Makosa hatari yanayomgharimu Tundu Lissu!

Mrema hana uwezo wa Lissu, hivyo ni makosa kabisa kumfananisha Mzee wa Kiraracha na hazina ya Taifa.
Kwa hoja ya CCM kumuogopa lissu sio hoja!
Hoja ni makosa anayofanya Lissu
 
Yani jamaa anamfananisha mzee wa kiraracha na Tundu Antipas Lissu, hahahahaha uwezo wa Lissu ni mara mia ya babu Mrema hata yeye anajua ukichanganya na senile dementia aliyonayo basi hakuna kitu tena! Tuache mlinganisha lissu na takataka za lumumba.
Mlitaka nilinganishe uoga wa CCM kwa lissu...nimefanya hivyo.
 
meningitis, naomba nikuulize kaswali kamoja tu nalo ni...Je Mh. Tundu Lissu amewahi kuhusika kwa namna yoyote ile katika kupendekeza, kupitisha, kusimamia na kutekeleza sera zilizotufikisha hapa tulipo kama taifa?
Swali lako halihusiani na makosa aliyoyafanya lissu..halina mantiki kwenye hoja hii.

Swali la kujiuliza je lissu anamkubali Nyerere?

Lissu anaukubali muungano?

Lissu anamkubali lowassa?

Lissu anaitetea Acacia?

Iwe amehusika au hajausika katika kupendekeza au kupitisha sera zilizotufikisha hapa.
 
Kasome kwanza historia ya Tundu Lisu ili umweelewe vizuri na hutapata shida.

Tundu Lisu ndio MTU pekee aliyebaki wa kuweza kumkosoa Magufuli hadhalani.

Lakini Wasomi wengine na Wanaharakati wameamua kugugumia kimyakimya huku wakishuhudia uvunjwaji wa wazi wa Katiba.

Acheni ujinga wa kutaka kuungwa mkono kilazima kwa makosa mliyoyafanya wenyewe.

Kwangu Mimi Tundu Lisu bado atabakia kuwa MTU wangu Bora kabisa wa Kizazi hiki. Lengo lenu mnataka Tundu Lisu asalimu amri, na akisalimu amri basi adhma yenu ya kutawala kibabe itakuwa imetimia maana mnaona ndio MTU anayewasumbua ndio maana hamuishi kumtajataja.
Kwa nini Tundu lissu hamkosoi lowassa au Mbowe?
 
Wewe ni kilaza na mshamba mkubwa hiyo namba 3 ujue Lowasa hakuwa fisadi bali ccm wabaya walitengeneza propaganda za kumchafua wakawapelekea wapinzani wakaamini lakini Lowasa alipohamia chadema alianika Ukweli wote na kusema kuwa mmiliki wa Richmond ni Kikwete, usiendelee kukariri ya zamani angalia ya sasa,
Ni nani huyo katika CCM aliitengeza hiyo propaganda mbaya?Na ni nani aliyeipeleka Chadema?
Na tena ni nani ndani ya chadema aliyeipokea hiyo propaganda pekee ya ccm na kuamua kuwa iwe ajenda ya chama?

Nani huyu aliyamua iwe ni sehemu ya list of shame?

Ni nani aliyeamua kuifuta hiyo propaganda ndani ya Chadema?

Ni kwa vipi ukweli wa lowassa uaminiwe 2015 na sio wakati anajiuzulu?

Nitaendelea na maswali ya Nani na Nani na Nani?
 
meningitis ,

1. Ni kweli TL aliboronga alipotoa maneno ya ukakasi dhidi ya Baba wa Taifa.

2.Ni kweli TL anapinga muungano serikali 2. Yeye anapendekeza muungano wa serikali 3 baada ya wananchi kuulizwa.

Hayo mambo mawili yanaweza yasiwe kikwazo ikiwa unampambanisha na mgombea ambaye ametoa kauli mbaya zaidi kushinda ile aliyotoa TL dhidi ya sera za Mwalimu.

