyerere
 
Dah Andiko hili linasikitisha sana
Nionavyo mimi liko shallow sana
Tuanze na sababu yako namba
1.Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.
Hivi ni lazima kumkubali Mwalimu? unaamini kila unachokusoma kuhusu mwalimu ndicho kweli kilichofanyika
Hiki ni kizazi cha kuhoji na siamini kama kuhoji baadhi ya maamuzi ya kipindi cha mwalimu ni kutokumkubali mwalimu
Binafsi ninapata shida juu ya maamuzi fulanifulani lakini haimaanishi simkubali Mwalimu
TAL hakuwahi kusema hamkubali mwalimu,na amekua akirejea matamshi ya mwalimu mara kadhaa hii yote inaonesha anamuheshimu.
2.Kutokuamini juu ya muungano hayo ni binafsi ila kuuvunja hapo tunaweza kusema ndio ukiukwaji wa katiba
3.EL sio kiongozi wa serikali,maswala yake na kupokelewa na chama chake sidhani kama ni ya muhimu sana wapo wengi tu upande wa pili ambao wako kwenye tuhuma mbali mbali na bado ni viongozi wakubwa nchini.
4.Binafsi naunga mkono Juhudi za Mh Rais lakini siamini kwamba wote tunatakiwa tuseme ndio wale wanaotoa hoja za tofauti wanatusaidia kupanua uelewa wetu juu ya mambo haya. hatuwezi kua na taifa ambalo wote tunasema ndio litakua ni la mazezeta.
5.Hilo la mwenyekiti wa CDM nadhani akipatikana na hatia katika hayo ndio tuhoji.
El sio kiongozi wa serilali lakini aliwahi kuwa kiongozi wa serikali.EL alituhumiwa sana na Chadema kuwa ni fisadi na ilikuwa ni hoja iliyoikuza Chadema.kumkubali fisadi kwa gia za anga ni kosa kubwa sana...na kuendelea kumtetea ndi kosa zaidi.

Mwenyekiti Mbowe anapotuhumiwa ni lazima ahojiwe au kuulizwa au kuandamwa kama ulivyo utamaduni wa enzi wa Chadema dhidi ya watuhumiwa wa CCM.
 
Tundu lissu ni mkweli asie na chembe ya unafiki...
Lisu ni kajitu kaogaa sana. Kalikuwa kanatutisha eti tutashitakiwa. Leo hii kamenyweaa, hata sijakasikia kakisema neno lolote lile. Kameumbuka na kamejificha huko kaliko.
 
Wenye akili tu mjiulize

Kampuni imesajiliwa au haijasajiliwa??
Kama imesajiliwa kamati ilimdanganya Rais...
Kama haijasajiliwa Rais anafanyaje mazungumzo na Kampuni hewa???
Rais kafanya mazungumzo na Barick sio acacia
 
Ngoja 2020 kama tutakuwepo tutaongea mengine, huyu Mshamba wa Kinyiramba anayejifanya mbunge wa Taifa ndio atajua Magu sio wa saiz yake hata kwa dawa, ila mim Lissu ni adui kwa nchi hii kuliko hata Baric na ningeambiwa nimchagulie adhabu ningemranda miguu na chensou
 
Hajaona cha maana cha kuwakosoa watu hao. Ni vyema watu wengine hata wewe ufanye kazi hiyo kama unadhani inawezekana. Kwa mfano, mimi binafsi sifurahii kabisa Lowassa kuwa CHADEMA kwa vile namuona kama sehemu ya mfumo wa CCM uliohujumu na unaoendelea kuhujumu mustakabali wa Tanzania hadi leo hii tena ulioua demokrasia ya kweli nchini. Lakini sina kashfa maalumu nayoweza kuielekeza kwa Lowassa binafsi nje ya mtandao na uongozi wa CCM.

Hata hujuma kubwa kubwa zinazotajwa leo hii na wana-CCM wenyewe, hulisikii jina la Lowassa likitanabahishwa. Utasikia Chenge, Mkapa, Kikwete n.k. lakini sio Lowassa. Ndio maana naona jana na yeye kajitokeza kusanifu "utendaji mzuri" wa Magufuli kwenye makinikia. Tunasubiri kibwagizo cha Mkapa na Kikwete.

Kuhusu Mbowe, hakuna kiongozi aliyejenga chama imara cha upinzani na yeye binafsi kusimama kama nguzo ya uhakika ya upinzani Tanzania kama Mbowe. CHADEMA ilianza kama "club of gentlemen"; haikuwa na nguvu yoyote kisiasa hadi Mbowe aliposhika hatamu. Hadi leo hii anayo jeuri ya kusema kuwa HANA BEI - katika nchi yenye utawala unaoetegemea kuona kila mtu akijinyenyekeza na kujikomba kwake ili apate riziki. Ni ujasiri wa kipekee katika nchi hii ambayo kuwa mpinzani/mkosoaji unakuwa adui wa Rais, serikali na chama tawala. Kama ana makosa basi yanafunikwa kwa mbali sana na sifa yake hiyo. Unamkosoa nini mtu wa aina hiyo huku hujuma za kutisha zikiendelea kwenye sekta za madini, nishati, ujenzi, n.k.? Jaribu.
Kwa hiyo Mbowe hakosolewi kwa kuwa kafanya mengi mazuri?
Unaachaje kumkosoa Mbowe iwapo ana mfululizo wa tuhuma ambazo wanachadema wamekuwa wakizishikia bango?

Ukwepaji kodi...Uzinzi...Ufisadi n.k
 
upinzani umebaki jamii forum,instagram na social media kiujumla but in reality hakuna upinzani Tanzania ni usanii na maigizo tu.
 
upinzani umebaki jamii forum,instagram na social media kiujumla but in reality hakuna upinzani Tanzania ni usanii na maigizo tu.
Ni maigizo ya usaliti...nashangaa kwa nini kodi zetu zinatumika kwa ruzuku badala ya kujenga zahanati
 
Back
Top Bottom