Pia kuhusu muungano hili ni eneo ambalo kwa huku Tanganyika wako watu wachache sana wenye uwezo wa kulichambua na kulijengea hoja kumzidi TL.

Kwa maoni yangu, TL akipewa nafasi anaweza kubadilisha mtizamo wa wananchi kuhusu muungano and the way forward. Hoja yake ya muungano wa serikali 3 siyo ngeni masikioni mwa waTz.
 
We jamaa inabidi ukapimwe akili!
Mbona unaandika kama mtu fulani mwenye power ya kuamua nani atakuwa nani kwenye Nchi hii! Ipo kama vile wewe ukishasema ndio final, you can decide for the state.... Or you have power of attorney to decide nani awe president wa nchi hii
Hio ni perception na fear yako tu...mimi nimeandika kama hoja tu ya kuijadili.
 
Lissu hana kosa lolote alilolifanya katika kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania. Ni watetezi wa wahuni na mafisadi tu ndiyo wanaumuona Kamanda ana makosa.

Kwa hoja ya CCM kumuogopa lissu sio hoja!
Hoja ni makosa anayofanya Lissu
 
Hilo unaloliita "fisadi kuu"ni lipi hilo?Kwa nini fisadi hilo msilitupe korokoroni katika ile mahakama yenu ya mafisadi iliyogeuzwa makazi ya popo mbwa,vimbulu na mapaka shume?

Bahati mbaya kwako unajaribu kuihadaa nafsi yako mwenyewe!Hivi kiongozi wa chini anawezaje kuwa " fisadi kuu"kwenye uchafu uliojadiliwa na kupitishwa na Cabinet iliyo chini ya uenyekiti wa Rais wa nchi?Kwa nini "fisadi kuu" asiwe yule mwenye maamuzi ya Mwisho juu ya mambo yote yahusuyo nchi na ambaye ndiye aliyesimamia maamuzi yote ya kipumbavu yanayoligharimu Taifa letu hadi leo?

Nafikiri "fisadi kuu"ni lile lililojianzishia ACACIA yake na kujimilikisha mgodi wa kiwira kinyume na sheria za nchi,kupitia fisadi hilo ndimo kulimozaliwa uchafu wote ambao wagonga meza wa wakati huo na ambao pia walikuwa sehemu ya Cabinet,leo wanatulazimisha tuwaone wazalendo kwa kutuhadaa kuwa wanapambana na wahujumu uchumi wakati mikono yao ilishiriki 100% katika kuwapokea majambazi wa kiuchumi wanaopora Rasilimali zetu.

Eti leo mtu anakurupuka kwa mwendokasi wa ukilaza wa " permanent head disorder" ya mazao ya korosho na kutuuliza nani aliyeturoga huku akijuwa fika tumerogwa na ccm na serikali yake na yeye alishiriki kuitikia "tawile" katika vikao vya kishirikina vya kuiroga nchi yetu kiuchumi,kutuuliza tumerogwa na nani wakati wewe ni sehemu ya wachawi wenyewe yaweza kuwa ni kejeli ya kiwango cha lami!

Eti kuna watu wanashangilia na kusifia kuwa ........,hivi hamjuwi kuwa hao mnaowavika ushujaa leo mikono yao imejaa damu za hatia kwa kuunyonga utajiri wetu kupitia chama na serikali ileile ya ccm?Wapumbavu wanawageukia kina TL na kuwasakama utadhani TL ndiye aliyelifikisha Taifa hapa lilipo,ajabu zaidi tukihoji na kuomba katiba ibadilishwe ili ituruhusu kuwapiga mawe hadi kufa viongozi wakuu wawili walioshiriki,kusimamia na kubariki Wizi huu,anatokea kiongozi mwingine ambaye pia alikuwa mgonga meza na mwana cabinet anafura na kuliagiza bunge liwafurushe wote watakaohoji uadilifu wa viongozi wastaafu na yeye atahitimisha kwa kuwadhibiti ndani ya dk5 pale watakapojaribu kupaza sauti zao nje ya bunge.

Mwenye akili timamu hawezi kuchukuliwa na hadaa hii ya kiwango cha lami,atahoji na kudadisi ujasiri huu wa kilaghai umetoka wapi na utatufikisha wapi ikiwa anayeusimamia ujasiri huo ameshajiapiza kutofukua makaburi?

Nitakuwa wa Mwisho kuimba na kusali sala za "litania ya watakatifu" ili kumtukuza mtakatifu wa ccm aliyeshiriki kulihujumu Taifa,lakini leo anajifanya yeye ni "malaika wa nuru" aliyeletwa kuja kulitoa Taifa letu gizani.Mimi si sehemu ya wanafiki na sidanganyiki kipumbavupumbavu.
Muulize Zitto,Kubenea,Slaa,Mnyika,Mbowe,Msigwa na Lissu watakueleza Fisadi kuu ni nani!

Waulize kwa nini hawakwenda mahakamani ?

Wagonga meza wa wakati ule ni kina nani haswa?Unawaaachaje wakuu wa wapeleka miswada au niwaite wasimamizi wa shughuli za serikali bungeni wa wakati ule yaani Lowasa na Sumaye?nao unawaita wazalendo au wanamabadiliko au wakombozi??

Hadaa iliyo kubwa ni hii ya kukataa kuwa anayetuibia sio mwizi na tusimguse kwani ni hatari...ni hadaa ya namna hii hii iliyonitenganisha na lissu kwa kusema fisadi kuu sio fisadi tena.
 
meningitis ,

1. Ni kweli TL aliboronga alipotoa maneno ya ukakasi dhidi ya Baba wa Taifa.

2.Ni kweli TL anapinga muungano serikali 2. Yeye anapendekeza muungano wa serikali 3 baada ya wananchi kuulizwa.

Hayo mambo mawili yanaweza yasiwe kikwazo ikiwa unampambanisha na mgombea ambaye ametoa kauli mbaya zaidi kushinda ile aliyotoa TL dhidi ya sera za Mwalimu.

Pia kuhusu muungano hili ni eneo ambalo kwa huku Tanganyika wako watu wachache sana wenye uwezo wa kulichambua na kulijengea hoja kumzidi TL.

Kwa maoni yangu, TL akipewa nafasi anaweza kubadilisha mtizamo wa wananchi kuhusu muungano and the way forward. Hoja yake ya muungano wa serikali 3 siyo ngeni masikioni mwa waTz.

Hayo ni makosa niliyoyaona hapo kabla na hata mimi sikuyajali sana..ingawa kuna makosa aliyoendelea kuyafanya baada ya hapo...ndio msingi wa mimi kuja na thread hii.
 
Niliwahi kumpigia chapuo Ndugu Tundu lisu kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliotakiwa kushika Uongozi waTaifa hili mwaka 2015 kama kijana na kama mtu mwenye msimamo ulio thabiti..sikukosea bali yeye mwenyewe ameshindwa kujitambua na kujipanga na hatimaye kuipoteza sifa hiyo adimu kwa sababu zifuatazo na ambazo zitaendelea kujitanabaisha kadri muda unavyojiri.

1-Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.

2-Tundu lissu haamini katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar na huu ni uvunjifu mkubwa wa katiba.

3-Tundu lissu alikosea sana kukubali kuwa mmoja wa wanachadema waliompokea mtuhumiwa mkuu wa ufisadi lowassa na hatimaye kugeuka kuwa mtetezi wake...leo hii lowassa hii lowassa amempinga kuhusu swala la hatua za Rais dhidi ya makanikia.

4-Tundu lissu amekosea tena kutokana na hulka yake ya jazba na arrogance kwa kukinzana na swala la kitaifa la juhudi za Magufuli katika kuliondoa Taifa kutoka mikono ya wizi wa mabepari.

5-Tundu lissu ameshindwa kuwa na msimamo thabiti na wa kiadilifu dhidi ya viongozi wa chama chake mfano Mbowe ambao ametuhumiwa kwenye ukwepaji kodi,madawa ya kulevya na uzinzi.

Kwa hayo machache nasikitika kumuona Tundu lissu akipoteza talanta na fursa adhimu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Pengine Tundu lissu angekuwa ndani ya CCM ingewezekana kufichwa kama hazina ili asiingie kwenye makosa ya kijinga ambayo yamemgharimu.

Iam sorry my broda TL but these are bitter medicines and we all have to swallow!

Niliwahi kuandika juu ya Tundu lissu....mwaka 2015 kabla ya gia za angani....Tofauti yangu mimi na yeye kwa sasa imekuja kwenye msimamo aliouchukua dhidi ya fisadi mkuu kwani naamini ndicho kilichombadilisha Tundu Lissu na ambacho kimembadilisha forever and ever!

Again sikukosea kutokana na muda niliokuwa nikiandika thread ile lakini pia kutokana na aina ya wagombea waliokuwa wakipigiwa upatu ndani ya CCM(Ukimuondoa Magufuli) na ndani ya Ukawa Original.

Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)
acha maneno mengi kama unataka kumuongelea lissu ebu kwanza kapitie ripoti ya tume ya bomani na tume ya osoro then utuletee dhamani za madini tuone izo tofauti zake anazosema lissu ndo umpe credit au umkosoe mana mwenzio anasoma na kuchambua hoja we unaleta upenzi

usipange nani apendwe kama kuna tatizo kwa nyerere na ni kwel lissu kalisema sio kosa hata nyerere mwenyewe aliomba ladhi kama kuna makosa aliwafanya na kung'atuka badae utataka hata mkapa sitajwa wakati wakina chenge wakisema mpaka na kikwete ndo wausika wakuu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lissu hana kosa lolote alilolifanya katika kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania. Ni watetezi wa wahuni na mafisadi tu ndiyo wanaumuona Kamanda ana makosa.
Maslahi ya Tanzania na watanzania ni yapi unapoongelea ufisadi na baba wa ufisadi?

Maslahi ya Tanzania na watanzania ni yapi unapoongelea ripoti za Makinikia na wizi wa acsia!?
 
acha maneno mengi kama unataka kumuongelea lissu ebu kwanza kapitie ripoti ya tume ya bomani na tume ya osoro then utuletee dhamani za madini tuone izo tofauti zake anazosema lissu ndo umpe credit au umkosoe mana mwenzio anasoma na kuchambua hoja we unaleta upenzi

usipange nani apendwe kama kuna tatizo kwa nyerere na ni kwel lissu kalisema sio kosa hata nyerere mwenyewe aliomba ladhi kama kuna makosa aliwafanya na kung'atuka badae utataka hata mkapa sitajwa wakati wakina chenge wakisema mpaka na kikwete ndo wausika wakuu
Tume ya Bomani ilifanya kazi yake...nzuri kwa kiasi chake na kwa wakati wake.

Tume ya bomani haikuongelea madini nyeti call tgem strategic metals...tume ya Bomani ilipata data zake kutoka kwenye makaratasi ya GST...

Tuma ya Bomani ilikuwa na members baadhi wakiwa ni sehemu ya tatizo mfano bi Kejo.

Kwa ufupi tume ya bomani ni outdated.

Isitoshe hata ukitumia matokeo ya Tume ya bomani kamwe huwezi ukasimama upande wa acasia ukaonekana ni mwenye akili timamu kwa watanzania...hapo ndipo kosa la lissu linapokuja.
 
You're not serious can you make any difference between Lowassa and the intended recipient in changes team
 
Huyajui maslahi ya Tanzania na Watanzania? Nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali lakini pamoja na miaka 56 ya uhuru hakuna cha maana chochote kile kwenye sekta yoyote ile ambacho ni cha kujivunia huku viongozi wakitumia nyadhifa zao kujitajirisha kwa njia za haramu!?

Huu utajiri mkubwa wa nchi badala ya kuwanufaisha Watanzania wote kwanini uendelee kuwanufaisha watu wachache tu huku mamilioni wakiendelea kuishi katika ufukara mkubwa wa kutisha hata mlo wao mmoja hawaujui utatoka wap?

Maslahi ya Tanzania na watanzania ni yapi unapoongelea ufisadi na baba wa ufisadi?

Maslahi ya Tanzania na watanzania ni yapi unapoongelea ripoti za Makinikia na wizi wa acsia!?
 
Mleta uzi anafedhehesha nafsi yake kwa mwandiko wa mikono yake. Yaani kwa ufupi anaachia mashuzi halafu anajifunika gubigubi. Sasa sijajua ni nani anapata dhahma ya ubabaishaji wake!
 
Huyajui maslahi ya Tanzania na Watanzania? Nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali lakini pamoja na miaka 56 ya uhuru hakuna cha maana chochote kile kwenye sekta yoyote ile ambacho ni cha kujivunia huku viongozi wakitumia nyadhifa zao kujitajirisha kwa njia za haramu!?

Huu utajiri mkubwa wa nchi badala ya kuwanufaisha Watanzania wote kwanini uendelee kuwanufaisha wata wachache tu huku mamilioni wakiendelea kuishi katika ufukara mkubwa wa kutisha hata mlo wao mmoja hawaujui utatoka wap?
Ni kweli wapo viongozi wanaotumia nyadhifa zao kujineemesha wao tu...wapo wanaoendelea kufanya hivyo hadi leo na wapo waliofanya hivyo kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuendelea kujineemesha na unyonyaji walipokuwa wanashika madaraka...Fisadi kuu na yule bwana Zero ni sehemu ya hao.

Pia ni vyema kuanza kujenga utamaduni wa kuangalia kwa umakini wa hali ya juu maslahi ya Taifa pindi na hususani adui yetu anapokuwa ni wa nje ya Taifa au anapokuwa ni kibaraka wa watu wa nje.

Ni vyema kutambua kuwa ushindi katika vita hii utanufaisha watanzania bila kujali nani ni wa itikadi gani.
 
meningitis : Swali la kujiuliza je lissu anamkubali Nyerere?

JIBU: Anamkubali kama kiongozi aliyezingatia miiko na maadili ya uongozi.
Anatofautiana naye ktk masuala ya demokrasia, haki za binaadamu, na aina ya muungano unaoendana na mazingira ya sasa ya Tanganyika na Zanzibar.

meningitis:Lissu anaukubali muungano?

JIBU: anaukubali muungano wa serikali 3 baada ya wananchi kuulizwa kupitia KURA YA MAONI.

meningitis: Lissu anamkubali lowassa?

JIBU: Ndiyo. Na amempigia kampeni.
EL hata kama ni fisadi haimaanishi kwamba TL naye ni fisadi.

meningitis:Lissu anaitetea Acacia?

JIBU: Hapana. Historia ya Lissu ktk kupigania Tz tunufaike na rasilimali zetu inajulikana na ni ya kupigiwa mfano.
 
Lissu hata siku moja hawezi kutumika na Taifa lolote lile ili awe kibaraka wao hata kwa sekunde moja.

Kamanda wangemsikiliza katika upingaji wake was mikataba ya kifisadi tangu late 90s labda nchi yetu miaka 20 baadaye ingekuwa na maendeleo makubwa sana kupitia utajiri wake wa rasilimali lakini wahuni na mafisadi wa CCM wakampinga kwa kila namna leo matokeo yake tunayajua.

Ni kweli wapo viongozi wanaotumia nyadhifa zao kujineemesha wao tu...wapo wanaoendelea kufanya hivyo hadi leo na wapo waliofanya hivyo kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuendelea kujineemesha na unyonyaji walipokuwa wanashika madaraka...Fisadi kuu na yule bwana Zero ni sehemu ya hao.

Pia ni vyema kuanza kujenga utamaduni wa kuangalia kwa umakini wa hali ya juu maslahi ya Taifa pindi na hususani adui yetu anapokuwa ni wa nje ya Taifa au anapokuwa ni kibaraka wa watu wa nje.

Ni vyema kutambua kuwa ushindi katika vita hii utanufaisha watanzania bila kujali nani ni wa itikadi gani.
 
meningitis : Swali la kujiuliza je lissu anamkubali Nyerere?

JIBU: Anamkubali kama kiongozi aliyezingatia miiko na maadili ya uongozi.
Anatofautiana naye ktk masuala ya demokrasia, haki za binaadamu, na aina ya muungano unaoendana na mazingira ya sasa ya Tanganyika na Zanzibar.

meningitis:Lissu anaukubali muungano?

JIBU: anaukubali muungano wa serikali 3 baada ya wananchi kuulizwa kupitia KURA YA MAONI.

meningitis: Lissu anamkubali lowassa?

JIBU: Ndiyo. Na amempigia kampeni.
EL hata kama ni fisadi haimaanishi kwamba TL naye ni fisadi.

meningitis:Lissu anaitetea Acacia?

JIBU: Hapana. Historia ya Lissu ktk kupigania Tz tunufaike na rasilimali zetu inajulikana na ni ya kupigiwa mfano.
Mkuu unajua kujitetea sorry kumtetea lissu kisiasa haswa!

Bahati nzuri kabla sijaandika ile thread yangu ya kipindi kile nilichukua muda kumchimba,kumfuatilia na kudadisi mengi juu ya lissu...nilimkubali na mapungufu yake ambayo by then yalikuwa machache ya kuvumilika...lakini pia kwa kipindi kile au niseme kwa muhula huu wa kisiasa na kwa kadiri nchi ilipofikia tulihitaji mtu bandidu,arrogant au mjuvi ili nchi ivuke salama...ndani ya CCM kati ya wote waliokuwa wakisemwasemwa sana hakukua na mtu wa namna hiyo...ndani ya Chadema kulikuwa na Dr Slaa ingawa kwa maoni yangu sifa ya ujana hakuwanayo (hii ilikuwa ni sifa muhimu kimkakati kwa Upinzani)...
Kwa ufupi nilimfuatilia na kumjua lissu vilivyo...

Hivyo ninapokuambia kuwa Lissu hamkubali Nyerere ninamaanisha...Lissu anamchukia Nyerere toka utotoni...Jaribu kufuatilia historia yake,Mazungumzo yake na yote yanayohusu era ya Nyerere utagundua hilo.

Kuhusu Muungano ...msimamo wa lissu umechagizwa na chuki dhidi ya Nyerere...He is just utilizing the available opportunities za kuuvunjilia mbali muungano ...sio tu eti Serikali mbili au tatu au maoni ya Tume ya warioba.

Kuhusu lowassa :Hilo ndio kosa kuu lililoniudhi hasa na ndio kosa lililoondoa credibility ya Lissu...ndilo kosa lililotuhakikishia kuwa pesa ni mwisho wa matatizo(read between the lines)

Lissu alimuita lowassa fisadi kwa tone ile ile anayoitumia kuwaita CCM majizi.Lissu anaujua ukweli kuhusu ufisadi lakini kachagua kuutetea...Shame!

Hivi utawezaje kumtetea na kumsafisha fisadi kama wewe si fisadi?

Kuhusu kuitetea Acacia:Tumesikia kuhusu mienendo ya kutafuta ushilawadu kutoka Tume...kiasi cha kumulikwa na camera.Tumeona matamko
Lissu
 
Back
Top Bottom